tetezi kesi ya Maranda, Farijala kuanza leo

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, leo itaanza kusikiliza utetezi wa kesi ya wizi wa Sh. bilioni 1.8 za Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayowakabili wafanyabiashara wawili, Rajabu Maranda na Farijala Hussein.
Kesi hiyo ilikwama kuanza kusikilizwa utetezi jana baada ya wakili wa utetezi, Majura Magafu, kuomba mahakama kumpa muda wa kujiandaa na wateja wake.
Utetezi huo utasikilizwa mbele ya jopo la mahakimu watatu, Saul Kinemela, Focus Bampikya na Elvin Mugeta, wanaosikiliza kesi hiyo.
Wakili wa Serikali, Boniface Stanslaus, alidai kuwa kesi hiyo iko katika hatua ya kusikiliza utetezi dhidi ya washtakiwa.
Hata hivyo, wakili Magafu alidai kuwa upande wa utetezi haujajiandaa ambapo aliomba mahakama kumpa muda wa kufanya hivyo hadi leo washtakiwa watakapoanza kujitetea.
Mahakama iliridhia ombi hilo ambapo washitakiwa wataanza kujitetea leo mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa la wizi wa Sh. bilioni 1.8 baada ya kudanganya kwamba Kampuni ya Kiloloma & Brothers Enterprises ya Tanzania, imehamishiwa deni na kampuni ya B.C Cars & Export ya India.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom