TFF katika kashfa ya Upangaji Matokeo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Katika Hali Isiyokuwa Ya Kawaida Na Ya Kutia Aibu Kabisa Soka La Tanzania RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA LA TANZANIA ( TFF ) JAMAL MALINZI Amehusika Katika KASHFA KUBWA YA UPANGAJI MATOKEO YA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA ULIOCHEZWA JANA UWANJA WA LAKE TANGANYIKA Mkoani Kigoma Baina Ya Timu Ya Geita Gold Mine FC Na FC Kanembwa Ambapo Timu Ya Geita FC Iliibuka Na USHINDI Wa Goli 8.

Akiongea Na Kipindi Cha Michezo Cha Sports Extra Cha Clouds FM Shuhuda Mmoja Ambaye ALIONGEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA Huku AKISEMA KUWA KUANZIA SASA ANAACHA TENA KUPENDA MPIRA WA BONGO NA SASA ANATAKA KUJIFUNZA KUCHEZA MCHEZO WA BAO. Shuhuda Huyo Bila KIFICHO Aliezea Mazingira Yote Ya Mchezo Huo Kama Yafuatavyo:

  • Mchezo Huo Kwa MAKUSUDI Ulianza Dakika 20 Bila Sababu Za Msingi.
  • Viongozi Waandamizi Wa TFF Kila Mara Walikuwa Wakitoa Maelekezo Ili Geita ISHINDE.
  • MESEJI Za Rais Wa TFF Zikitoa Maelekezo Timu Ya Geita FC Isaidiwe Ishinde Kwani Timu Hiyo Ya MGODINI Imekuwa Na Msaada Mkubwa Mno Kuisaidia TFF Kipindi Hiki HAINA HELA Zimeonekana Wazi Wazi Na Tayari Zimenza Kusambaa Kwa Wadau Wa Soka Hasa WAANDISHI WA HABARI WAANDAMIZI Wa Michezo.
  • Kipa Wa Timu Ya KANEMBWA Kwa Makusudi Alitoka Uwanjani Na Kutokomea Vyumbani Hadi Alipofuatwa Na Wachezaji Kuwa Arudi Lakini Akawa Anakataa Hadi Baadae Akakubali.
  • Mchezo Badala Ya Kuchezeshwa Dakika 90 au 95 Ukiongeza Zile Za Nyongeza Ulichezeshwa Kwa Dakika 108.
  • Kulikuwa Na MAKUBALIANO Kuwa Mechi Mbili Ambazo Zinahusisha Timu Mbili Ambazo ZINAPAMBANA Kupanda Ligi Kuu Yaani Police FC Ya Tabora Dhidi Ya JKT Oljoro Na Ule Wa Geita FC Na Kanembwa Yote Irekodiwe Lakini Cha Kushangaza Tena Kwa MAKUSUDI Kabisa Mechi Ya Geita FC Na Kanembwa Uliokuwa Ukichezwa Mkoani Kigoma Uwanja Wa Lake Tanganyika Ulizuiwa KUREKODIWA Kwa MAELEKEZO MAALUM.
  • Referee Wa Mechi Hiyo Ya Kigoma ALISAFIRI BASI MOJA Na Timu Ya Geita FC Huku AKIKARIMIWA Kwa Kila Huduma Mkoani Kigoma.
RAI Yangu Kwa WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA MICHEZO NCHINI TANZANIA KAMA KWELI TUNATAKA KUMSAIDIA RAIS WETU DR. MAGUFULI KATIKA KUPAMBANA NA MAJIPU HEBU NAOMBA KWA PAMOJA MSHIKAMANE KATIKA HILI ILI KUWEPO NA UWAJIKIBAJI KUSUDI TUNUSURU SOKA LETU. Na Naomba TAARIFA Hii IMFIKIE Mara Moja Waziri Wa Michezo Nape Nnauye Na WADAU Wote Wa Michezo Nchini Tanzania.

JAMAL MALINZI Rais Wa TFF Huna Haja Ya KUTUZUGA KWA MANENO YAKO ULIYOSEMA JANA BALI TUNAKUTAKA UPESI NA HARAKA SANA ACHIA NGAZI NA JIUZURU UPESI KWANI USHAHIDI WOTE WA ULICHOKIFANYA JANA HASA WA MESEJI WENYE NAMBA ZAKO WATU WANAZO NA UTAAIBIKA ZAIDI.

Kwa WATAKAOTAKA KUTHIBITISHA HAYA Na KUMSIKIA HUYU MTU ( SHUHUDA ) WAENDE CLOUDS FM WAKAOMBE CLIP YA KIPINDI CHA MICHEZO CHA LEO JUMAPILI MCHANA KISHA WAKISIKILIZE NA WAMSIKILIZE HUYO JAMAA AMBAYE ALIONGEA KUANZIA SAA 7 NA DAKIKA 27 HADI SAA 7 NA DAKIKA 33 AMBAKO ALISEMA SIRI ZOTE NA UOZO WOTE WA UPANGAJI MATOKEO UNAOMUHUSISHA MOJA KWA MOJA RAIS WA TFF NDUGU JAMAL EMILLY MALINZI.

Naomba Kuwasilisha.
 
Tumemwamini aliye sema kwa sababu kaongelea clouds? Saa nyingine naogopa sana nyuzi kama hizi unaweza kuta kuna personal interest au chuki binafsi....waswahili wanasema "fitna"....
 
harafu kwa TFF hii wanataka kocha wa timu ya taifa aendelee kulipwa na serikali?
 
Kuwa rais wa TFF.yataka uwe na roho ya paka. Lazima uwe tayari kubeba mizigo na lawama zote timu ikifungwa.

Tuwekee hizo sms
 
Dah kwa kweli kwa hii ni aibu kwa soka letu kwa upangaji huu wa matokeo inabidi tim zote zishuke daraja na fine kali kabisa na huyu malinzi ndio sababu hana budi kujiuzuru
 
Mtafute Mtangazaji Wa Michezo Mwandamizi Wa Clouds FM Alex Luambano Anazo Zote Kama Ushahidi Na Hata Ikibidi Watu Wa TAKUKURU Wakamwone Huyo Mtangazaji Kutokana Na Kwamba Ana Mzigo Kamili. Huwa SIKURUPUKI Kuja Na TAARIFA Humu Na Habari Ndiyo Hiyo. Na Kwakuwa Umechokoza Zaidi Sasa Nakuambia Tayari Kuna Mchezo Mwingin MCHAFU Huyo Huyo Mtu Wenu ANAHAHA Kuufanya Hadi Muda Huu Nao Ni Wa KUWAHONGA WAANDISHI WA MICHEZO WASIOJUA MIIKO YAO Na PESA Ili WASIZIDI KURIPOTI au KULIZUNGUMZIA HILI SUALA Na Kupitia Hii Post NAWAONYA VIKALI SANA Hao Waandishi Wa HABARI Kuwa Wasiporudisha Hizo HONGO WALIZOZIPOKEA WALLAHI Kesho Nawaanika Humu Humu. Sina CHUKI Na Malinzi Ila Nina Chuki Na Jinsi ANAVYOLIPELEKA SOKA LETU HUKU AKIWA Ni MSANII ALIYETUKUKA. Na Kuna BOMU LINGINE Lake Yeye Na Wale Jamaa Wa TAZARA Ambao Leo WAMEADABISHWA Na Waja Leo Warudi Leo LINANUKIA. Waandishi Wa Habari Fanyeni Kazi Zenu Ili Muokoe Soka La Tanzania Na Muweze Kumsaidia Rais Dr. MAGUFULI Katika Vita KALI YA UFISADI Na UJANJA UJANJA.
NGOJA NISUBIRI KESHO SPORTS BAR, wataweka madini yote hewani hawa kina Luambano, haya mambo ya kufuatilia figisu figisu wako poa sana!
 
hiyo timu yako kuna goli walifunga likakataliwa?mangapi?vipi perfomance ya mchezo ilikuaje?ball position kwa timu zote ilikuaje?tuanze hapo twende kisomi ili kuepuka majungu na fitna.
 
kwa kua tff kuna watu wanamatatizo basi ndio mtumie hiyo mafasi kuhalalisha upuuzi wenu yaani mshabiki tu alopoke basi na sisi tuamini?kwa taarifa yako mimi sio nyumbu

Ila timu kushinda 8 je record zake za nyuma zikoje? Alishawahi kufunga hata 3 bila au??
 
hiyo timu yako kuna goli walifunga likakataliwa?mangapi?vipi perfomance ya mchezo ilikuaje?ball position kwa timu zote ilikuaje?tuanze hapo twende kisomi ili kuepuka majungu na fitna.
Sasa mbona unaenda kiushabiki kuliko kisomi? Hakuna swali la kisomi hata moja uliloandika hapo!
 
Mpira wa Tanzania unamhitaji mtu kama Michael R. Wambura au Mhina Ally Seif Kaduguda
 
HAPA SOLN N MOJA TU ITAFUTWE HIZO MSG MWENYE CHANZO YAANI ANA MSG TOKA NAMBA YA JMALINZI

ANIPM NIMWELEKEZE CHA KUFANYA
 
Mtafute Mtangazaji Wa Michezo Mwandamizi Wa Clouds FM Alex Luambano Anazo Zote Kama Ushahidi Na Hata Ikibidi Watu Wa TAKUKURU Wakamwone Huyo Mtangazaji Kutokana Na Kwamba Ana Mzigo Kamili. Huwa SIKURUPUKI Kuja Na TAARIFA Humu Na Habari Ndiyo Hiyo. Na Kwakuwa Umechokoza Zaidi Sasa Nakuambia Tayari Kuna Mchezo Mwingin MCHAFU Huyo Huyo Mtu Wenu ANAHAHA Kuufanya Hadi Muda Huu Nao Ni Wa KUWAHONGA WAANDISHI WA MICHEZO WASIOJUA MIIKO YAO Na PESA Ili WASIZIDI KURIPOTI au KULIZUNGUMZIA HILI SUALA Na Kupitia Hii Post NAWAONYA VIKALI SANA Hao Waandishi Wa HABARI Kuwa Wasiporudisha Hizo HONGO WALIZOZIPOKEA WALLAHI Kesho Nawaanika Humu Humu. Sina CHUKI Na Malinzi Ila Nina Chuki Na Jinsi ANAVYOLIPELEKA SOKA LETU HUKU AKIWA Ni MSANII ALIYETUKUKA. Na Kuna BOMU LINGINE Lake Yeye Na Wale Jamaa Wa TAZARA Ambao Leo WAMEADABISHWA Na Waja Leo Warudi Leo LINANUKIA. Waandishi Wa Habari Fanyeni Kazi Zenu Ili Muokoe Soka La Tanzania Na Muweze Kumsaidia Rais Dr. MAGUFULI Katika Vita KALI YA UFISADI Na UJANJA UJANJA.
umetisha
 
Back
Top Bottom