Tetesi ya kuondolewa huduma ya magari ya Bolt

Tetesi ya kuondolewa huduma ya magari ya Bolt

Denjo

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
359
Reaction score
118
Kuna tetesi kuwa katikati ya mwezi huu kampuni ya usafirishaji ya magari (Online Taxi) Bolt inasitisha huduma za usafiri kupitia magari. Watakaopata huduma ni kundi dogo nasikia. Hii inakaaje na gharama zetu za maisha tuliozoea ku-request? Watalaamu mje kutusaidia hapa au ndio tunarudi kwenye taxi, Kinondoni - Mwenge unalipia Sh. 25,000/=

===

Bolt yatishia kusitisha huduma zake Tanzania

Baada ya Kampuni ya Uber kusitisha baadhi ya huduma zake Nchini Tanzania, huenda Kampuni ya Bolt nayo ikafanya hivyo kwa upande wa huduma za Usafiri wa gari maarufu kama teksi kutokana na ada ya huduma ya 15% iliyowekwa na LATRA.

bolt.jpg

Huduma ya usafiri wa mtandaoni, Bolt

Meneja wa Bolt Kanda ya Afrika Mashariki, Kenneth Micah amesema Kampuni hiyo imeomba kukutana na wadau ili kujadili zaidi suala hilo kwa matumaini ya kufika mbadala.

Bolt imepanga kuwafikia wadau husika, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), ili kujadili upya masharti mapya yaliyowekwa.

"Bolt ameomba kukutana na wadau husika ili kujadili zaidi suala hili kwa matumaini ya kufikia kanuni nzuri za ushuru na kamisheni, hata tunapoendelea kutafuta na kutafuta njia mbadala za ushawishi zinazotolewa ndani ya mfumo wa kisheria ikiwa ni pamoja na mfumo wa udhibiti wa LATRA." alisema. Meneja wa Bolt Kanda ya Afrika Mashariki, Kenneth Micah.

Bolt, ambayo inawatoza washirika wake kamisheni ya asilimia 20 ilisema kwamba itazima aina ya magari yake iwapo hakuna kitakachobadilika.

"Tunatii kwa muda ili kuonyesha nia njema na kujitolea kwetu kushirikiana na LATRA kwa kanuni zinazofaa zaidi zinazowezesha uwekezaji zaidi. Tunafahamu ukweli kwamba iwapo LATRA itadumisha hali ilivyo sasa, soko hatimaye litakoma kuwa na faida kwa Bolt, na hii italazimu kuzima kitengo chetu cha magari." alisema Micah.

Hata hivyo, kampuni ya mtandaoni ya Uber ilisitisha shughuli zake nchini hapa wiki kadhaa zilizopita kutokana na suala hilo hilo, ingawa ilisema kuwa itarejesha biashara hiyo ikiwa masharti yatakuwa mazuri.

Bolt ambayo inafanya kazi katika mataifa saba barani Afrika, ikiwemo Kenya, Afrika Kusini, Uganda, Ghana na Nigeria, imesema kuwa huenda takriban Madereva 10,000 wakalazimika kutafuta ajira nyingine ikiwa watasitisha huduma.

Chanzo: EATV
 
Kuna Tetesi kuwa Kati Kati ya ya mwezi huu kampuni ya usafirishaji ya magari (Online Taxi) B* inasitisha huduma za usafiri kupitia magari watakao pata huduma Ni kundi Chache naskia hii inakaaje na gharama zetu za maisha tuliozoea kurequest ? Watalaamu mje kutusaidia hapa au ndio tunarudi kwenye taxi kinondoni mwenge unalipia 25,000/=
hii ni kampuni gani Bolt au?
 
Kuna kitu hakipo sawa kati ya pande tatu, serikali, wenye mtandao na wenye magari...... Maana walianza uber kusitisha hizo huduma na sasa wanakuja Bolt na woote hao waliondoa huduma za magari wakaacha za bajaj na bdbd
 
Hapo wabongo washafanya yao
 
Kuna Tetesi kuwa Kati Kati ya ya mwezi huu kampuni ya usafirishaji ya magari (Online Taxi) B* inasitisha huduma za usafiri kupitia magari watakao pata huduma Ni kundi Chache naskia hii inakaaje na gharama zetu za maisha tuliozoea kurequest ? Watalaamu mje kutusaidia hapa au ndio tunarudi kwenye taxi kinondoni mwenge unalipia 25,000/=
Tanzania ni nchi ya hovyo sana
 
.....Kati Kati...!
....katikati...inapendeza zaidi.
....nazani...!
....nadhani...inapendeza zaidi.
Kunajamaa alikuwa akijitapa kuwa eti watanzania tunajua kiswahili vizuri sana.
 
Kila Bolt Tax niliyopanda hapa karibuni dereva aliomba ni cancel hiyo request ila nimlipe ela iliyoandikwa kwenye app, hayo yote sababu wanataka 30% ambayo dereva akiwapa anakuwa anawafanyia kazi wao.

Wakae na madereva waongee vizuri.
 
Taxi mtandao maarufu kama Bolt imetangaza kusitisha huduma zake nchini Tanzania kuanzia tarehe 17/08/2022, ikitaja nauli elekezi za Mamlaka ya udhibiti Usafiri Ardhini -LATRA kama sababu ya maamuzi hayo na kudai itarejesha huduma zake kwa nchi hiyo iwapo sheria zitabadilishwa. Wataendelea kutoa huduma hizo kwa wateja wa makampuni pekee.
 
Kila Bolt Tax niliyopanda hapa karibuni dereva aliomba ni cancel hiyo request ila nimlipe ela iliyoandikwa kwenye app, hayo yote sababu wanataka 30% ambayo dereva akiwapa anakuwa anawafanyia kazi wao.

Wakae na madereva waongee vizuri.
Ni kweli madereva wanawaibia sana, wanatumia mtandao kumpata mteja, mnaelewana Bei, then anakushauri ucancel alafu anakupeleka bila pesa kuingia kwenye campuni, nadhani Itakua Moja ya sababu, wabongo nuksi, hawashindwi kitu.
 
Back
Top Bottom