TETESI: Serikali yatishia gazeti la KULIKONI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TETESI: Serikali yatishia gazeti la KULIKONI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, May 12, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Baada ya gazeti la KULIKONI kuandika tahariri yenye kuonyesha kupingana na taarifa ya serikali, serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, imeelezwa kutoa tishio la kulichukulia hatua gazeti hilo ikiwa halitajitetea.

  Upo uwezekano wa gazeti hilo kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufungiwa katika siku chache zijazo. Hii ni sehemu ya vitisho ambavyo kuanzia sasa vitavikumba baadhi ya vyombo vya habari ikiwamo Jamiiforums na mitandao mingine ambayo itaendelea kuishambulia na kuishushia hadhi serikali.

  Watendaji wa serikali wamesema walikaa kimya kwa muda mrefu na walimshauri JK (na yeye alisema) kuchukua hatua lakini akadharau na sasa nchi imekuwa katika "matatizo" makubwa kwa muda mrefu na hivyo sasa ni wakati mwafaka kuchukua hatua za NGUVU NA HARAKA. "Baadhi ya hatua zimekwisha kuchukuliwa," anasema mtoa habari wa JF ndani ya serikali.


  Tahariri iliyoikera serikali ndiyo hii:

  Serikali iwe wazi, kuna kesi ngapi za mafisadi kortini?


  TAMKO la Serikali lililotolewa jana kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuhusu mjadala ulioibuka hivi karibuni kuhusu tuhuma za ufisadi nchini imeacha maswali mengi kuliko majibu katika muktadha wa utawala wa sheria nchini na mapambano dhidi ya wizi wa mali ya umma. Serikali badala ya kutoa mwongozo, imeonekana kujitoa na zaidi kuwatisha wananchi na wapambanaji kwa kutumia mwanasesere.

  Baada ya kutumia muda mwingi kueleza kuwa mjadala unaoendelea sasa ni 'malumbano ya Rostam Aziz na Reginald Mengi,' na yanayohatarisha usalama wa Taifa, Serikali kupitia tamko hilo lililoandikwa na kusainiwa na Waziri George Mkuchika lakini katika mazingira tata likasomwa na Naibu wake, Joel Bendera, ilionekana kushindwa kuonesha hasira zake na kutimiza ahadi zake za kuchukia ufisadi badala yake ikajidhihirisha kuwa imeanza kusita.

  Serikali hiyo hiyo kupitia tamko hilo hilo moja baada ya kuutaja mjadala huo kuwa ni 'malumbano' ikaishia kutoa ushauri kuwa wahusika wapeleke hoja zao kwenye vyombo husika vya dola. Tunajiuliza 'malumbano yasiyo na tija' yatapelekwa vipi kwenye vyombo vya sheria?

  Lakini katika moja ya mambo ambayo tumelazimika kuyasemea ni kuhusu aya moja katika tamko hilo la Serikali ambayo ukiitazama vyema haiwiani na mfululizo uliokuwa awali kwenye aya nyingine- hii ni kama imeingizwa ghafla ikionekana kumlaumu moja kwa moja Mengi kwa kutaja mafisadi na kumtishia kwa 'kuvunja' sheria huku ikishindwa kutoa tamko lolote kuhusu waliotuhumiwa kwa ufisadi-aliyeibiwa simu ndiye anaitwa mwizi.

  Katika aya hiyo tamko hilo linasema: “Serikali imesikitishwa na kitendo cha Reginald Mengi cha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu , watu kuzungumzia ama kujadili suala ambalo tayari liko mahakamani.

  “
  Kwa kufanya hivyo Bwana Reginald Mengi amewahukumu watuhumiwa hao na kuwatia hatiani bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa (They have been condemned unheard). Kwa mujibu wa sheria za nchi, mahakama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhumiwa.

  Kauli hiyo imetushangaza, kutustusha na kutulazimisha kurejea kwenye kile alichokisema Mengi ambacho baada ya waliotuhumiwa kujitahidi kukipotosha sasa, Serikali nayo inayopaswa kuwa kati, nayo inaingia na kuonekana ikishiriki kupotosha zaidi.

  Kwanza tuweke wazi jambo moja-Mengi katika taarifa yake ya kuandika orodha ya watuhumiwa aliowaita wa ufisadi papa alikuwa akijua alichokuwa akikisema na pia alijua kwamba ukiacha sheria za daawa (civil law) zitakazowapa watuhumiwa hao haki ya kumshitaki kama wataona amewakashifu, hakuna sheria ya nchi hii na yoyote inayomzuia raia mwema kuwataja watu ambao anaamini wanahusika na makosa ya jinai.

  Tofauti na Serikali kujaribu kupotosha kuwa Mengi 'kahukumu,' rejea ya tamko lake inaonesha kuwa alitumia neno “watuhumiwa.” Je, kuna kosa gani hapo kuwataja watuhumiwa tena kwa kujitolea ili wachukuliwe hatua?

  Hoja hiyo inatufikisha katika kujadili kauli tata ya “sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama kujadili suala ambalo tayari liko mahakamani....”

  Kwanza tungeomba Watanzania waelimishwe ni sheria gani ya nchi hii inayokataza “mtu,watu kuzungumzia suala ambalo liko mahakamani,” kama ilivyodai serikali.

  Utafiti wetu umeshindwa kubaini hilo na kwa kuwa limekuwa likitumika kama ngao ya kuwanyima wananchi haki ya kujadili masuala ya msingi kitaifa tunadhani ni vyema hilo likawekwa wazi.

  Sisi wa KULIKONI tunafahamu ipo dhana ya kisheria ya uhuru wa mahakama ambayo pia ina kipengele ndani yake cha kutaka mahakama isiingiliwe katika kufikia uamuzi wake. Lakini kwa bahati mbaya, tofauti na inavyoelezwa, dhana hii haikatazi watu “kutaja” suala lililoko mahakamani wala “kujadili.”

  Kinachozuiwa kupitia dhana hiyo ni kutoa ushahidi au kutaja masuala ambayo yanaweza kuifanya korti ishawishike kuamua vinginevyo, hakuna mahala panapokataza “kutaja” wala “kujadili.”

  Jaji Willem van der Merwe aliyekuwa akisikiliza kesi ya tuhuma za kubaka dhidi ya Rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ni mmoja wa majaji waliotoa jibu ambalo Serikali ya Tanzania inapaswa kulitafakari kama kiigizo na msimamo jadidi ambao mahakimu na majaji wote nchini wanaujua kuliko kuwatisha wananchi kwa kuunda makosa ambayo hayapo katika sheria yoyote.

  Ikiwa kesi hiyo imejadiliwa sana kwenye vyombo vya habari, mitaani, kwenye tovuti na blogu, Mei 8, 2006 aliposoma hukumu hiyo, Jaji huyo alikiri kuwa yeye akiwa mwanajamii hakusita kuisikiliza mijadala mbalimbali nje ya mahakama wala kukwepa kutazama mijadala kwenye televisheni, lakini mwishowe alihukumu kesi hiyo si kwa kutumia mijadala hiyo bali ushahidi uliowasilishwa kortini na pili sheria za nchi na si vinginevyo.

  Mkuchika awaeleze wazi Watanzania ni sheria gani inayounda kosa la “kutaja” au “kujadili” kesi zilizoko mahakamani?

  Tamko la serikali pia limesema Mengi amejadili masuala yaliyoko mahakamani, baada ya kuona kuwa hakuna mantiki kusema watu hawana haki ya kujadili masuala yaliyoko mahakamani, pia tuzungumzie sasa kauli hii japo kwa uchache.


  Wananchi wengi wanaamini kuwa Serikali ina watu makini na wanaofanya kazi kwa viwango. Tamko la jana limedhihirisha hali ni tofauti.


  Wakati Serikali ilitarajiwa ingetoa tamko lililofanyiwa utafiti, jana imeonekana kukariri maneno yale yale yaliyotumiwa na baadhi ya watuhumiwa na mashabiki wao waliochangia mjadala wa ufisadi kwa kutoa madai potofu kuwa Mengi kataja masuala ambayo yako mahakamani. Hebu twende pamoja katika hili.

  Watuhumiwa watano waliotajwa kwa ufisadi papa ni Rostam Aziz, Yusuph Manji, Subash Patel, Tanil Somaiya na Jeetu Patel.

  Katika watuhumiwa hao ni mmoja tu ambaye kwa sasa walau yuko mahakamani tena kwa kesi ya ufisadi wa EPA, Jeetu Patel, ambaye katika tamko la Mengi hata hivyo hakuna mahali, tuchukulie kuwa ni kosa kutaja suala la mahakamani, alipotajwa au kujadiliwa na Mengi kwa sababu ya kesi yake hiyo iliyoko sasa mahakamani.

  Watuhumiwa waliobaki, kwa sasa hawana kesi yoyote mahakamani ya kuhalalisha 'kosa' la Mengi kama lilivyoelekea kufanya tamko la Serikali. Sasa kimetumika kigezo gani kusema kwamba watuhumiwa hao wamehukumiwa kabla mahakama haijafanya hivyo?

  Je, huku si kurudisha nyuma kwa dhahiri mapambano dhidi ya ufisadi, mapambano ambayo wananchi wamekuwa wakiambiwa washiriki kwa kuwafichua waovu?

  Je, huku sio kulinda mafisadi kwa mlango wa nyuma? Je, huku si kuacha sheria nzuri na dhana nzuri ya utawala wa sheria ambayo haiwapi mafisadi nafasi na kuanza kukumbatia 'sheria za watawala' zinazowapa ahueni mafisadi?

  Tunachoweza kuishauri tu kwa sasa Serikali ni kwamba wanafalsafa na wahenga wameshaonya: “Unaweza kuwapumbaza watu wachache tu na kwa muda mchache, lakini huwezi kuwapumbaza watu wote na kwa muda wote.”
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana lakini pia haishangazi. Mwenendo wa serikali ya Kikwete (hasa waziri wa habari) ulikuwa unaelekea huku. Walidhani kuwa wakifungua kesi hewa za ufisadi basi vyombo vya habari vyote vitapiga vigelegele na kusifia juhudi za serikali ya awamu ya nne.

  Baada ya kuona kuwa hakuna kinachobadilika, wamerudi kwenye kitabu ambacho viongozi wengi madikiteta wakiafrika hutumia kuongoza - dhibiti vyombo vya habari. Hata hii JF wamekuwa wakipanga mkakati wa muda mrefu wa namna ya kuidhibiti. Binafsi, sioni ajabu kama wakifungia kulikoni.

  Naungana na Nyani Ngabu ...... miafrika (viongozi mifisadi ya kiafrika) ndivyo ilivyo.
   
 3. S

  SpinDoctor Member

  #3
  May 12, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yoyote iliyojaa watendaji waliopenyezwa kwenye nyadhifa zao kupitia urafiki au upendeleo huku ikilenga kutimiza matakwa ya watu fulani ni lazima ifanye vitisho kama hivyo. Ila kuna kitu kimoja huwa kinasahaulika, nacho ni kuwa unaweza kuzima vuguvugu za vyombo vya habari lakini kadiri nchi itakavyozidi kuporwa na maisha ya mwananchi yakizidi kuwa magumu; wananchi watadai haki zao....mifano inaonekana kule Busanda....
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,258
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana lakini pia haishangazi. Mwenendo wa serikali ya Kiwete
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mmh.. basi kesho itakuwa vurugu maana miye ndiyo nimefyatuka!
   
 6. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Binafsi naona Serikali na washauri wake wanakoelekea ni kubaya. Hata mimi nilivyosoma ile tangazo la serikali kuhusu Mengi na Roast nilibaki na maswali mengi kuliko majibu. Who wrote, Objective yake nini, For what and Why so ??. Moja kwa moja ilionekana ni Tangazo ambalo mawazo yaliyoandikwa yamekoka kwa one of the Mafisadi na the so called washiriki.

  Huwezi kutaja vyombo vya habari vichache ukiacha chombo cha serikali kilichotumika na one of the Fisadi zaidi ya 10 Minutes kama Rais wa nchi akitoa hotuba kwa waTanzania!!! Na wala hajakemea kwa hiyo waziri huyo arifurahia sana kuona TBC inafanya vile. Na ndani anang'ang'ania yale yale mawazo ya mafisadi kwamba ushahidi upelekwe kwenye vyombo husika yaani PCCB . What the hell is this rotten PCCB !!! , ambayo bila hata aibu hadi juzi bado Boss wake anazidi kuwachefua Watanzania kwa kuzidi kuitetea Richmonduli !!! .

  Yaani ameshaona Watz wajinga sana watakuwa wameshasahau. Kwa hiyo wanachoogopa kupeleka mahakamani nini?? si waende mahakamani ili Mengi apeleke ushahidi wake huko!!! Kwa nini waogope, na kwa nini Serikali inawatetea, Hapa wananchi wenye akili watafikia kikomo cha uvumilivu.
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,497
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280

  chama cha mapinduzi daima (ccmd) = chama cha ma-spin doctors)
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii "tahariri iliyoikera serikali" ni response ya KULIKONI kwa kile SERIKALI serikali ilichosema jana, Jumatatu, tarehe 11, kupitia Naibu Waziri Bendera, hivyo hii makala ni ya leo, Jumanne tarehe 12.

  Leo hii hii KULIKONI wametoa makala, na leo hii hii serikali ikatoa tishio, na leo hii hii "mtoa habari wa JF ndani ya serikali" akainasa data na kukuletea, na leo hii ukaja bandika "tetesi" hapa..du, vyanzo vyako vikali. "Tetesi"...
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kama hutaki unasema "sitaki".. unabisha.. kwani yote hayo hayawezekani kufanyika ndani ya siku moja!?
   
 10. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Majibu ya maswali yako yote hapo juu ni .... NDIO mwalimu
   
 11. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Swali gani?
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  hilo hapo ^^^^^^
   
 13. H

  Hongasuta Member

  #13
  May 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2006
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni miongoni mwa tahariri nzuri zilizowahi kuandikwa na magazeti ya Bongo. Ni very objective na imeeleza ukweli mtupu. Sasa ukweli unauma? Hebu wajaribu kulifungia hilo gazeti halafu waone moto utakaowaka. Sijui atauzima nani! Watanzania sio wajinga kama wanavyodhani. Sasa kumepambazuka!
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huu ni wakati wako, na hii ni taarifa yenyewe, na hizi bado ni tetesi, hadi pale serikali itakapotangaza rasmi, kwa taarifa itakayoandaliwa mahali pale pale na kupelekwa kule kule na kutolewa na wale wale, mahala pale pale.

  Hivi ndivyo ilivyo katika nchi ile ile, inayoongozwa na wale wale, kwa mbinu zile zile, kama walivyofanikisha wakati ule kule kule ambako teacher alimpa yule na kumnyima huyu.

  Na wataendelea kuwaunganisha kama walivyowaunganisha wale kule kule kwa kesi zile zile ambazo wale wale hawaguswi, kwa kuwa ni wao wao wenye kuongoza pale pale panono wanakowaweka wale wale waliowafanya vile vile wenzao kwa kuwachora vile vile.

  Lakini, Watanzania wale wale ndio hawa hawa ambao leo wamegeuka na kuwa sio wale tena bali hawa hawa wenye sugu katika vichwa vyao na sasa kule kule wanaendelea kuwasha moto kama ule ule wa MwembeYanga
   
 15. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Kwa tahariri kama hii hata wewe unge-react. Imetulia.

  Mimi naamini nchi yetu inakoelekea siyo kuzuri. Maana watawala wameshindwa kujenga nyufa. Itabidi jengo libomoke..na wote tuanze kujitwisha matofali kulijenga upya. Kwa watakaokuwa wamebaki.

  Kama tunataka maendeleo ya kweli hatuna budi kupita kipindi kigumu kama hiki KINACHOKUJA. Kwa wale waliofikiri maendeleo na mapinduzi ya kweli yanakuja kwenye silver plate..were day dreamers. Be prepared kuona watu wanaswekwa jela na wengine kunyanyaswa than you have even seen. We just have to undergo this stage!

  Ningewashauri watanzania..kwa sasa ndo kipindi cha kusimama KIDETE na kuexpose madhambi ya hii serikali yetu. It has failed us. And we just cant take it any more. Its too much. Ofcourse wengi wetu ni waoga. LAKINI at some point lazima wajitokeze kondoo wa kafara! Kwa nini hata sisi TANZANIA ni sehemu ya ulimwengu hatuwezi kuikimbia historia.

  Haiwezekani taifa la watu million 40 tuwe wajinga kiasi hiki kwa siasa za akina Mkuchika na Rostam wanaoangalia matumbo yao na mabwana zao. Something needs to be done1 Huu unafiki wa amani na umoja wakati keki wanakula wachache at the expense of millions. No way it has to end at some point.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  this makes absolutely no sense.. yaani kuguswa Rostam ndiyo imekuwa hivi.. basi tumuache tu kama mmoja alivyotutaka
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Jamani serikali kamwe haliwezi kulifungia gazeti la Kulikoni kwa mdngisababu kwa kulifungia kulikoni, serikali itakuwa imempatia Mengi kile anachokitaka. Hivyo kwa sasa inamuogopa Mzee Mengi kama ukoma, haiweyi kuthubutu hata kidogo.
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  "Serikali ya Kikwete imejaa mafisadi, wanapumua ufisadi, wanaongea kifisadi, wanatenda kifisadi, wanaamua kifisadi, na wana mwelekeo wa kifisadi" - author - in my pocket (mfukoni).

  Watafanya kile ambacho wanaendelea kufanya kila siku - ufisadi.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi mnafikiri hata Jk mwenyewe anajua kinachoendelea? Jamaa wamemuwekea ukuta kiasi kwamba sitoshangaa suala la Rostam na Mengi bado hajalisikia! Ni wa mwisho kujua kinachoendelea, msiniulize kwanini.
   
 20. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo ndo patamu, wanadhani watanzania bado ni mandondocha? not anymore! tumechoshwa na unyonyaji wao! something has to happen, indeed it must happen soon!
   
Loading...