MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,330
Nimesikitishwa sana na kauli ya Mkurugenzi mkuu wa TFDA Hiiti Sillo kuwa amefunga kiwanda cha dawa kilichopo Njiro Arusha baada ya kubaini kuwa ndicho kilichojusika kusambaza dawa bandia za ARVs.
Ikumbukwe kuwa kilichoanza ni dawa bandia kugundulika katika soko na backward tracking ikafanyika kubaini ziliko toka na mchakato huu ukachukua muda huku sintofahamu na utata wa mhusika ukitawala hadi walipokuja kugundua very late na kuamua kufunga kiwanda.
Alichokifanya Mr. Sillo ni kujikosha kuwa hahusiki hata kidogo na uzembe wa dawa bandia kuuzwa na hatimaye kufanya kiini macho kwa kujibaraguza kuwa wako makini na wakali na hivyo kuchukua hatua za kukifungia kiwanda kiwanda cha dawa.
Kazi za TFDA ni kama ilivyoandikwa hapa " Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA) is a regulatory body under the Ministry of Health and Social Welfare which is responsible for regulating the quality and safety of food, drugs, cosmetics and medical devices.
Kwa ufupi TFDA walitakiwa wafanye monitoring ya uzalishaji wa madawa katika viwanda hivi regularly ili kuhakikisha dawa zinazozalishwa zinakidhi viwango. Swali je wao walikuwa wanafanya na walikuwa wapi nini hadi dawa zikazalishwa na kuingia sokoni? Ninaamini uzembe wa wao kutosimamia vema viwanda na hatimaye kuacha mianya ya uchakachuaji imepelekea dawa bandia kuzalishwa.
Hata hivyo najiuliza je viwanda vya dawa viko vingapi hata washindwe kuvifanyia proper monitoring?
Kama wangelijua hilo basi walitakiwa wao kwanza kuwajibika kwa kutofanya kazi yao sawa sawa na kuacha mianya ya na hivyo kusababisha uchakachuaji.
Kufunga kiwanda ni sawa na kutibu dalili badala ya kutibu chanzo cha ugonjwa. Pia kufunga kiwanda ambacho ni mojawapo ya viwanda vichache vya madawa nchini ni kuendeleza wimbi na kuruhusu mianya ya dawa feki kutoka nyje kuendelea kupenya TZ.
Siafiki na wazo la kufunga kiwanda ambacho kwa TZ viko vichache sana kwa sababu tu mtu mbinafsi anarusha mpira kwa mwenzake kujikosha bila kujali mamilioni ya waTZ watakaoathirika kwa kufungwa kiwanda si kwa kukosa ajira tu bali kutopata dawa za kutosha.
Kwa mtu makini kufunga kiwanda badala ya TFDA kuwajibika ni option suicidal kuliko zote na siamini kama viongozi wenye dhamana na uchungu na hii nchi watauona ni uamuzi wa busara.
Kuna kila sababu ya kuamini kuna chain ya events hapo zenye lengo la kutaka kunufaisha baadhi ya wanaoagiza dawa nje na si tusidanganyike kuwa lengo ni kuboresha mfumo wa utengenezaji dawa.
Namshauri Mkurugenzi wa TFDA akubali kuwa uzembe uko upande wao katika kusimamia viwanda vya kutengeneza madawa na cha kufanya ni kuwajibika na kuimarisha monitoring system yao. Alichokifanya ni sawa na ku eliminate ugonjwa kwa kumuua mgonjwa badala ya kupambana na chanzo cha ugonjwa. Kama bado utendaji wa TFDA hautaboreshwa ikiwamo monitoring system yao basi tutarajie viwanda vingi zaidi kufungwa!!!
Lazima tukubali hii ni failure ya TFDA na kosa liskwepwe kwa kufunga viwanda bali wahusika wawajibike.