John F Kenerdy alikuja bongo miaka hiyoo,kukawa na hafla ikulu, mwenyeji Nyerere akawa anamtembeza mgeni wake maeneo ya ikulu,kwa mbali kulikuwa na jamaa anakojoa, Kenerdy alishangaa sana,akamuuliza Nyerere kwanini watu wanachafua mazingira ya Ikulu.mwenyeji akatuma maofisa usalama na kumkamata yule mtu,baada miezi kadhaa Nyerere nae akaenda USA..Kenerdy nae akawa anamtembeza mgeni wake....kwa mbali akaoneka kuna jamaa anakojoa.Nyerere akamuuliza vipi na kwako pia ni wachafu hivi?,Kenerdy akastaajabu sana,kwani ni tukio la ajabu kwa mtu kukojoa maeneo ya white house...watatumwa walinzi akamatwe...alipoletwa khaaa alikuwa waziri aliyeongazana na Nyerere huko USA...story za zamani bhana fiksi tupu..