Terminal ya Clouds FM wanapiga kampeni michango ya Harusi.

Wachaga hawawezi kukuelewa kwao kuchangia Sio swala la hiari ni la lazima utake usitake.Unakuta mwenyekiti anafoka kuwa kima Cha chini hiki hapa utatoa wapi utaiba au vipi lazima utoe
Mimi ni mchaga, kwanini mtu anisumbue wakati sio ndugu yangu?
 
Naunga mkono hoja... ukitaka kuoa jipange...

Michango ya watu siyo lazima...



Cc: mahondaw
 
Ungewapigia simu na kuwasilisha hoja yako kuwapinga
 
Wachaga hawawezi kukuelewa kwao kuchangia Sio swala la hiari ni la lazima utake usitake.Unakuta mwenyekiti anafoka kuwa kima Cha chini hiki hapa utatoa wapi utaiba u utatoa wapi utajijua lazima utoe
Safi sana hii, kusaidiana hata kwenye mitaji hili hufanyika
 
Lkn sasa wa tz misiba wanatoa buku na mgonjwa wanaenda kumuona na chupa ya chai na maandazi ya jero lkn harusi kamati 100000,double 70000 na single 40000 mpaka kadi zinaisha.
Upuuzi mtupu
aaaaahhhhhaaaaaaaahhh
 
Watanzania wakiambiwa wachange pesa ya kuwasaidia hao maharusi kuanzia maisha na sio kwenda kunywa na kula hawawezi kukubali.
 
Kuna wakati kuna jamaa yangu alikuwa anafatilia michango kufanikisha harusi yake. Kuna boss mmoja alimsumbua sana. Boss katoa ahadi lakini jamaa kila akienda anakula kalenda. Siku moja akamuita na akaanza kumpa wosia mrefuu kama wote vile halafu akamkabidhi jamaa elfu 10 km mchango wake. Jamaa yngu kila ukikutana nae anasema hajawahi kumsahau yule bwana ktk maisha yake.
 
Hajamsahau kwa mchango mdogo au wosia?
 
Nisicho kipenda mm kwenye michango hii ni kuwekewa kiwango alafu unakuta hakishuki 50k kwa single & 80k kwa double
 
Mkuu mimi nikienda harusini /send off either directly nimechangia 70k au cost sharing( kuchangia 35k watu wawili), nahakikisha
Napiga supu
Napiga wine( full chupa nzima mezani)
Karanga zile
Napiga msosi wa maana( highly selective- items)
Ikifika kwa zawad... natoa mkono au naondoka kabla.
 
Hata mimi naunga mkono, sijawahi kuchangia mtu harusi na sitakaa nichangie. Siku ya harusi yangu napanga budget ya watu 150 tuu basi bila kuchangisha. Hizo zama za michango zilishapitwa na wakati tubasilike.
 
Kuchangishana harusi ninkuendekeza umasikini . Mwalimu Nyerere hakufundisha kuchangia bia na kusaza ila kuchangia maendeleo.

Nawaunga mkono terminal tufikie mahami tuchangie elimu afya na mitaji na si harusi ni aibu kufanya sherehe kwa mifuko ya watu. Kama huna ishi within your means.
 
Kwann uoe Kwa michango ya wengine ?? Hii tabia mbovu ipo Tanzania Tu,
 
Chinua Achebe alisema ...Ukiona mtu anatoka kwake anaungana na wenzake kwenye mbalamwezi usiku..sio kwamba kwake huo mbalamwezi haumuliki lkn ni kwa sababu ni vizuri watu kukaa pamoja na kujumuika, huu ndo utaratibu wa kiafrika...mila zetu zimetujenga hivyo...
Hivyo hata michango ya harusi...ni kitu chema watu kujumuika...pili michango sio lazima, hakuna mtu atakae kupeleka polisi au mahakamani sababu hujamchangia harusi...Cha msingi jipime tu..uwezo wako.....
Kama huna hela kausha tu.....lkn ujue sherehe ni watu, watu ndo sherehe....na ndo maisha hayo....Furahi na wanaofurahi, lia na wanaolia.....kusaidiana kupo tu......

Mtu anaesema et atawaalika ndugu, wajomba etc..hivi ni kweli kwenye maisha ndugu tu ndo wanatushika mikono au kutuma connections etc......???Tafuta watu wa karibu marafiki, ndugu etc..washirikishe...sherehe ipendeze...Mwisho wa yote haya ni Futi Sita....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…