TFF ya Malinzi yashikishwa adabu

Yaani wewe ndio bure kabisa. Akikanusha Jenny Mro ndio unachukulia ni tamko rasmi la TFF? Yaani mdaiwa anakanusha na wewe unachukulia kama source ya habari? Ungesema TFF imekanusha hapo sawa. Jipangeni kumchangia YM hizo sh. 530M ili CAF, TFF, DRFA, Wachina na TRA wachukue chao. Ndio matokeo ya kuwa na uongozi usioelewa mambo!
Tumia akili kufikiria kidogo sio unaleta ushabiki kila kitu

1.Source ya hiyo habari ni nani TFF au CAF ?
2.CAF huwa wanahusiki na viingilio vya mechi ?
3.Kwenye mapato ya mechi kuna mgawo CAF wanapata ?
4.Mechi imechezwa Jumanne jioni taarifa imetoka jana jioni,CAF walikaa lini kupitia ripoti za wasimamizi ?
 
Kwa hiyo na huo uwanja ni wa Manji au baba yake na Manji. Unadhani huo ni uwanja wa Kaunda pale jangwani ama. Hebu tumia akili zako japo robo tu bwanamdogo.

Anaepanga viingilio vya mechi ni Yanga au msimamizi wa mashindano? Huwa ninachukizwa sana na mijitu inayoabudu watu na kushindwa kutumia akili zao.
Uwanja utalipwa kwani hiyo ni direct cost, siyo mpaka wa calculate asilimia
Ambulance italipwa
Hela ya usafi italipwa na hizo ni fixed costs
Mbona Msemaji wa Yanga jana aliongea vizuri tuu ndugu yangu

Let say uwanja hajaingia shabiki hata mmoja unadhani haulipiwi!!?

Kwa hiyo hizo ni pesa tofaut kabisa

Direct cost (fixed) yatalipwa

Makato (not fixed) hutokana na mapato ya uwanjani, soTFF hawapati kitu

Usitumie jazba mkuu mambo madogo haya
 
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) na
Shirikisho la Soka nchini (TFF), limeitaka
Yanga kulipa fidia ya gharama za mchezo
wake na TP Mazembe Sh milioni 530.
CAF na TFF imefikia hatua hiyo baada ya
Yanga kufuta kiingilio katika mchezo wao
huo wa makundi wa Kombe la Shirikisho
Afrika unaotarajiwa kuchezwa leo kwenye
Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na sasa
mashabiki wataingia bure.
Katika kikao chao cha jana kilichofanyika
kwenye hoteli ya Coral Beach jijini na
kukutanisha maofisa wa CAF, uongozi wa
TFF, Polisi, Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo na viongozi wa Yanga
wakiongozwa na Katibu mkuu wa klabu
hiyo, Baraka Deusdetit wametakiwa kulipa
kiasi hicho cha fedha kama gharama za
mchezo.
Makato katika mchezo huo wa hatua ya
makundi Kombe la Shirikisho asilimia 15
ya fedha hizo zitaenda CAF, asilimia 15
nyingine gharama ya uwanja, TFF asilimia
tano, Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
asilimia 10, na Chama cha soka Dar es
Salaam (DRFA) asilimia tano.
Tayari Yanga ilikuwa imechapisha tiketi
31,000 ambazo zingeuzwa kwa Sh7,000
ambazo zingeingiza Sh 217,000,000 huku
zile za Sh 25,000 zilikuwa zimechapishwa
tiketi 8,200 zingeingiza Sh milioni 205
huku VIP zilikuwa tiketi 5,000 ambazo
zingeingiza Sh milioni 150 jumla ya fedha
zote ambazo zingepatikana katika
mchezo huo ni Sh milioni 572.
Pia Yanga wametakiwa kuingiza
mashabiki wasiozidi 40,000 wakizidi
kiwango hicho mchezo huo utafutwa na
Yanga watalazimika kuwajibishwa.
Sheria ya mtandao ilianzishwa kwa ajili ya wazushi kama nyie
 
IMG_20160630_160228_749.JPG
 
Yanga walichofanya ni kama kwa mfano kupanga kiingilio shilingi moja. Wako sawa.
 
Yani malinzi na tff yake nimewaona watu wa ajabu sana, yani kila wakiona thread huku jf wanapata hasira, wakihojiwa na vyombo vya habari wanakosa majibu.

Leo Msabaha kamtwanga swali malinzi ila badala ya kujibu akaishia kujitapa anajua haya mambo mara ooh hababaiki mwisho nayeye akamwuliza Msabaha kua anatoka chombo gani cha habari, jamaa akapewa jibu zuri tu, "Naitwa Msabaha wa radio Times FM". Kupe kusikia hivyo akachoka na kusema hana la kujibu.

Nashauri malinzi na katibu wake waache jaziba kwenye soka letu na huo umaimuna wao waupeleke walikotoka huko kwenye ndondi.

Jamal Malinzi nuna tena
 
Mkuu bila shaka umenifananisha na mashabiki wa yanga. Utakua hauko sahihi, mimi si mshabiki wa yanga ila ni mpinga ukupe na unyonyaji unaofanywa na tff. Kama utafuatilia vizuri kwa sasa vilabu vingi vina mgogoro na tff ila yanga ndo angalau wameonyesha uthubutu wa kupambana na upuuzi wa tff. Kwa hiyo hapa nazungumzia unyonyaji wa kupe la tff kwa vilabu vya soka Tanzania.
Leo malinzi kadai kuanzia mechi ijayo wao ndio watakaosimamia viingilio na utaratibu wote wa kuwapokea waamuzi na timu itakayocheza na Yanga!kiukweli kanishangaza sana,km ni hivyo hao tff wakapange hadi line up ya wachezajibwa Yanga
 
Leo malinzi kadai kuanzia mechi ijayo wao ndio watakaosimamia viingilio na utaratibu wote wa kuwapokea waamuzi na timu itakayocheza na Yanga!kiukweli kanishangaza sana,km ni hivyo hao tff wakapange hadi line up ya wachezajibwa Yanga
Tff ni maskini wa akili na oesa pia
Yaan ni wakuwapinga tuuu
 
Umesahau na POINT NI 0.
Ila hii 0 ya point haigawanywi ni ya Yanga peke yao.
MANJI alijua ule ni msiba na msibani watu hawatoi kiingilio.
Ndio mukome kuacha kazi zenu alfajiri kwenda uwanja wa taifa.
Toka lini gongo wazi na mpira wa kimataifa.
Hiyo ndio faida ya kununu marefa na timu ktk ligi yenu ya hapa.
Munawaonea kina Ndanda na Mgambo na marefa wenu njaa mukitia pua tu kwa timu za nje munachezea kichapo.
Simba pia wanaonewa wamekuwa kikundi cha ushangiliaji kwa sasa timu hamna
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom