Tetemeko dogo la Ardhi(aftershock) latikisa tena Bukoba usiku Sept 11, 2016

Poleni sana.nashauri serikali inabidi ilete wataalam wa kimataifa wafanye tafiti za kisasa ili kuwe na tahadhari, sio kuishi kwa kubahatisha
 
Hali hii hutokea na mara nyingi matetemeko yanayofuata huwa ni madogo ukilinganisha na tetemeko husika ila mara chache yanaweza kuwa makubwa zaidi kuliko tetemeko husina na ndiyo sababu waliothiriwa na tetemeko la ardhi hushauriwa kulala nje kwa siku chache (inaweza kuwa wiki moja au hata zaidi) mpaka hapo itakapoonekana kwamba hali imetulia.

Hii hali inaitwa "afterquake". mara nyingi inakuwa na magnitude kidogo kuliko tetemeko lenyewe lakini mara nyingi huwa na madhara makubwa kama hakuna tahadhali.

hii hutokana na kwamba nyumba zilizoathirika na tetemeko hubaki na ufa ama ubovu usioonekana waziwazi sasa afterquake inapotokea hupelekea nyumba hizo kuanguka kabisa. hii ndio sababu hushauriwa maeneo yaliyoathirika na tetemeko watu wakae nje ya nyumba kwa kipindi hadi wiki kmoja. afterquakes inaweza kutokea kwa zaidi ya mara moja
 
Poleni sana ndugu zetu,tuko pamoja ktk maombi lakini pia la msingi ni kuchukua tahadhari kwa kuwa eneo salama zaidi kama kulala eneo la wazi mradi usalama uwepo,kujikinga na baridi na mbu has a watoto kwa usiku huu.
 
Nadhani watu mtaanza sasa kuthamini hii Amani tuliyonayo maanake mmeanza kuishi maisha wanayoishi wasomali wa Mogadishu.

Nyie mtakuwa mabalozi wazuri wa amani nchi hii.
 
Mwanza na hayo mawe sijui itakuwaje!!
Any way Mungu atunusuru na haya majanga asili(natural disasters)
kwenye milima mingi nguvu/madhara ya mitikisiko ya tetemeko huwa nackiaa sioo kubwa sana kama maeneo ya tambarare
 
Back
Top Bottom