Tengeneza muziki mzito kwa kununua vifuatavyo

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Wakati nipo chuo kuna watu walikuwa wanasumbua sana na subwoofer zao mpaka wanawake nikaona huu ujinga sasa kila mtu subwoofer la kichina nikapata wazo la kutengeneza mziki mkubwa sana wa kuunga unga nikanunua vitu hivi.
  • Car audio crossover and equalizer
  • Car music booster
  • Spika 2 za bass ( woofer ) za kwenye magari aina ya sony
  • Tweeters 2 ndefu za home theater
  • Transformer inayopokea AC na kutoa DC 12 V ampia 15
  • Redio ya gari
  • Nikatafuta fundi wa kuchonga box za spika akachonga box mbili za bass spika 12 inch ndani ya box akajaradia na godoro nyembamba.

Nilipoufunga huo mziki nakwambia vijana wakifanya visherehe vyao chuoni walikuwa wanakuja kukodi mziki kwangu nilinyamazisha vi subwoofer vya mchina vyote.

Fanya hivyo utaniambia mzee baba....💪💪💪💪
 
Deep bass hapo unaipata mzee nzito hasa.
  • Bass spika 2 👉 300,000
  • Equalizer & Crossover 👉 200,000
  • Radio 👉 80,000
  • Transformer nenda kwenye mitumba utapata nzuri sn 👉 30,000
  • Booster 150,000.
  • Box spika 👉 100,000.

Gharama inakuwa kiasi gani? Nahitaji deep bass kwa low volume.
 
Wakati nipo chuo kuna watu walikuwa wanasumbua sana na subwoofer zao mpaka wanawake nikaona huu ujinga sasa kila mtu subwoofer la kichina nikapata wazo la kutengeneza mziki mkubwa sana wa kuunga unga nikanunua vitu hivi...
Hatari sana kwa wapenda mziki mkubwa. Mimi sound bar tu inanitosha kwa matumizi ya nyumbani. Hata kwenye gari speaker za gari tu zinanitosha maana nikipiga mziki mkubwa masikio uwa bjioni yanakuwa kama yamejaa maji yani kama vile niliogelea. SIjui nina shida gani, hata nikitumia headphone napata hili tatizo, lakini sina jinsi wka kazi nnayofanya kuna siku alzima nizitumie siku nzima.
 
Deep bass hapo unaipata mzee nzito hasa.
  • Bass spika 2 👉 300,000...
Milioni hiyo tayari!

Hivi vyote vinakaa sehemu moja au kila kimoja na kwake?

Maana vyumba vyenyewe ni vidogo siku hizi!
 
Upo sahihi mtoa post , mm nilinunua radio nyingi nikawa sipati nikitakacho KUMBUKA redio za maana nizile za kijapan ENZI za mkapa za CD Ila sio sikuhizi.

Sasa nilichokifanya nilinunua subwoofer speaker mbili za gari pioneer TS-W309D4 watts RMS ni 400 kila moja Kisha nikafunga ktk box moja kubwa Kisha nkadaka equolizer ya Boschmann na booster/amplifier yake + tweeter za pioneer Kisha nikaunganisha na home theater yangu ya Sony nikaondoa Ile subwoofer yake tu, japokuwa booster inatumia power supply kubadili mfumo wa umeme hivyo kuhusu mid speakers ninatumia moja kwa moja za home theater Yani pale niliongeza bass tu, aisee Mziki ninaokula asikuambie mtu BINADAMU wanapenda sound Yani majirani zangu wananitembelea kila siku kisa tu wasikie sound na Kuna majirani Kama wanne walishafanya hivyo.

Kuna Jirani aliniuliza napataje Ile deep bass nikamuuliza subwoofer yako uliinunua kwa kiasi gani, akaniambia 100,000/= nikamwambia unaziona hizo speaker ktk box, Sasa Ile speaker moja nimeinunua kwa 150000 jumla laki3 hizo mbili , nikamuuliza subwoofer yako Ina watts RMS ngapi akajibu ni 80rms nikamwambia izo spika zangu jumla ni RMS 800 ,JE tunaweza kufanana ktk sauti?

Alicheka Sana na hapo alianza kujichanga, nilichomshauri kulingana na uchumi wetu kufanana nibora aanze kununua spika mdogo mdogo kwani akishapata spika nirahisi kupata booster, equolizer n. K Kwan spika ktk Mziki ndio nguzo na inatakiwa km unataka spika2 basi zilingane kilakitu hasa watts, Herts/Hz/Ohm, size(inch),mwonekano(Toleo) n. K...

👉Chukueni huo ujanja hutojuta jichange mdogo mdogo unda sound nzito utajikuta unajihisi Amani KUSHINDA home😁
 
Nataka booster ya gari nitumie na receiver yangu. ile nafanyaje mkuu? na inatumia umeme wa dc?
Utakachokifanya Kama head units yako(receiver) ina audio out put kule nyuma utatumia kuunganisha na hiyo booster ya gari na Kama Haina out put utakachokifanya Kama una booster TU na umenunua booster kusukuma subwoofer maana yake utachukua waya utaunganisha ktk spika za nyuma(rare speaker) kwenda ktk channel ya Rare speaker Kama booster ni channel 4 kwa sababu rare out put ya redio inatoa freequence za chini hii Ni nzuri kwa subwoofer hata ukiunga ktk rare channel ya Amplifier utapata bass lenyewe kuliko KUTOA ktk front speaker ambayo inatoa freequence za juu ambazo ni sauti nyembamba,

Ila Kama una equolizer basi utachukua waya utaunganisha na spika za radio yako hasa front speaker ili kupata full range sound utaipeleka ktk in put ktk Ile equolizer Kisha ndio utaunga na booster.

image_downloader_1645559531450.png
image_downloader_1646137691963.png
Screenshot_20220222-164309.png
image_downloader_1646137512936.png
 
Utakachokifanya Kama head units yako(receiver) ina audio out put kule nyuma utatumia kuunganisha na hiyo booster ya gari na Kama Haina out put utakachokifanya...
Kuhusu booster ya Gari utakachofanya utanunua power supply ya computer ukienda mjini hasa kariakoo zinauzwa ama nenda kwa fundi utanunua transformer inayotoa 12-13.8 v Yani kubadili umeme wa AC to DC hii inaifanya booster kupokea current za kutosha kusukuma spika ya bass ya gari maana zinanguvu mno zinahitaji current za kutosha , unajua umeme wa nyumbani una voltage kuanzia 110-240v lakini current hua ni 20 wakati voltage za gari ni 12 Hadi 14 lakini current hua ni 70,40
 
Ukiona kimya humu basi nicheki fb kwa jina Naligia Mninoi, siweki namba kwa sababu maalumu , kule fb Nina darasa kuhusu Ukiroho na watu huitaji Namba zangu ambao humu pia wapo , so ukija fb NITAFUTE kwa yeyote anaetaka ushauri tusaidizane wale music lovers✌️profile ni Kama hiyo picha utanitambua
 
Kuhusu booster ya Gari utakachofanya utanunua power supply ya computer ukienda mjini hasa kariakoo zinauzwa ama nenda kwa fundi utanunua transformer inayotoa...
hili hasa ndilo jibu nililotaka. kuhusu kuunganisha haina shida naelewa na receiver ina rca output ya subwoofer.

Power supply nanunua ya watt ngap? au yoyote tu?

psu inakuwaga na mapin mengi naunga wapi pale?
 
Nunua spika utakalo mm nashauli tafuta spika ya watts 400 RMS yenye p. M. P O Yan max watts 1400 ya NCHI 12 Yani ukubwa, Dukani zipo za pioneer, JBL, kwa Bongo japo zipo kampuni nyingi Ila kwa Sasa hizo ndio zipo sokoni kwa Bongo , nunua hasa pioneer , Kisha tafuta booster itakayo drive, Kama booster IPO basi inatakiwa Kujua ukubwa wake(watts) na ujue hiyo Ni mono amp Yani njia moja TU ya subwoofer au ni njia 2,3,4.

Yani (channel 1,2,3,4) Kama ni mono amp basi chukua out put ya receiver peleka ktk Amp lakini Kama amp yako ni channel4 basi usichukue ktk subwoofer output ya receiver utapata bass bovu Bali chukua KUTOKEA ktk spika za nyuma Rare speaker kwa sababu Rare speaker Ina freequence za chini na za chini kiasi kwani ni 20hz Hadi 500 Hz hivyo Subwoofer yako ikiwa na uwezo wa kukokotoa Hz kuanzia 20 Hadi 250 Hz maana yake Spika itatoa zaidi milio kuliko ukitoa ktk subwoofer output Kama spika Ina piga freequence Hadi 250 maana yake output ya receiver inaishia Hz180 hivyo basi litakosa full range ya deep bass.
 
hili hasa ndilo jibu nililotaka. kuhusu kuunganisha haina shida naelewa na receiver ina rca output ya subwoofer.

Power supply nanunua ya watt ngap? au yoyote tu?

psu inakuwaga na mapin mengi naunga wapi pale?
Dah sory nimejibu swali tofauti nilijua unauliza ununue spika za ukubwa gani , Ila kwakuwa niliandika kwa kina sijafuta jibu kwa faida ya mtu mwenye swali Kama nilivyohisi, sory

Ok swali lako kuhusu power supply ununue ukubwa gani kwakweli Huwa sijui zaidi mm nilinunua transformer fundi akafanya yake Ila ukiingia mtandaoni power supply wanazipromote Sana kwa car Amp kutumika home hivyo jaribu kuperuzi utapata jibu now.

Yote ya yote kuhusu power hakikisha shirikiana na fundi hasa wanaofahamu sound system ya Mziki wa gari hutojutia
 
Nunua spika utakalo mm nashauli tafuta spika ya watts 400 RMS yenye p. M. P O Yan max watts 1400 ya NCHI 12 Yani ukubwa, Dukani zipo za pioneer, JBL, kwa Bongo japo zipo kampuni nyingi Ila kwa Sasa hizo ndio zipo sokoni kwa Bongo , nunua hasa pioneer , Kisha tafuta booster itakayo drive...
Receiver yangu tayari ina port ya powered subwoofer moja ya rangi nyeusi.

ina maana tayari ni mahususi kwa low frequency.

ni Av receiver ya channel saba yaani 7.1
 
but nataka zile za moja kwa moja zenye Amplifier ndani yyani nikifika me ni kuunga tu na kula mdundo.
 
Receiver yangu tayari ina port ya powered subwoofer moja ya rangi nyeusi.
ina maana tayari ni mahususi kwa low frequency.
ni Av receiver ya channel saba yaani 7.1
Hiyo Ni nzuri tu kwa kuunganisha Active Subwoofer Yani Ile inbuilt subwoofer(spika yenye booster yake ktk box) Ila Kama unaunga Passive Subwoofer itategemea Amp yako ni mono au ni 4channel.

Nb. Peruzi google andika how to connect car Amp to the receiver , utapata ufafanuzi mzuri
 
Hiyo Ni nzuri tu kwa kuunganisha Active Subwoofer Yani Ile inbuilt subwoofer(spika yenye booster yake ktk box) Ila Kama unaunga Passive Subwoofer itategemea Amp yako ni mono au ni 4channel.
Nb. Peruzi google andika how to connect car Amp to the receiver , utapata ufafanuzi mzuri
yaah ni hivyo.
ni pin ndogo ya rca.

hata sasa nimeunga na subwoofer yangu ya zamani ya mchina. but hailet matokeo mazuri sana. kuna muungurumo flani usioeleweka umekuja kutokea na unaongezeka siku hadi siku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom