TFDA yakamata kiwanda bubu cha kutengeneza vipodozi Arusha

Matukio Jamii

Member
Sep 9, 2015
12
8
Mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kaskazini kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamembaini na kufanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja jijini Arusha anayemiliki kiwanda bubu kinachotengeneza vipodozi bila usajili wa TFDA pamoja na shehena ya zaidi ya tani saba ya vipodozi mbalimbali vikiwemo vile vilivyopigwa marufuku vikiwa vimehifadhiwa kwenye ghala lisilokidhi viwango.

Akizungumza na ITV katika eneo la tukio mtaa wa Sakina mkuu wa operesheni wa TFDA Benson Mcheza anasema wamefanikisha zoezi hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kwamba mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria na kulipia gharama zote za kuteketeza bidhaa hizo.

Kwa upande wake mfanyabiashara anayemiliki kiwanda hicho Chalo Makala amesema bidhaa zilizoko kwenye ghala ni bidhaa za dukani kwake ambazo amelipia kodi zote stahiki na kwamba zile anazozalisha zilikua kwenye majaribio.

Kwa upande wa uongozi wa kata ya Kiranyi kilipo kiwanda hicho wakatoa wito kwa jamii kutoa taarifa mapema pale wanapobaini uendeshaji wa biashara yoyote kinyume cha sheria ili kuepusha madhara kwa watumiaji lakini pia kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
 
Ndiyo maana wanunuzi hawaishi kubabuka na kuweka michirizi ktk ngozi kumbe sababu ndiyo hii ya kudondokea kwenye vipodozi fake
 
viini macho tu maana viwanda na berkary bubu zimejaa Ar mitaani mwetu na wenyewe wanajicfu kuwa wameshika viongozi wote makalio hata tufanyeje hawatochukuliwa hatua na tunaona viongozi wa kijiji wwakipta na kujifanya kama hawaoni lolote linaloendelea maeneo hayo.
 
Ndomana wakati mwengine unaweza kununua Lotion ya kawaida uliyo kwisha izoea ukashangaa baada ya kujipaka ikaanza kukuwasha
 
Watu kama hawa wapewe mafunzo sahii jinsi ya utengenezaji wa hizo mavitu vyenye viwango..
 
Mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kaskazini kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamembaini na kufanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja jijini Arusha anayemiliki kiwanda bubu kinachotengeneza vipodozi bila usajili wa TFDA pamoja na shehena ya zaidi ya tani saba ya vipodozi mbalimbali vikiwemo vile vilivyopigwa marufuku vikiwa vimehifadhiwa kwenye ghala lisilokidhi viwango.

Akizungumza na ITV katika eneo la tukio mtaa wa Sakina mkuu wa operesheni wa TFDA Benson Mcheza anasema wamefanikisha zoezi hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kwamba mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria na kulipia gharama zote za kuteketeza bidhaa hizo.

Kwa upande wake mfanyabiashara anayemiliki kiwanda hicho Chalo Makala amesema bidhaa zilizoko kwenye ghala ni bidhaa za dukani kwake ambazo amelipia kodi zote stahiki na kwamba zile anazozalisha zilikua kwenye majaribio.

Kwa upande wa uongozi wa kata ya Kiranyi kilipo kiwanda hicho wakatoa wito kwa jamii kutoa taarifa mapema pale wanapobaini uendeshaji wa biashara yoyote kinyume cha sheria ili kuepusha madhara kwa watumiaji lakini pia kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
sijui hata shuguli wanayofanya hawa TFDA mtaani maabara bubu zimejaa kila kona,tandika kuna hospitali pale wanadunga dunga watu misindano,jamaa wamelaza mpaka wagijwa wana cancer wanafia pale pale lakini wapo kimya tu,hao wanaotumia vipodozi wanajitakia wenyewe ya nini wanahangaika wenyewe??
 
Back
Top Bottom