TGIF - Unajua hesabu za kujumlisha?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Nimekaa hapa na kuanza kujumlisha. I mean, nimeanza kufanya hesabu za kujumlisha na zikanishinda. Nilikuwa najaribu kujumlisha vitu vifuatavyo:

a. Ni ziara ngapi za nje ambazo Rais Kikwete amezifanya ndani ya mwaka huu uliopita.

b. Katika msafara wa Rais ni watu wangapi ambapo anasafiri nao. Hapa nina maana walio kwenye presidential entourage. Wale wanaotakiwa kuwemo kwenye safari yoyote ya Rais kwenda nje

c. Ni maafisa wangapi wa ziada wanaoenda pamoja na Rais aidha kama sehemu ya ujumbe maalum au kudandia lift ya kutalii?

d. Ni Siku ngapi kwa ujumla amekuwa nje ya nchi ukilinganisha na alizokuwa ndani ya nchi.?

Hesabu zenyewe:

1. Wanapofikia kwenye miji anayofikia Rais hufikia hoteli gani na zinachargi kiasi gani kwa siku?

2. Je ujumbe wa Rais hufikia kwenye hoteli gani na wanachukua standard gani za vyumba? (Alipokuja Rais Bush hapa Detroit mara tu ya Septemba 11, nilikuwa nafanya kazi hoteli moja ambapo maafisa wa usalama walifikia. Wao walichukua vyumba "Standard" na kwa vile vilikuwa ni vingi wakapewa discount maalum - sijui kama wa kwetu wanafanya hivyo?)

3. Walio katika msafara wa Rais huwa wanalipwa posho ya kiasi gani kwa siku. Kuna ndugu mmoja katika ziara ya mwisho alikuwa na kama dola 50,000 cash kuja kuangalia ununuzi wa Cadillac..!

Sasa mwenye kujua hizo namba atumegee halafu tuanza kujumlisha tujue zimetumika kiasi gani?

Halafu:

Tulinganishe na Marais wengine wa eneo letu, Museveni, Kibaki, Kagame, Ndayizeze, bwana Mdogo Kabila, Mwanawasa, Guebuza na Mutharika.

Tukishaingiza gharama zote hizo (tunazozilipia) tulinganishe na mapato yatokanayo na safari hizo.

Halafu tufanye Equation hii:

Jumla ya Matumizi ya Ziara za Rais - Misaada na mikopo toka alikokwenda = Faida kwa Taifa.

Endapo Faida kwa Taifa ni Hasi basi tumepata hasara, na kama ni Chanya basi tumepata faida. Faida hiyo inaweza isiwe kubwa kutokana na offset ya gharama za kumsafirisha Rais na wasaidizi wake.

Haya wa ndugu "tuselebuke"..!
 
Mungu wangu; hivi Rais na maofisa wote wana bajeti zao za kazi zao. Rais anapokwenda nje ya nchi kuna bajeti karibu nne zinahusika na zote ni za kisheria (zilipangiwa fungu). Kuna bajeti ya Ofisi ya Rais, Bajeti ya Mambo ya Nchi za Nje, na Bajeti ya Ofisi au Wizara husika. Hivyo, Waziri anaposafiri na afisa toka Wizara ya Kilimo, siyo ikulu inayolipa bali ni toka bajeti ya wizara hivyo.

Hivyo, kaka usitafute mchawi, hakuna. Kama hujui hesabu unaweza kuwaacha wengine tu wakufanyie lakini miye naona unatafuta sifa za bure tu kwenye hili la ziara.

asante.
 
Yaani maadamu bajeti ina fungu basi ni kutumbua tu bila kujiuliza safari hizi zimeleta faida gani? Kwani ni bajeti ya kutalii, au?
 
Nakumbuka suplementary budget ya mwaka jana, pamoja na mambo mengine, zaidi ya Shilingi bilioni 20 zilikua kufidia ziada iliyotumika kwa safari za viongozi... maana katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo walitumia kwa safari ziada ya sh bilioni 20 na ushee hivi....
 
Mungu wangu; hivi Rais na maofisa wote wana bajeti zao za kazi zao. Rais anapokwenda nje ya nchi kuna bajeti karibu nne zinahusika na zote ni za kisheria (zilipangiwa fungu). Kuna bajeti ya Ofisi ya Rais, Bajeti ya Mambo ya Nchi za Nje, na Bajeti ya Ofisi au Wizara husika. Hivyo, Waziri anaposafiri na afisa toka Wizara ya Kilimo, siyo ikulu inayolipa bali ni toka bajeti ya wizara hivyo.

Fikiria zaidi, ili siku moja uje kujua kuwa fedha zote hizi ulizotaja toka wizara mbali mbali hakuna mtu aliyekuja nazo toka nyumbani kwake, ni za walipa kodi.

Ni muhimu kujua faida na hasara ya kuzitumia kwenye safari..."tuache uvivu wa kufikiri", B.W. Mkapa, Rais Mstaafu wa URT.
 
mzee mwanakijiji please Soma pm, kuna mtu ana shida na wewe haraka na muhimu
 
Mungu wangu; hivi Rais na maofisa wote wana bajeti zao za kazi zao. Rais anapokwenda nje ya nchi kuna bajeti karibu nne zinahusika na zote ni za kisheria (zilipangiwa fungu). Kuna bajeti ya Ofisi ya Rais, Bajeti ya Mambo ya Nchi za Nje, na Bajeti ya Ofisi au Wizara husika. Hivyo, Waziri anaposafiri na afisa toka Wizara ya Kilimo, siyo ikulu inayolipa bali ni toka bajeti ya wizara hivyo.

Hivyo, kaka usitafute mchawi, hakuna. Kama hujui hesabu unaweza kuwaacha wengine tu wakufanyie lakini miye naona unatafuta sifa za bure tu kwenye hili la ziara.

asante.

Bibie,
Tunachohangaika nacho hapa ni mizania (balance sheet), kati ya kile tunachopoteza kwa kusafiri kwenda kukopa (ama kutalii) na kile kinachoingia kutokana na safari hizo. Siyo kwa sababu pesa ipo kwa ajili ya masurufu ya safari basi safari zinaandaliwa tu! Hapana!
Ndio sababu tulimuuliza Lowassa alipokwenda kushangaa mashamba ya kabichi New Zealand, huku msafara wake ukiwa hauna mkulima hata mmoja kutoka kule kabichi zinakolimwa Tanzania. Ziara za mkuu zimekuwa kero, yaani haupiti mwezi, safari! Lazima tuhoji, kwa sababu pesa zinazoungua kulipia misafara na masurufu ni za sisi walipa kodi, kwa hiyo tuna haki ya kuuliza matumizi ya pesa zetu. Lazima tuhpji mizania.
Nadhani nimeeleweka.
 
Kuna rates mbali mbali zinzotumika serikalini.

Kuna wakuu ambao rate zao hazijulikani kulingana na rasimu za serikali. Isipokuwa najua rate ya kuanzia waziri Directors, na all senior staffs wanaposafiri njee ya nchi kwenye mji mikubwa kama NY, London, Paris na mingine ambayo hatel ni ghali wanalipwa USD 370/siku(per diem)ambayo ina include malazi na kila kitu. middle class wanalipwa 290/kwa siku (sizani madereva na junior staffs wengine kama wanasafiri njee so to ignore kwa sasa).

Ikitokea serikali imegharamia malazi wanasema (Full booked)then wanalipwa 60% ya hizo rate wanazopaswa kulipwa.

Mwanzoni mwa mwaka huu Kikwete na deligation yake alifanya ziara kwenye nchi za Baltic na Scandinavia kwa siku 13, alikua na deligation ya watu 37 (bodyguards, Usalama, mawaziri 3 including Karamagi, waandishi na wafanyabiashara included) na katika taratibu zao msafara wa rais na for security reasons wote mtakaa hotel moja ama zilizo karibu kama waliofikia hapatoshi.
 
Hata hivyo kuna baadhi ya safari zinazogharamiwa na wenyeji ambayo usafiri na malazi na hii nadhani ni kwa specific number of people.

Niliwahu kuwauliza baadhi ya waliokua kwenye msafara wa rais alipokuwa nchi za scandinavia kujua nani analipia gharama maana huyu bwana hakua mfanya kazi wa serikali na jibu ni kwamba employer wake analipia usafiri wa ndege tu mengine serikali.
 
Yaani bajeti ina fungu basi ni kutumbua tu bila kujiuliza safari hizi zimeleta faida gani? Kwani ni bajeti ya kutalii, au?

Majibu aina hii ni ya mtu mwenye harufu ya uvundo wa udokozi.
Fungu likiwepo basi ni nongwa, mnaweka mpaka Tumbiri wa mikumi kwenye misafara?
Fungu la wizara fungu la Ikulu yote ni mafungu ya serikali.
Utetezi wako wa fungu haujengi hoja ya kujibu tuhuma za ubadhirifu wa safari za rais.Hayo mafungu ya kusafiri nje toka ikulu na wizarani ni makubwa kuliko bajeti ya nchi kiasi kwamba hata usafiri vipi na kiwingu kipi fungu halizidiwi uwezo?

Eti kuna fungu! Nani asiye jua hilo?
 
Mungu wangu; hivi Rais na maofisa wote wana bajeti zao za kazi zao. Rais anapokwenda nje ya nchi kuna bajeti karibu nne zinahusika na zote ni za kisheria (zilipangiwa fungu). Kuna bajeti ya Ofisi ya Rais, Bajeti ya Mambo ya Nchi za Nje, na Bajeti ya Ofisi au Wizara husika. Hivyo, Waziri anaposafiri na afisa toka Wizara ya Kilimo, siyo ikulu inayolipa bali ni toka bajeti ya wizara hivyo.

Hivyo, kaka usitafute mchawi, hakuna. Kama hujui hesabu unaweza kuwaacha wengine tu wakufanyie lakini miye naona unatafuta sifa za bure tu kwenye hili la ziara.

asante.

Watu kama hawa wenye fikra za mwaka 47 ndio wanaotaka tuamini kwamba kila kitu ni shwari ndani ya nchi yetu. Hatuna haki ya kuhoji chochote kile kinachofanywa na viongozi wetu hata kama hakina maslahi na nchi yetu. Kwa taarifa yako tu Watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 47, wanajua haki zao na pia wana haki ya kuhoji chochote kile kinachofanywa na viongozi wao, pia ujue fika kwamba kuhoji mambo mbali mbali haina maana tuna tafuta mchawi bali tunataka kujua je kuna manufaa gani kwa Tanzania katika maamuzi hayo.

Kikwete sasa hivi uongozi wake umelegalega sana na hii safari ya Marekani haina umuhimu mkubwa kwa nchi yetu. Kama angekuwa makini angetakiwa kudelegate safari hii kwa kiongozi mwingine ili yeye ashughulikie matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupanga upya baraza lake la mawaziri ambalo katika kipindi alichokuwa madarakani cha miaka miwili limepwaya sana na kusubiri ripoti ya ukaguzi wa BOT ambayo tumeambiwa itatoka karibuni ili achukue hatua zinazostahili.
 
Haya ndiyo matatizo yetu sisi Wa TZ. Mtu mzima anathubutu kusema kila wizara ina fungu kama vile hizo pesa hazitokani na kodi zetu. Nina hofu mtu anayesema hivyo hajui kuwa analipa kodi kwa njia nyingi sana kiasi kwamba yeye anaendelea kuwa maskini huku akisema mafungu yalisha pangwa kwa hiyo acha watumie watakavyo!!!

Kumbuka kuwa yawezekana unakatwa asilimia 30 kwa ajili ya PAYE, 20% ya pesa inayobaki inaenda kwenye VAT, bado service charge ya TANESCO, bado kila kitu kimepanda ghalama kwa sababu mkku wa nchi anahitaji pesa nyingi ya kusafiri nje. Leo mtu mzima anasema mafungu yalisha pangwa...huu ni umbumbumbu tu wala hakuna lingine.

Tuna haki ya kujua kila sent ya nchi hii inavyotumika. Serikali kuu wasikazanie kusema wananchi wana haki ya kujua matumizi ya pesa ya halmashauri za miji, bali pia na pesa ya serikali kuu ikiwemo ya IKULU.

Fikiria haka katabia ka serikali yetu...kila siku wananchi wanatakiwa kuchangia kujenga shule, matibabu. Lakini hata siku moja hawakosi pesa za kufanya misafara ya nje na ndani ya nchi???

Inabidi tuamke na kudai haki yetu.
 
Haya ndiyo matatizo yetu sisi Wa TZ. Mtu mzima anathubutu kusema kila wizara ina fungu kama vile hizo pesa hazitokani na kodi zetu. Nina hofu mtu anayesema hivyo hajui kuwa analipa kodi kwa njia nyingi sana kiasi kwamba yeye anaendelea kuwa maskini huku akisema mafungu yalisha pangwa kwa hiyo acha watumie watakavyo!!!

Kumbuka kuwa yawezekana unakatwa asilimia 30 kwa ajili ya PAYE, 20% ya pesa inayobaki inaenda kwenye VAT, bado service charge ya TANESCO, bado kila kitu kimepanda ghalama kwa sababu mkku wa nchi anahitaji pesa nyingi ya kusafiri nje. Leo mtu mzima anasema mafungu yalisha pangwa...huu ni umbumbumbu tu wala hakuna lingine.

Tuna haki ya kujua kila cent ya nchi hii inavyotumika. Serikali kuu wasikazanie kusema wananchi wana haki ya kujua matumizi ya pesa ya halmashauri za miji, bali pia na pesa ya serikali kuu ikiwemo ya IKULU.

Fikiria haka katabia ka serikali yetu...kila siku wananchi wanatakiwa kuchangia kujenga shule, matibabu. Lakini hata siku moja hawakosi pesa za kufanya misafara ya nje na ndani ya nchi???

Inabidi tuamke na kudai haki yetu.
 
Halafu tufanye Equation hii:

Jumla ya Matumizi ya Ziara za Rais - Misaada na mikopo toka alikokwenda = Faida kwa Taifa.

Endapo Faida kwa Taifa ni Hasi basi tumepata hasara, na kama ni Chanya basi tumepata faida

Mzee MJJ
Nadhani equestion iwe hivi:-
Misaada na mikopo toka alikokwenda - Jumla ya Matumizi ya ziara za rais = Faida kwa Taifa
 
Lakini nani anakumbuka hasa alikwenda wapi na mara ngapi pengine hiyo itasaidia wataalamu wa hesabu kupata hiyo hesabu.. Lakini pia vipi Museveni, Kibaki na Kagame, huwa munawaona huko majuu kila mara?
 
Hivi hawa wazungu wana usahaulifu wa kiasi hicho? Maana mwanzoni walituambia anaenda kujitambulisha....
 
Back
Top Bottom