tezi za pua/adenoid-msaada wa kitaalamu pls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tezi za pua/adenoid-msaada wa kitaalamu pls

Discussion in 'JF Doctor' started by sweetdada, Oct 12, 2011.

 1. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wandugu natumai mu wazima wa afya.

  Nahitaji msaada wa kitaalamu kuhusu hizi tezi za pua.

  Nina mtoto wa miaka miwili amekuwa akisumbuliwa na mafua kwa muda mrefu tangu akiwa na wiki mbili, ila kila nikimpeleka hospital anapewa tu dawa za mafua na kikohozi akimaliza atakaa kama wiki then yanaanza upya. wiki tatu zilizopita daktari wa watoto akanishauri nimpeleke kwa ENT specialist of which jana ndo nikampeleka. Mtoto akafanyiwa xray na kuchunguzwa na doctor then nikaambiwa ana uvimbe mkubwa kwenye pu inabidi surgery..nikifikiria surgery kwa kweli nasikia kuumwa kabla sijampeleka.

  kama kuna anayefahamu inakuwaje na hii surgey haina madhara baadaye kwa mtoto?na hizo uvimbe zinaletwa na nini.. Please help!!niko kwenye wakato mgumu wa kufanya maamuzi ila sitaki kuyajutia baadae.

  Natanguliza shukrani.

  sweetdada
   
 2. fxb

  fxb Senior Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana Sweetdada, ila nina maono tofauti na wataalamu na sisi tunaokutwa na maradhi.
  Unapokuwa unasumbuliwa na maradhi yanayojirudia rudia ni veme unapokuwa hospitali uombe kuona bingwa zaidi wa kitu kinachosumbua.
  Nashauri wataalamu wanasema pata second opinion onana na ENT specialist mwingine akueleze nini hasa tatizo, linasababishwa na kitu gani na jinsi ya kumsaidia mtoto ukitoa hiyo sujari.
  Lete hapa jamvini halafu wajuzi waweza kukupa ushauri mzuri zaidi. Ila Pata second opinion ya ENT mwengine ikiwezekana different hospital
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Adenoids huwa mara nyingi zinasababishwa na allergy, japo sio zote. Kama chanzo chake ni allergy (mimi ninazo hizo za allergy) si lazima ufanyiwe surgery...ukitumia anti-histamine nasal sprays basi zinanywea na mtoto anapumua na kulala vyema tu. Faida ya surgery ni kuwa unaondoa kabisa tatizo, kwani kama ni za allergy zitamsumbua all his/her life!

  Nakubaliana na ushauri wa kupata second opinion kwa ENT surgeon...I recommend Dr Edwin Liyombo wa Muhimbili lakini pia anapatikana Regency Medical Centre, I trust his decisions especially on children ENT problems.
   
 4. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu nitafanya hivyo
   
 5. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Thank you Riwa, nimeshapiga simu Regency anapatikana evryday at 4pm nitampeleka leo jioni..ubarikiwe
   
Loading...