Mendelian Inheritanc
Member
- Dec 25, 2011
- 86
- 11
tatizo ccm imeshalaaniwa...
Tatizo sio kulaaniwa tu mkuu PIA ukumbuke SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA..
tatizo ccm imeshalaaniwa...
ni kweli kabisa ndugu Bufa..., migomo haina tija na inarudisha maendeleo nyuma. ila si kwa nchi kama tanzania. iweje uendelee kuumia na kazi wakati kinachopatikana hakifanyi kazi iliyokusudiwa????. kinaishia mikononi mwa wachache wanaojilimbikizia mali. tunalipwa kidogo n bado tunakatwa kodi kubwa ambayo hatuoni inachikifanya. UKITEKA MAJI MBALI NA KUYAMWAGA KWENYE PIPA LINALOVUJA, NA BADO UKAENDELEA TU, HAKIKA UTAKUWA MWENDAWAZIMU. ziba matundu kwanza ndo uendelee kuweka maji. Migomo inaweza saidia kidogo kwa hilo.Nchi masikini ya pili kutoka chini na bado tunamuda kibao wa kugoma huku tunataka tuendelee, Labda mbingu zishuke ndo bongo itaendelea.
Jana nilimuona kwenye gazeti moja la kila siku akiwa anaongea na mama mmoja huku akiwa amelala sakafuni........sikuelewa maana yake ni nini, au ndo anajihami kutokana na sababu ulizozitoa hapo juu?Kipindi cha mfungo si ndicho ambacho DHAIFU huwa anaanguka!, akisikia hivyo lazi asalimu ardhi. yangu macho.
hakuna nchi maskini labda wewe mwenyewe watu wana fedha nje ya nchi zaidi ya bajeti ya serikali ya mwaka usema nchi maskini ,ungesema nchi yenye watu waroho na wabinafsi ningekuelewa.
Tanzania si maskini hata kidogo
Roho za mabalaa zinamwandama kwa kuwa ulinzi wa majeshi aliyoahidiwa na Sheikh Yahya umeyeyuka!! Asipotubu na kumrudia muumba wake, huo ndio mwisho wake!!Ili kupunguza hizi stress dr feki itabid asafiri nje ya nchi kodogo
Tumbo la kuhara laingia Magogoni
Jamiiforum ni jukwaa tosha. Na usidanganyike hao watendaji wakuu wa serikali wanatembelea humu kwenye hili jukwaa kwa sana kusikia kinachoongelewa.
hakuna kitu hapo danganya toto hiyo hahahhh
Nchi masikini ya pili kutoka chini na bado tunamuda kibao wa kugoma huku tunataka tuendelee, Labda mbingu zishuke ndo bongo itaendelea.
Madaktari mgomo wanini tena wakati wameshaambiwa asiyetaka aache?au wanakuja na madai mengine tofauti na yale ya kwanza?
Ulichosema ni kweli kabisa,ninacho kiona mimi tatizo lipo kwa watunga SERA! kwanini? WANABAGUA WATUMISHI. idara ya kilimo mishahara yao ni mizuri sana lengo lilikuwa ni kuwashawishi waweze kukaa vijijini ambako ndio kwenye mashamba na wakulima pia. lakini wakasahau kuwa huko vijijini kuna walimu wengi tu ambao nao wanahitaji motisha.Jambo hili linaleta manung'uniko miongoni mwa watumishi wa umma.haiwezekani mwalimu alipwe tshs 300,000 mtu wa ugani akaanza na tshs 700,000/= na wote wanaishi kijiji kilekile na wote wana shahada za fani zao.Ni kweli kuwa mishahara ya wafanyakazi walio wengi ni midogo sana kumudu mahitaji muhimu ya binadamu. Lakini tuangalie chanzo ni nini? how can we move forward? je kulalamika kwenye mitandao is a solution? kwa nini tusiombe jukwaa tukayazungumza wakiwepo watendaji wakuu wa serikali? tujaribu kuangalia njia mbadala ya kurekebisha hali. Mawazo yetu yatasaidia. Lakini kwa halli ya sasa ilivyo ya uchumi mishahara mikubwa haitawezekana na huo ndio ukweli. Ingawaje vitu vinaweza kufanyika mambo yakawa mazuri. PIa tusipende ku generalize issues. Sio wote walioko CCM ni wabaya na sio wote walioko upinzani ni wazuri huo ndio ukweli. Watanzania bado tuna ubinafsi mkubwa na hiyo inachangiwa na sera za nchi yetu.
We sijui ndo wa wapi unataka kusema bongo ni tajiri? acheni kujidanganya wabongo kwamba nchi yenu ni tajiri, mbuga na milima pekee havifanyi nchi kua tajiri.Wewe vipi? Nani alikuambia kuwa nchi yetu maskini? Wewe ni magamba?