Tested HIV positive, looking for a soul mate

Nimeuliza ili awe specific,njia zipo nyingi sana nilizisoma kwenye biology mwaka 1997(Kuna sexual intercourse,blood transfusion,accident,sharing of sharps instruments with infected people etc)

Haitoshi kuwa specific kwa ninayemhitaji? Unaonaje hapo? Thanks.
 

Hongera kwa ujasiri. walau ulipima japo haikuwa kwenye Plan. Hivi tunavyotembea na huwa hatupimi sijui jamii yetu ipoje. Unasema unajijua ulikuwa clean mkuu so baada ya mwezi wa 8 hukuwa na mahusiano na mtu kabisa au? sijaelewa kidogo ?


All in all , you are a hero and May God make you stronger and healthy.
 

Amiin! Kupima haikuwa kwenye plan siku ile lakini huwa sina tatizo katika kupima. Sikuwa na mahusiano kinyau. Kwaheri ee!
 

Kwa sasa sina hofu ya kutetwa, labda natetwa kwa mazuri tu. Kwa hiyo nitakuwa makini katika maamuzi kwa kuzingatia mazingira yangu ili nisijisababishie tatizo. Nitapima faida na hasara ya maamuzi mbalimbali. Incharge yuko sahihi kwa maoni yake, nawe pia uko sahihi kama nlivyowahi kukwambia kuwa ujumbe wako ni muhimu; lakini ni kawaida wakati mwingine binadamu kutofautiana kimtazamo kama ilivyo kwenu. Kazi kwangu sasa kuyatafsiri mawazo yenu katika mazingira yangu. Nawashkuru sana mnavyozidi kunijenga
 
Mkuu Pave,kwanza nikupongeze kwa moyo wako unaounyesha ktk issue hii kwa kuwajali wenzanko kwenye wakati huu mgumu kwako,hakika Mungu ndiye anaejua atakulipa nini,ushauri wangu kwanza:-weka akilini mwako kwamba lazima ipo siku utawaambia ndugu zako,rafiki zako na wafanyakazi wenzako kuhusu afya yako,(2)omba Mungu akujaalie upate mke mwema kadiri ulivyoomba,pia akujaalie mpate mtoto/watoto kisha ndio ugeukie kuwaambia ukweli jamaa zako,naamini hapo...watashtuka ila watafarijika coz watakuona una mke wako,mna mtoto wenu na ana afya nzuri tu na utaonekana ambaye huna wasiwasi kwani wakati huo nadhan utakuwa na amani moyoni.wala usijilaum kwa lolote maana hakuna aijuaye kesho yake,hayo ni maradhi mtu yeyote anaweza kuyapata pasi'nakutegemea..nakutakia maisha marefu na Mungu akuzidishie moyo wa huruma wakati huu unapohitaji kumpata mwenza wakuifanya kazi yake aliyokutuma hapa duniani,amini Mungu hampi kisogo mja wake ni kiasi cha muda tu utatimiliziwa hitaji lako,kila la kheri kaka...Asante!
 
Last edited by a moderator:
For what? Utawakamata wengi kwenye story yako ya kufanya research.

Sio vizuri mkuu,muache tu mdau madhali hajaja kukuhoji hapo ulipo sidhani kama ni sahihi ku-judge alichokiandika hapa...unless uniambie kakushikia bakora kwamba usome bandiko lake na kukulazimisha ucomment,matatizo tumeumbiwa wanadamu ndugu yangu usim-beze mwenzako kesho yakakukuta na wewe ukakosa faraja...ni maoni tu mkuu.
 
Pave unaniconfuse na sorry kwa kuuliza uliza : Inawezekanaje umepima August huna na after sometime unao na unasema hukuwa na mahusiano. Au ulikuwepo haukuonekana kwa sababu ya window period? Am so sorry but please clarify
 

Ahsante na imebidi nifrahi kuona ni kama umeyasoma mawazo yangu. Kila kitu ni hivyo hivyo; yaani najua uwezekano wa kuwaambia baadhi ya ndugu upo, lakini ni pale ambapo wataona mke na mtoto au watoto na mambo mengine yakiwa kwenye mstari. Kwa sasa labda itokee dharura itayonilazimu kufanya hivyo, vinginevyo niko okay.
 
Last edited by a moderator:
Pave unaniconfuse na sorry kwa kuuliza uliza : Inawezekanaje umepima August huna na after sometime unao na unasema hukuwa na mahusiano. Au ulikuwepo haukuonekana kwa sababu ya window period? Am so sorry but please clarify

Kwa udadisi wako nilihofia kukukanganya, na sasa imetokea. Lakini tambua mambo yote yanamajibu na jibu lolote utakalojitwalia ni sawa tu kwangu- haitanisumbua. Tafadhali hapa zingatia zaidi hitaji langu. Nilitumia neno 'inawezekana' kwa kuwa sikutaka iwe ndio jibu la moja kwa moja. Na dhumuni la kutaja kile kipindi ni kutaka nitoe picha kuwa yawezekana sikuwa nao muda mrefu kwa hiyo mtu anaweza ku imagine afya yangu japo kwa sasa nimesikia kuwa wengine hupata athari kiafya muda mchache baada ya maambukizi. Ningeweza kusema hivi, "Huwezi gundua kuwa nimeathirika maana ndio kwanza nawaza nidhibiti mwili wangu kunenepa, uzito nlikuwa nachezea 65 sasa 70 + huku tatizo la kuvusha mida ya chakula ninalo sana ninapotingwa na kazi, na stress za kazi na maisha kwa sana, najiwazia mimi na nawaza kufanya mabadiliko makubwa kimaendeleo katika familia yangu kwa ujumla jambo lililosababisha nichelewe hata kuoa, muda wangu wa kupumzika ni mdogo na mihangaiko ni mingi....." Pamoja na hayo yote status ndo hiyo na wala sikubagua anayetumia dawa. Ukiniuliza mimi binafsi nimepataje nitakwamba bado sina jibu la uhakika. Je? nitumie muda mwingi kutafuta ilikuwaje au niwekeze kwenye suluhu?
Nilimaanisha kukwambia kwaheri Kinyau , lakini kwa kuwa umeomba nikaamua kujibu tena. Sasa malizia na uje na jingine.
 

Naomba ayaelewe vizuri maoni yako
 

Mungu ni mwema mkuu amini mambo yatakuwa kama ulivyopanga kwa uwezo wake..mtu anakatwa miguu yote na mkono mmoja na anaishi itakuwa mtu kuwa HIV-ve,nguvu unazo kazi unayo nenda taratibu kaka yani bila hofu yoyote utayafikia malengo yako bila wasiwasi wowote.
 
Hongera sana mkuu kwa ujasiri,iwe fundisho kwa waathirika wengine wanao nyong'onyea kwa mawazo na kukosa matumaini.Hope you get the right one.Blessed
 

Amina mkuu! Mungu akuongezee busara na hekima. Pamoja!
 
Hongera sana mkuu kwa ujasiri,iwe fundisho kwa waathirika wengine wanao nyong'onyea kwa mawazo na kukosa matumaini.Hope you get the right one.Blessed

Asante sana mkuu. Mungu atufanyie wepesi panapo uzito.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…