TGIF: Vodacom na misaada

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
886
376
Something light to start the weekend.
NINAWAFAGILIA SANA VODACOM kwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii chini ya Vodacom Foundation na mwenyekiti/ mkurugenzi wa Foundation hiyo kwa ubunifu walionao mara nyingi tunaona wametoa misaada kwa yatima, wasiojiweza madawati na udhamini mbalimbali wa michezo, elimu na nyanja zingine.
Lakini pia inafaa kujiuliza je hela hizi zinaweza pia kuingia kwenye kodi na wenyewe tusambaze huduma hizi ?
Nakumbuka muda sio mrefu Ethiopia na sasa Rwanda walikuwa na majadiliano na kampuni kubwa ya kahawa ya STARBUCKS juu ya manunuzi ya kahawa yao. Starbucks walisema wao watanunua kilo moja ya kahawa kwa dola moja na pia watasaidia kujenga mashule na barabara kwenye sehemu watakazonununua kahawa. Ethiopia walikataa, wakasema wao wanataka dola 3 kwa kila kilo na barabara na mashule watajenga wao wenyewe.
Lakini jirani zetu DRC wao walifuata model nyingine, wao waliwapa China madini ya thamani ya $ bilioni 10 kwa makubaliano kwamba China iwajengee mfumo mpya wa mabarabara na mfumo mpya wa reli kwa nchi nzima.

Utaratibu gani unafaa kwa nchi yetu? Kama tumeshindwa kukusanya kodi itakiwavyo, kama wawekezaji wamejenga viwanja vya ndege kwenye maeneo waliyopewa bila kuwepo uhakiki wa kuratibu mali wanayochuma,Je ni bora tikijua mwekezaji fulani akija basi atajenga barabara fulani, au shule fulani au hospitali fulani na kwa muda fulani ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom