TFDA yakamata zaidi ya tani sita za tende zilizohifadhiwa kwenye Madebe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mamlaka ya chakula na dawa nchini tawi la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania imekamata shehena ya bidhaa aina ya tende zaidi ya tani sita zilizokuwa zikitokea uarabuni kupitia nchi jirani ya Kenya kufuatia bidhaa hizo zilizokuwa zikiletwa nchini kwa ajili ya matumizi ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuhifadhiwa katika madebe yanayodaiwa kuwa yanaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.

Akizungumza na ITV katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania mkaguzi wa mamlaka hiyo katika mpaka huo Thomas Nkondola amesema zipo baadhi ya tende ambazo zinaingizwa kutoka uarabuni kupitia nchi jirani ya Kenya zinakuwa na nembo ya ubora na kufungashwa katika vifungashio ambavyo havina madhara na wanaziruhusu tofauti na hizo zilizokamatwa.

Baadhi ya watumiaji wa bidhaa hiyo ya tende waliokutwa katika mpaka huo wamesema baadhi yao walitumia tende zilizofungashwa katika madebe waliathirika afya zao kwa kushikwa na homa za matumbo hatua ambayo wameshauriwa na daktari kuwa bidhaa hiyo isitumike kwa matumizi ya binadamu.

Kufuatia hatua hiyo mkaguzi mkuu wa (TFDA) tawi la Horohoro Bwana Nkondola amewashauri watumiaji kuwa makini na bidhaa aina ya tende ambazo zimeingizwa katika njia zisizo rasmi huku mamlaka hiyo ikiendelea kuzuia zile ambazo zimehifadhiwa katika madebe ambayo yanahifadhi kutu ambayo ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

Chanzo: ITV
 
Kati ya taasisi bora kabisa Tanzania na Africa kwa ujumla,Jamaa wanajitahidi kwa udhibiti hata kama mipaka yetu ni mikubwa,ambayo husababisha wajanja wachache kupitisha bidhaa zisizoruhusiwa.
 
Sasa kwanini wafunge kwenye madebe? au wakifunga vizuri wanalipa ushuru mkubwa?
 
Kati ya taasisi bora kabisa Tanzania na Africa kwa ujumla,Jamaa wanajitahidi kwa udhibiti hata kama mipaka yetu ni mikubwa,ambayo husababisha wajanja wachache kupitisha bidhaa zisizoruhusiwa.
jamaa wako kitaaluma zaidi.
 
Kati ya taasisi bora kabisa Tanzania na Africa kwa ujumla,Jamaa wanajitahidi kwa udhibiti hata kama mipaka yetu ni mikubwa,ambayo husababisha wajanja wachache kupitisha bidhaa zisizoruhusiwa.
Africa? umetumia kigezo gani kujumlisha nji 50 +kuisifia TFDA?

wanajitahidi .......... ndio ila kwa Africa nzima mh hapo inabidi nikune kichwa kidoogo
 
Kwahiyo Madebe hayafai kuhifadhia vyakula? Hakuna vyakula na hasa mafuta ya kula yanayohifadhiwa kwenye Madebe? Au madebe yanatofautiana ubora? Naomba kueleweshwa....Mleta mada kama unapicha tupia please..
 
Back
Top Bottom