Zijue faida za kutumia Limao katika mwili wa mwanadamu

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
Faida za limao au ndimu zinajumuisha matumizi kama tiba kwa ajili ya vidonda vya kooni, matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya meno, homa, kuvuja damu ndani ya mwili, baridi yabisi, kutibu malengelenge, uzito kupita kiasi, matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kipindupindu na shinikizo la juu la damu. Pia ni dawa nzuri kwa ajili ya nywele na ngozi.

Tangu karne nyingi limao linajulikana kama dawa, husaidia pia kuongeza kinga ya mwili, kusafisha tumbo na hujulikana pia kwa kazi yake nzuri ya kusafisha damu.

Juisi ya limao ina faida kadhaa nyingi kama vile kuondoa mchanga katika figo, kupunguza kukamaa kwa mishipa (strokes) na kupunguza joto la mwili. Kama kinywaji ambacho huondoa uchovu mwilini, juisi ya limao itakusaidia kubaki mtulivu na mpole.

Faida nyingi za limao zinatokana na virutubishi vyake vingi mhimu kwa mwili kama vile vitamini C, vitamini B6, vitamini A, vitamini E, folate, niacin thiamin, riboflavin, pantothenic acid, shaba, kalsiamu, chuma, magnesium, potassium, zinki, phosphorus na protini.

Limao ni matunda ambayo yana kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini kiitwacho kwa kitaalamu kama “flavonoids” ambacho chenyewe ni mhimu sana katika kupigana na kansa mbalimbali mwilini.

Limao husaidia pia kuzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo la juu la damu, homa, husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na matatizo mengine mengi yakiwemo kuimarisha ngozi ya mwili, nywele na meno.

Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo cha Marekani (American Urological Association) unaonyesha kuwa juisi ya limao8 au ‘lemonade’ inaweza kuondoa au kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.

Watu hutumia limao na Asali kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade”.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

- Chukua asali mbichi nusu Lita

- Chukua limao kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa nusu lita.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.

Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limao nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalsini lita 2 ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5. Ihifadhi katika friji isiharibike.

Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.

Marashi au harufu ya limao hufukuza mbu, wakati huo huo kuinywa juisi ya limao iliyoongezwa mafuta ya zeituni husaidia kuondoa mchanga katika kibofu cha mkojo. Limao inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi na hutumika kwa namna nyingi tofauti.

Zifuatazo ni faida mbalimbali za limao mwilini:
1. Kufunga choo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula

Juisi ya limao husaidia kutibu matatizo yahusianayo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula na kufunga choo. Ongeza matone machache ya limao kwenye chakula chako (kuwa makini sababu limao huwa haipatani na maziwa), na itakusaidia katika kumeng’enya chakula.

Limao hufanya kazi kama wakala msafisha damu na mwili kwa ujumla. Na hii ni nzuri kama unapata juisi yako ya limao baada ya chakula cha mchana au cha usiku. Juisi ya limau inatengenezwa kwa kuchanganya maji ya limau, maji kidogo, chumvi ya mawe kidogo na asali au hata sukari. Weka na barafu kidogo pembeni.

Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.

2. Hutibu homa
Juisi ya limao inaweza kumtibu mtu anayesumbuliwa na homa, mafua au baridi. Limau husaidia kutibu homa kutokana na sifa yake ya kuongeza kiasi cha jasho mwilini.

3. Huongeza afya ya meno
Juisi ya limao mara nyingi imetumika katika kulinda afya ya meno. Kama juisi fresh ya limao itanyunyizwa juu ya jino linalouma inaweza kusaidia kuondoa maumivu. Kusugua (masaji) juisi ya limau juu ya fizi za meno kunaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kutokwa damu kwenye fizi huku ikiondoa harufu mbaya katika fizi na mdomo kwa ujumla.

Unaweza kupata faida hizi kama utakuwa unapiga mswaki ukitumia dawa yenye limau ndani yake (lemon tooth paste).

4. Hutunza nywele
Juisi ya limao imejidhihirisha yenyewe kuwa dawa nzuri kwa upande wa matatizo mbalimbali ya nywele. Juisi ya limao ikipakwa kwenye ngozi ya kichwa inaweza kutibu matatizo kama ya mba, kupotea au kukatika kwa nywele, na matatizo mengine yahusuyo nywele na ngozi ya kichwa.

Kama utakuwa ukisafisha nywele zako kwa kutumia juisi au maji ya limao moja kwa moja basi utazifanya nywele zako zipate mng’aro wake wa asili bila gharama yoyote ya ziada.

5. Hulinda ngozi
Kwakuwa Juisi ya limao ni dawa ya asili dhidi ya bakteria, inaweza pia kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi. Juisi ya limau inaweza kutumika kupunguza maumivu kwenye ngozi sababu ya kuungua na jua, pia husaidia kupunguza maumivu kutokana na kung’atwa na nyuki. Juisi ya limao au majimaji ya limau yanaweza kutumika kupakaa juu ya ngozi na kutibu chunusi na ukurutu.

Limao pia hutumika kama dawa ya kukufanya usionekane mzee kwakuwa yenyewe huondoa mikunjo na madoadoa ya ngozi.

Kunywa maji ya limao yaliyochanganywa na asali kunasaidia ngozi kuwa na afya zaidi na hata ukipekuwa huko sokoni utazipata baadhi ya sabuni ambazo zimetengenezwa kutokana na limau.

6. Hutibu majeraha ya moto
Upakaji wa maji ya limao (juisi) kwenye eneo la ngozi lililoungua huweza kusaidia makovu kupotea na hii husaidia pia kwa mtu aliyepatwa na malengelenge au vipele vyenye maji maji yanayouma ndani. Na kwa sababu limao ni wakala wa kupooza au wakala mtulizaji (cooling agent), huweza kupunguza maumivu au kuhisi kuungua kwenye ngozi hasa wakati unakuwa na majeraha yanayounguza ngozi.

7. Huzuia kuvujika kwa damu
Limao inayo sifa ya kudhibiti bakteria mwilini (antiseptic properties) na kugandisha damu, sifa hizi au kazi hizi mbili za limao husaidia kusimamisha kuvuja kwa damu ndani ya mwili. Unaweza kutumia maji ya limau ukiweka kwenye kipande cha pamba na kuiweke puani kuzuia pua kuvuja damu.

8. Hupunguza Uzito
Ikiwa utakunywa juisi ya limao iliyochanganywa na asali na maji ya uvuguuvugu, hasa asubuhi tu unapoamka inaweza kusaidia kupunguza uzito.

9. Hutibu matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
Juisi ya limao husaidia katika kutuliza matatizo katika mfumo wa upumuwaji kama vile pumu. Kwakuwa limau ina kiasi kingi cha vitamini C, husaidia kutibu na kutuliza matatizo ya muda mrefu kwenye mfumo wa upumuwaji.

10. Kipindupindu
Magonjwa kama kipindupindu na malaria yanaweza kutibika kwa kutumia juisi ya limao tu kwa sababu limau hufanya kazi ya kusafisha damu na mwili kwa ujumla.

11. Hutuliza maumivu ya miguu
Limao huwa na harufu ya kuvutia (aromatic) na pia inayo sifa ya kudhibiti bakteria na hutumika kutuliza maumivu au miguu kuwaka moto. Ongeza juisi (maji ya limau) kwenye dishi lenye maji ya moto kidogo na utumbukize miguu kwa dakika kadhaa kwa kuondoa haraka maumivu ya miguu na utajisikia umepata tulizo fulani (relaxed).

12. Baridi Yabisi
Limao au ndimu pia ni kikojoshi, yaani ni kitu kinachosisimua uzalishwaji wa mkojo na kwa sababu hiyo inaweza kutibu baridi yabisi na maumivu ya kwenye mishipa. Husaidia kutoa nje bakteria wabaya na sumu mbalimbali mwilini.

13. Hutibu malengelenge (Corns)
Juisi ya limao inaweza kusaidia kukausha malengelenge au vipele ambavyo huwa na majimaji ambavyo hujitokeza mara nyingi chini ya unyayo au katikati ya vidole vya mikono. Kunywa juisi ya limao na maji ndani yake husaidia wagonjwa kupunguza mawe kwenye nyongo.

14. Hutibu maambukizi ya kwenye koo
Limao ni tunda bora kabisa ambalo hupigana dhidi ya matatizo yanayohusiana na maambukizi kooni sababu ya sifa yake kubwa ya kudhibiti bakteria mwilini.

15. Hutibu shinikizo la juu la damu
Kunywa juisi ya limao kuna msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya moyo kwa sababu limau lina kiasi cha kutosha cha potasiamu. Limau hudhibiti shinikizo la juu la damu, kizunguzungu, na uchovu sugu kwa sababu yenyewe limau hutoa hisia za utulivu kwa mwili na roho pia. Mara nyingi limau imetumika kwa watu wenye mfadhaiko wa akili na majonzi.

Sent using Jamii Forums mobile appiphone
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom