Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,337
Nimekaa hapa na kuanza kujumlisha. I mean, nimeanza kufanya hesabu za kujumlisha na zikanishinda. Nilikuwa najaribu kujumlisha vitu vifuatavyo:
a. Ni ziara ngapi za nje ambazo Rais Kikwete amezifanya ndani ya mwaka huu uliopita.
b. Katika msafara wa Rais ni watu wangapi ambapo anasafiri nao. Hapa nina maana walio kwenye presidential entourage. Wale wanaotakiwa kuwemo kwenye safari yoyote ya Rais kwenda nje
c. Ni maafisa wangapi wa ziada wanaoenda pamoja na Rais aidha kama sehemu ya ujumbe maalum au kudandia lift ya kutalii?
d. Ni Siku ngapi kwa ujumla amekuwa nje ya nchi ukilinganisha na alizokuwa ndani ya nchi.?
Hesabu zenyewe:
1. Wanapofikia kwenye miji anayofikia Rais hufikia hoteli gani na zinachargi kiasi gani kwa siku?
2. Je ujumbe wa Rais hufikia kwenye hoteli gani na wanachukua standard gani za vyumba? (Alipokuja Rais Bush hapa Detroit mara tu ya Septemba 11, nilikuwa nafanya kazi hoteli moja ambapo maafisa wa usalama walifikia. Wao walichukua vyumba "Standard" na kwa vile vilikuwa ni vingi wakapewa discount maalum - sijui kama wa kwetu wanafanya hivyo?)
3. Walio katika msafara wa Rais huwa wanalipwa posho ya kiasi gani kwa siku. Kuna ndugu mmoja katika ziara ya mwisho alikuwa na kama dola 50,000 cash kuja kuangalia ununuzi wa Cadillac..!
Sasa mwenye kujua hizo namba atumegee halafu tuanza kujumlisha tujue zimetumika kiasi gani?
Halafu:
Tulinganishe na Marais wengine wa eneo letu, Museveni, Kibaki, Kagame, Ndayizeze, bwana Mdogo Kabila, Mwanawasa, Guebuza na Mutharika.
Tukishaingiza gharama zote hizo (tunazozilipia) tulinganishe na mapato yatokanayo na safari hizo.
Halafu tufanye Equation hii:
Jumla ya Matumizi ya Ziara za Rais - Misaada na mikopo toka alikokwenda = Faida kwa Taifa.
Endapo Faida kwa Taifa ni Hasi basi tumepata hasara, na kama ni Chanya basi tumepata faida. Faida hiyo inaweza isiwe kubwa kutokana na offset ya gharama za kumsafirisha Rais na wasaidizi wake.
Haya wa ndugu "tuselebuke"..!