Yanga yalia na TFF yataka iwasaidie hali yao ngumu kifedha

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,551
1,777
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Matawi nchini, Bakili Makele, umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uwalipe fedha zao haraka wanazozidai.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa TFF iliwakata Yanga kiasi cha pesa ambazo ni zaidi ya milioni 200 kupitia VAT baada ya kuingiza mashabiki bure katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.

Yanga iliingiza mashabiki bure wakati huo ikiwa chini ya Mwenyekiti wake, Yusuph Manji, ambaye alilipia gharama zote za tiketi Juni 18 2016 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Makele ameutupia lawama uongozi wa TFF akisema kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa ilihali wanajua klabu inapitia wakati mgumu hivi sasa haswa katika suala la kuyumba kiuchumi.

Ameongeza kwa kusema kuwa wao wanatakiwa wailee Yanga kama baba wa soka la nchi hii kuliko kuzidi kuikata fedha na kuzidi kuikandamiza.

Aidha, Makele amesema TFF wamekuwa wakifanya utamaduni huo kuzidi kuifanyia dhuluma timu hiyo na pia akieleza hata fedha za mdhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom kuwa wamebaniwa kupewa.

Mbali na fedha za mdhamini, Makele amefunguka pia kuhusiana na kutopokea vifaa vya CAF kwa ajili ya mashindano ya kimataifa kwa kuilaumu TFF kuwa inahusika kwa maana vinapitia kwao.

Kiongozi huyo wa matawi amewaomba TFF chini ya Rais Wallace Karia, wabadilike na warejee katika usahihi wa ujabikaji ili walitendee haki soka la Tanzania wakiwa kama mlezi mkuu.

Mbona ana makelele halafu hajui hata kusoma?
Who TF is he, mpaka asome hiyo kitu? Kwanini asimuachie public relations secretary?
Halafu kwanini Yanga haisemi inahitaji kiasi gani cha fedha? Siyo tu useme tuna hali ngumu.
 
Ameiandika Clement Sanga baada ya kusikia anatakiwa aitishe uchaguzi. Huyo ni mjumbe tu
 
Dah aisee. Hii Yanga kama itendelea na ukata kiasi hicho huenda itashuka daraja la kwanza.. Hali ni mbayaa mno
 
Mbinu pekee ya kuiondoa Yanga kwenye utamaduni wake wa kubeba NDOO kila msimu ni kwa kuihujumu kiuchumi. Natabiri kuwa haya yataendelea hadi dirisha la usajili litakapofungwa ili kuhakikisha Yanga inakimbiwa na wachezaji.
 
Ameiandika Clement Sanga baada ya kusikia anatakiwa aitishe uchaguzi. Huyo ni mjumbe tu
Mjumbe wa nini brother?
Watu kama hao ndio wanaojichukulia madaraka mikononi.
We muangalie jinsi katibu uenezi alivyo kwenye sura yake tu inaonyeshwa hapendezewi na huyo mzee kutoa taarifa. Huyo mzee ni kama mkuu wa genge fulani la maninja na watu kama hao hawatufai Yanga.
Huyo mzee asirudie tena kuongea mambo ya Yanga na vyombo vya habari.
Yanga inajulikana Africa kwa sababu ya makatibu uenezi wa klabu ya Yanga ni watu wenye nguvu katika tasnia ya habari na Public relations.
Tangu enzi za kina Abdul Masoud (RIP), Peter Hassan ( aliwahi pia kuwa SC Villa). Uenezi Yanga ni kitengo maalum sana na kina mtandao mkubwa humu nchini na nchi za jirani. Waandishi wengi mahiri na watangazaji ni watu wa uenezi Yanga. Kina James Nhende, Omar Jongo etc...
Huyo mzee amekalia kiti muhimu sana, akiachie mara moja na asirudie tena!!
 
Wana vituko, TFF iwasaidie kwani yenyewe ni Team ya Taifa? Kama hawana hela wakacheze ndondo Cup huko!!

Simba haikua na hela ilisaidiwa na nani? Kama msaada wapewe team zote zinazoshiriki ligi kuu!!
Ni jambo la kushangaza wengi.. TFF inaendesha mpira kwa Sheria za Soka na Kanuni zake, ukata wao wanaona mchawi ni TFF

Wamesahau kuwa hizi si zama za Malinzi
 
Nimeshangaa mbona wakati wao wana ufadhili wa manji ,simba ina ukata ila ilikua hailiilii.
Yaani hata mwaka bado walalama njaa ikifika 2yrs itakuwaje? Mbona Simba SC imevumilia miaka 4.. Lakini yote hayo ni kwa sababu Malinzi hayupo na Manji

Walikuwa na jeuri sana, acha waipate walidhani Mungu atakuwa kwao siku zote..
 
Wana vituko, TFF iwasaidie kwani yenyewe ni Team ya Taifa? Kama hawana hela wakacheze ndondo Cup huko!!

Simba haikua na hela ilisaidiwa na nani? Kama msaada wapewe team zote zinazoshiriki ligi kuu!!
Umeisoma ukaielewa lkn mbona naona katoa ufafanuzi kuna hela wanasema wanadai sasa hizo club zingine nazo zinaidai TFF?
 
Mbinu pekee ya kuiondoa Yanga kwenye utamaduni wake wa kubeba NDOO kila msimu ni kwa kuihujumu kiuchumi. Natabiri kuwa haya yataendelea hadi dirisha la usajili litakapofungwa ili kuhakikisha Yanga inakimbiwa na wachezaji.
We utakua kama mwenyekiti wako wa matawi, Yanga inahujumiwa kivipi wakati kweli inadaiwa, Yaani nyie mmeingiza watu bure uwanjani afu mnataka kodi msilipe, Makato ya TFF, makato ya uwanja, makato ya CAF, yote msilipe kwa nini?
Wenzenu wanapoamua kufanya hivyo wanahakikisha gharama zote za uhendeshaji zinalipwa,
Maji alivyokua anawangiza bure mlishangilia saizi kawachia deni mnamlalamikia TFF.
Tena Yanga viongozi wenu wangekua na akili na hekima wasingetumia hii njia ila Mngewaomba TFF kimya ila deni lenu lisiwe linakatwa saizi hali yenu ya uchumi itulie ndo mje mlipe.
Mana dawa ya deni kulipa
 
kumbe na hili bomu ni kiongozi na yule mkemi wote hovyo

Back
Top Bottom