darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 9,038
- 17,933
ITAKAPOFIKA Oktoba 26 mwaka huu, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, atafikisha miaka mitatu tangu alipoingia madarakani akimshinda mpinzani wake, Athman Nyamlani.
Kuanzia Oktoba 27 mwaka huu, Malinzi atakuwa amebakisha mwaka mmoja katika uongozi wake, hivyo atahitajika kuitisha uchaguzi mkuu mwingine mwakani, utakapokoma muda wake wa uongozi.
Kwa mujibu wa katiba ya TFF, Malinzi ana awamu nyingine ya kuomba kuwania nafasi hiyo, kwani atakuwa amemaliza kipindi kimoja cha miaka minne, lakini kuna kingine cha miaka minne.
Haikuwa kazi rahisi kwa Malinzi kupata nafasi ya kuliongoza shirikisho kutokana na mgogoro ulioibuka, baada ya kamati ya uchaguzi ya rufaa TFF chini ya Idd Mtiginjora, kuondoa jina lake katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu moja ya kukosa sifa ya uzoefu wa uongozi katika masuala ya soka.
Kuondolewa kwake, kulileta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wana familia wa soka kutokana na baadhi yao walipinga hatua hiyo wakidai aliondolewa kwa mizengwe ili Nyamlani aweze kupita kirahisi.
Hawakutaka kufuatilia tena kigezo cha Malinzi cha kukosa uzoefu katika masuala ya uongozi wa soka na kilichotawala ni kwamba aliondolewa kwa chuki zilizotengenezwa na uongozi uliopita chini ya Rais Leodegar Tenga.
Mengi yalizungumzwa, lakini Malinzi hakutaka kuishia njiani, alipeleka malalamiko kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambao walituma wajumbe wake kwa lengo la kumsikiliza na wengine.
Hatimaye, Malinzi aliingia katika kinyang’anyiro hicho baada ya kamati ya utendaji ya TFF chini ya Tenga kufanyia kazi ushauri wa Fifa, uliokuwa umependekeza kuunda chombo cha sheria kabla ya kwenda kwenye uchaguzi.
Fifa ilipendekeza kuunda kamati mbili za maadili kwenye katiba ya TFF, ikiwamo kamati ya kwanza ya maadili na kamati ya rufaa lengo lilikuwa ni kushughulikia haki kutokana na kamati zilizokuwepo kutokuwa na mamlaka kisheria.
Baada ya kuunda vyombo hivyo, mchakato wa uchaguzi uliendelea huku Malinzi akibebwa na baadhi ya watu walioamini kwamba angeweza kufanya makubwa kwenye soka zaidi ya yale ya Tenga na timu yake ya uongozi.
Siku ya kwanza ya uongozi wa Malinzi, alionekana tayari ameshindwa kuliongoza shirikisho hilo baada ya kutangaza kuwafungulia waamuzi na viongozi ambao walifungiwa na viongozi waliomtangulia kutokana na sababu mbalimbali.
Baadaye, alimtimua usiku wa manane aliyekuwa katiba mkuu wa shirikisho hilo, Angetile Osiah, kisha benchi la ufundi la Taifa Stars, lililokuwa chini ya Kim Poulsen na kumleta Mart Noorj.
Lakini alipoona amefeli sasa amemrudisha Poulsen kama mshauri wa benchi la ufundi kwa timu za taifa, wengine waliofuata ni Sunday Kayuni aliyekuwa mkurugenzi wa fundi na wengine wengi waliokuwa watumishi katika utawala wa Tenga.
Haikupita siku nyingi, Malinzi aliingia katika mgogoro na Bodi ya Ligi na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, aliyeamua zikatwe asilimia tano ya mgawo wa fedha za klabu kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo.
Kitendo hicho kilipingwa na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Ligi, Damas Ndumbaro, ambaye alipelekwa kwa kamati ya nidhamu ya TFF na kufungiwa miaka saba kutojihusisha na soka.
Malinzi aliendelea kujenga chuki kwa watu ambao alikuwa anawaona hawako katika upande wake, kwani baada ya kumalizika hilo, ulikuja mgogoro na Simba.
Aliingilia mchakato wa uchaguzi uliokuwa umeanza, baadaye alimtaka aliyejuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, kuitisha mkutano wa dharura ndani ya siku 14 ili kuunda kamati ndogo katika katiba yao na baadaye kuendelea na uchaguzi.
Alitoa agizo hilo baada ya kamati ya maadili ya TFF kushindwa kusikiliza kesi zilizokuwa zimewasilishwa na kamati ya uchaguzi ya Simba, zilizowahusu Michael Wambura na wagombea wengine wa klabu hiyo.
Katika hili, Malinzi alishindwa na mwisho wa siku Rage alionekana ni shujaa baada ya kugomea maagizo yake na baadaye mchakato wa uchaguzi uliendelea kama kawaida.
Katika utawala wake, Malinzi ameendelea kuvuna migogoro kila kona, watu wamesahau mpira na sasa wanaendelea kusikiliza migogoro kwenda mbele.
Migogoro sasa hadi ngazi ya wilaya ambako TFF si mwanachama wake, huku Temeke hakukaliki, Kinondoni usiseme mpira hauchezeki kama zamani.
Lakini huko Tabora nako usiulize, viongozi wamefungiwa kutojihusisha na soka kwa sababu ambazo hazijitoshelezi kutoa adhabu hiyo.
Ukisubiri kusikia ya Tabora, uliza huko Shinyanga, klabu ya Stand United iko vipande vipande, mgogoro mbele kwa mbele, sasa timu mbili zinasajiliwa na kambi mbili za wanachama ni hatari hiyo.
Kabla hujapata jibu, uliza Yanga kuna nini sasa? Hautapata jibu ukisikia, Yanga kuruhusu mashabiki kuingia bure mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imekuwa ishu kubwa.
Kinachoendelea kwa sasa Yanga ni Mkuu wa Idara na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro, amefungiwa na kamati ya maadili ya TFF kwa madai kibao.
Mzee wa Kupasua anaona miaka mitatu ya Malinzi katika uongozi wake ni kama miaka 20.
source:Gazeti la Bingwa TFF kila kona sasa ni mgogoro - Bingwa