Tetesi: Shoprite imefungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi: Shoprite imefungwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jan 20, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi kwamba yale maduka maarufu ya shoprite ymefungwa na waajiriwa wote kupoteza ajira pamoja na malipo mengine muhimu
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Tumechoka kununua vitu expired!
   
 3. T

  Tango Member

  #3
  Jan 20, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  wameona wanapata loss ama wameshindwa kuelewana na wenye brand/jina lao... inasemekana walikuwa wanatumia tu nembo ya shoprite na si shoprite halisi. Hayo ndio mambo ya franchising. Apart from kupoteza ajira ...wafanyakazi kuna tetesi kuwa walikuwa wezi sana...sishangai, hakuna mkulima ama mwenye kiwanda wa Tanzania atakaye loose sana na ufungwaji huo kama ni kweli. Asilimia 90 ya vitu vyao vilikuwa vinatoka SA.
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  mamama weee jamaniii ni balaa......poleni ndugu zetu kama ni kweli....inakatisa tamaa maana huwezi jua ni wangapi wamepoteza na watu wangapi walikuwa wanaishi sababu ya ajira za ndugu,jamaa zao pale..........
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hilo ndilo tatizo la biashara za nguvu ya soda,iweje bidhaa zao nyingi kutoka nje,ni vizuri Wa TZ wazisusie kwani hazina tija kwa TZ.Tusiwape wageni biashara zote shauri ya 10% halafu wakisusa au wakishapata faida na kuamua kuondoka ni hasara kwa uchumi wa TZ.Hivyo wazalendo wawezeshwe washikilie uchumi wa Nchi(TZ).
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Jamani, kwa mujibu wa Shy hizo ni tetesi. NAdhani tupate uthibitisho hapa ndo tuanze kutoa michango. Ni wazo tu!
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mimi siku zote iwa simwamini shy mnajua huyu ni mtunzi angalia huyooooooo katoweka.
  Shoprite saizi zinakula vichwa sana eti wafunge duhh ngoja tuisubili hii tetesi.
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wewe kaa shangaa tu hata mhasibu wao mkuu anatakiwa kwenda bondeni kuwa data clerk kuficha madhambi yao waliyokuwa wanayatenda haswa na watu wa kodi na hawanunui bidhaa za viwanda vya tz kwa sasa kutokana na kufanya huko biashara zao
   
 9. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #9
  Jan 20, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni shoprite ya slipway ndo inafungwa na wala sio zote. Inadaiwa kuwa wanaiba (staff) sana na hivyo kusababisha hasara kwa kampuni.

  As kuhusu bidhaa zao nyingi kutoka Afrika ya kusini nadhani tukiwalaumu tutakuwa hatuwatendei haki sana. Hivi kuna sheria yeyote inayowabana wasiingize bidhaa kutoka sehemu wanayo ona wao inafaa? Hata kama linge kuwa duka lako wewe lazima ungeaangalia wapi unapata mzigo kwa bei nafuu ili ukiuza upate faida. Wanachokifanya hawa jamaa ni kutumia vizuri weaknes ya system iliyopo kwa faida yao. Au mmesahau mfanyabiashara anaangalia umezubaa wapi na kisha akupige bao?


  Ni hayo tu.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Yes its only Shoprite ya Sleepway. Hivyo sio tetesi tena, shoprite zingine zote zinaendelea kama kawaida na ni kweli wanaiba sana ili sie wengine ambao hatuwezi kuaford vile vizuri vya hapo, tuuziwe kwa bei poa. Pamoja na wizi wote, Shoprite hazitafungwa kwa vile zina make super profit, wafanyakazi wanalipwa mishahara peanut, hivyo wale wanaoiba, wanagawana faida na makaburu. Mpaka nyanya, nyama zinatoka SA wafaidika wakubwa wakiwa Afrika Kusini.
  On-the other side, bidhaa zetu zinakosa nafasi kutokana na poor packaging. Acha matenga ya nyanya na mapakacha ya matunda ambayo ni organic yaende Sokoni Kariakoo na wenye pesa zao waendelee kula Genetic Modified Foods za Shoprite. Wamarekani walisha stuka zamani, kila kitu mpaka maji ya kunywa, wanaa
  Import toka kwao!.
   
 11. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Haya weeeeeeeeeee kaaaaaaaazi kweli kweli
   
 12. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Lazima tujiandae na vitu kama hivi, serikali inasema nini kuhusu wafanyakazi waliopoteza ajira? ilijiandaa kuwasadia kwa jinsi gani, sasa hivi serikali nyingi ulimwenguni wanaangaika kuwasaidia wafanyakazi wao kwani kila sehemu biashara na viwanda vinafungwa kila siku.

  kwa uchumi wadunia iliyogeuka kuwa kijiji kimoja tutakwepa lakini matatizo yaq credit crunch yatakuja muda si mrefu na viwanda vyetu na biashara zetu zitahathirika, na kwetu madhara yatachukua muda kwani hatuna maandalizi ya kuepukana na madhara hayo.
   
 13. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,187
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Mkuu thibitisha hii tetesi kwanza..
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Saa nane mchana pale Mlimani ilikuwa wazi na inaendelea na biashara.
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Jan 21, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  ...watanzania tubadilike ..wawekezaji wengi wanalalamika sana kuwa watanzania ni wadokozi sana .....ndio maana maduka kama shoprite,scores, etc yataendelea kufungwa......

  wafanyakazi wa hizi supermarket wanahujumu sana....ukinunua kitu ukifika kwa cashier anakuchekea chekea akiona unaeelekea anaweza kufanya wanavyojua bili yako ya tsh.100,000 inasomeka 40,000 na yeye unampa 20,000...kwa kweli tabia hii sio nzuri...

  wale vijana wa kwenye ma shelf nao wana deal zao ....anabandua price tag anaweka ya bei ndogo unampa pesa!...yaani ni vurugu...na sidhani kama hatutaacha tabia hii huu ustaarabu wa supermarket utadumu hapa...

  tatizo tumelelewa kwenye maduka ya kijiji yenye grill yaani huwezi hata kugusa mali ya dukani hadi ununue..sasa huu utaratibu wa self service kidogo tatizo........

  watanzania tunalalamikia viongozi ufisadi na sisi tunafanya udokozi supermarkets ....du!!
   
 16. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nafikiri kariakoo ikiboreshwa vizuri kila kitu kinapatikana fresh from shamba kuliko kwenda pale shoprite unanunua mkaouko wa vitu. Ila watanzania tuna kasumba mbaya sana, hivi kweli unashindwa kwenda kuwaunguisha watanzania wenzio wa kariakoo unaenda kununua uozo wa Shoprite???

  Ilimradi utoke unasukuma vifaa vyako kwenye trail ndiyo raha ya mtanzania. Kibaya zaidi shoprite vitu juu sana ukilinganisha na kariakoo.

  tafakarini jamani, utumwa mwingine sisi ndiyo waanzilishi kama siyo wendelezaji.
   
 17. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #17
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Da Caro,
  Ukiangalia kwa side ingine watu wanaenda kwenye hizo maduka za kisasa kwa sababu zilizo wazi kabisa. Mfano, usafi wa vitu/bidhaa, mda wa kupata huduma, usalama wakati unapata huduma, nk nk. Cha msingi watanzania wenye biashara zao wajifunze kuwa wabunifu na wenye lugha nzuri kwa wateja...Unakumbuka Chesco alivyo anzisha biashara yake ya marunda pale Africa sana? Watu walikuwa wanatoka place nyingi sana na kwenda kununua matunda kwake (sijui kama bado yupo). Lakini sio Chesco matunda peke yake..pia kule msasani kama sijakosea kuna wapemba wana magenge yenye mvuto kabisa na wanapata wateja wa kutosha kabisa. So unaona kama watu wanajua huduma yako ni nzuri basi watakuja tu. Wenye biashara wakiacha kurundikana pale Kariakoo na kuanzisha sehemu zenye kuvutia basi ndipo hapo watu watashawishika kuachana na hizo bidhaa toka sauzi, otherwise makaburu wataendelea kula faida tu na hivi mfumo unawafavour basi ndo kabisaaaaaa!

  Asante.
   
Loading...