Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Katika mfumo wa kidola tulionao, Bunge ni kila kitu. Pamoja na uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama kama mihimili ya kidola, Bunge ni mhimili muhimu kuliko yote katika kufanya siasa, kuisimamia Serikali, kutunga sheria na hata kupitisha bajeti. Mwenye wingi wa wabunge ndiye 'anayekula bata' kwakuwa alitakalo ndilo linalofanyika na kuwa Bungeni.
Kwa wingi wa Wabunge walionao CCM katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CCM inalimiliki itakavyo Bunge. Wana haja gani ya kuwanunua Wabunge wa upinzani? Vyama vyenye Wabunge Bungeni ni CCM, CHADEMA,CUF,NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo. Kati ya vyama hivyo, CCM ina wabunge wengi kuzidi jumla ya wabunge wa vyama vya upinzani. Kuna haja gani ya kununua Wabunge wa upinzani?
Kuhusu Madiwani, CCM inaongoza zaidi ya asilimia 80 ya Majiji, Manispaa, Miji na Miji Midogo nchini kutokana na kuwa na wingi wa Madiwani. Wana Mameya, Manaibu Meya, Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa kutosha katika kuongoza Halmashauri hizo.Ndiyo kusema, Ilani ya CCM inatekelezwa bila kikwazo. Madiwani wa upinzani wa nini kununuliwa?
Katika sura hiyo ya kisiasa Bungeni na kwenye Halmashauri, tuamini kuwa Wabunge na Madiwani wa upinzani wanaojiunga na CCM wanajiunga kweli kwa utayari wao binafsi katika kumuunga mkono Rais Magufuli na Serikali yake (kama ni kweli)? Au, tuamini kuwa kinachofanyika (kama ni kweli) ni jitihada za kuua upinzani na kuturejesha katika mfumo wa chama kimoja? CCM inafaidikaje ikiwa tayari ina wingi wa aina hiyo?