Teuzi zijazo tufikiriwe na sie wa Mitaani

Huwa nawaza mama akimaliza mda wake nan atakuwa tena raisi ? AU TUMPE HUYU MKUU WA MKOA WA DODOMA NAONA KAMA ANAMAWAZO MAZURI....nimemsikiliza kwenye clip moja kuhusu mafuta nikaona huyu jamaa anamawazo mazuri kama akipewa nchi akashindwa badilika tutakuwa tume bet vizur
 
Swali dogo mkuu nikuulize. Mteuzi atakujuaje kama upo?
Jibu dogo
Kabla ya kuteua mabslozi angewasiliana na chuo cha diplomasia pale kurasini akaulizia ma graduate wazuri waliotoka hapo miaka ya karibuni,angepewa list na hapo ndipo angeliona jina langu kama mmoja wa wahitimu wazuribchuoni pale.
Hapo angekua amenipata
 
Umeongea kwa hisia kali as if unasali aisee. Anyway jitahidi kukaa jirani na vyanzo vya maji hauwezi kukaa na kiu ya maji.
 
Mzee kutoboa sio hadi nyote mteuliwe, wewe piga kazi kitaa ukipata pesa usisahau kujifurahisha kama mwisho wa mwaka nenda mbugani huko, mara moja moja ukipata pesa unakanyaga hata grants na nyama ya kuokwa, usisahau kuacha kuvaa mabwanga, kama kadet piga kali, watoto wa mjini wakivaa raba na wewe piga raba, ukiwa na stress nenda beach kapigwe upepo kidogo iwe uko karibu na bahari au ziwa, usisahau kujichanganya na masela wale wa maana upate michongo na changamoto za hapa na pale mengine yatakuja mbelembele huko ukichora mstari
 
Mtoa mada, kama umetoka kijijini kama mimi , Dar ulifika kwa treni yaani kwenu hata mtendaji wa kijiji hawafahamu, umesoma hadi barchelor hujawahi kua monitor, hujawahi kua chipkizi wa ccm, jina lako umoja wa vijana halipo, kadi ya ccm hauna, ukililia teuzi mwamba unakwama
 
Utaratibu uliopo hautendi haki wala kutoa fursa sawa kwa waTZ wote kuweza kuteuliwa kutumikia Taifa lao.

Ni mpaka akujue Rais au kupitia wasaidizi wake au wapambe kinyume na hapo ni kwa majaliwa ya MnyaziMungu!

Nchi hii kuna mambo mengi sana ya kurekebishwa kupitia Katiba wenzetu nchi jirani walishaachana na utaratibu huu wa kikoloni kwa miaka mingi ilopita.
 
Utaratibu uliopo hautendi haki wala kutoa fursa sawa kwa waTZ wote kuweza kuteuliwa kutumikia Taifa lao.

Ni mpaka akujue Rais au kupitia wasaidizi wake au wapambe kinyume na hapo ni kwa majaliwa ya MnyaziMungu!

Nchi hii kuna mambo mengi sana ya kurekebishwa kupitia Katiba wenzetu nchi jirani walishaachana na utaratibu huu wa kikoloni kwa miaka mingi ilopita.
Umeongea point
 
Kutokana na tatizo la ajira ije ifikie na wahitimu tunaozurula na vyeti kusaka ajira miaka nenda rudi. tukumbukwe,watu walioko kwenye ajira na wastaafu wasubirie kwanza na sie wa kitaa tupewe nafasi hali ngumu sana mtaani.
Sasa si mpaka uwe unafahamika na wajuba
 
Back
Top Bottom