TFDA pressed to stop Babu's 'miracle drug'

Serikali nzima ikiongozwa na mkuu wa kaya wameshakunywa kikombe cha babu sasa wanamgeuka.
 
Ningependa kupata ushahidi wa humu jamvini. kuna aliyeshuhudia mtu kupona?
 
Ningependa kupata ushahidi wa humu jamvini. kuna aliyeshuhudia mtu kupona?
Mkuu, si mmoja...ni wengi!
Kuna familia ambayo ilisafiri all the way toka kijijini kwangu huko Gungulugwa, na ilikuwa na mtu ambaye ana hali mbovu, na alikuwa hajagusa kazi yoyote nyumbani kwake kwa miezi 8, lakini baada ya kikombe, hadi dakika hii naandika yupo dukani mwake anauza mabazee kama kawa!..
Humwambii kitu kuhusu babu!
 
yule aliyeingiza dawa mseto na kuitangazia kwenye vyombo vya habari na kupewa kibali na sasa imegundulika haiwezi kutibu malaria tumfanyej?
mwacheni babu ale bata.
magonjwa yenu ndiyo yaliongeza usugu ngojeni babu aingie tena maabara(maombi) atakuja na kiboko ya magonjwa yenu.
 
... Dawa ya Babu HAITIBU kwa sababu wapo wachache waliokufa (just like Muhimbili, KCMC, India, South Africa, etc)
... Dawa ya Babu INATIBU kwa sababu wapo wengi walipoona (just like Muhimbili, KCMC, India, South Africa, etc)

AKILI KICHWANI MWAKO MTANZANIA.
 
Kulipoibuka tiba ya kikombe cha babu wa Loliondo watanzania wengi hasa viongozi wa dini, wanasiasa na madaktari walikiunga mkono kikombe cha babu lakini sasa wadau hawa hawa wamekigeukia kikombe cha babu na kuitaka serikali ipige marufuku huduma ya Babu Mwaisapile wa Loliondo.

MTIZAMO WANGU NI:

Kwa kuwa Serikali ilishathibitisha kuwa dawa hiyo ni salama kwa matumizi ya binaadamu basi watu waachiwe uhuru wa kwenda kunywa kikombe watakaopona bahati yao nzuri na wasiopona basi wajaribu tiba zingine.

Manake hata dawa za malaria hazimtibu kila mtu nyingine huua kabisa na ushahidi upo so WHAT CAN BE MEDICINE TO YOU MAY BE POISON TO OTHERS(and vice versa is true) likewise common sense is not common to all!

Nawasilisha

Inahitaji ujasiri wa mwendawazimu kumpigia debe leo Babu! Biashara ya Babu imedoda, once and for all. Haiwezi kuinuka tena, hata ingebebwa kwa winch! Watanzania wengi tumelizwa, kiasi kwamba hata kusikia jina la Babu tu, tunapata kichefuchefu! Ni vigumu nyoka aliyeko katika shimo moja, kumwuma mtu mara mbili!
 
Ukweli ni huo, kuwa watu wengi sana wameachana na matatizo waliyokuwA NAYO mara baada ya kupata kikombe.
Ambao hawajapona, well, waangalie taratibu zingine, lakini wasimdharau babu!

we jamaa una roho ngumu kweli,toka enzi hizo unamsapoti babu?bahati yako hujanywa kikombe usingekuwapo jamvini tena.inaonyesha wewe ni jitu nene hivi halafu jeusi tii.
 
we jamaa una roho ngumu kweli,toka enzi hizo unamsapoti babu?bahati yako hujanywa kikombe usingekuwapo jamvini tena.inaonyesha wewe ni jitu nene hivi halafu jeusi tii.
Rangi na maumbile yangu hayana tija hapa!
I just substantiate my thangs with living precedents!...right?
 
Serikali nzima ikiongozwa na mkuu wa kaya wameshakunywa kikombe cha babu sasa wanamgeuka.

Wanamgeuka nadhani baada ya kuona haijawaponya. Maskini kumbe hawana imani ya kweli ndio kikombe cha babu hakiktwaponyesha.
 
yule aliyeingiza dawa mseto na kuitangazia kwenye vyombo vya habari na kupewa kibali na sasa imegundulika haiwezi kutibu malaria tumfanyej?
mwacheni babu ale bata.
magonjwa yenu ndiyo yaliongeza usugu ngojeni babu aingie tena maabara(maombi) atakuja na kiboko ya magonjwa yenu.

kwa wanaotumia mseto hii dawa haiondoi malaria hasa kwa watoto ni HAIFAI nina ushaidi ya watoto malaria inarudi
 
Back
Top Bottom