Tetesi za usajili Ulaya kabla ya dirisha kufungwa Septemba 1, 2023

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Dirisha la usajili Ligi Kuu kubwa Ulaya linatarajiwa kufungwa Saa 5:59 Usiku wa Septemba 1, 2023, kuna taarifa nyingi kuhusu usajili, hizi ni baadhi

Chelsea ina nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa Brighton, Moises Caicedo (21) kwa Pauni Milioni 115 (Tsh. Bilioni 364) ambaye pia anawaniwa na Liverpool

Liverpool inaweza kumkosa Kiungo wa Southampton, Romeo Lavia (19) ambaye ameonesha nia ya kutua Chelsea kwa Pauni Milioni 55 (Tsh. Bilioni 174).

Kipa Kasper Schmeichel (36) anatarajiwa kujiunga na Chelsea akitokea Nice kuchukua nafasi ya Kepa Arrizabalaga (28) ambaye atajiunga na Real Madrid kwa mkopo wa msimu mmoja.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili kiungo wa West Ham, Lucas Paqueta (25) baada ya kuumia kwa Kevin de Bruyne.

Neymar anaamini atafanikisha nia yake ya kurejea Barcelona ndio maana anapambana kuhakikisha anaondoka Paris St-Germain, pia Al Hilal ya Saudia nayo imewasilisha ofa kubwa ili kumsajili.

Real Sociedad imejiondoa kwenye mpango wa kumsajili kiungo Donny van de Beek (26) kutoka Manchester United.

Source BBC
 
Back
Top Bottom