Tenga la kuku ndani ya mabasi ya mwendo kasi

sirjohn

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
767
677
Naona bado tunahitaji kuwaleta wazungu kutufundisha ustaraabu.

Hivi haya mabasi ya mwendo kasi watumishi wake wana uelewa gani mpka waruhusu kuku kuingizwa ndani ya gari.

au tunataka kila kitu magufuli atwambie!

IMG-20160609-WA0004.jpg
 
Wakati ule uvutaji wa sigara unaruhusiwa kwenye mabasi, nilipanda basi Mnazi Mmoja ninakwenda kwetu Muheza, kando yangu amekaa kaka yangu wa kisambaa akawasha sigara, moyo ukaanza kuchefuka, nilitamani kutapika, nikamwambia si ungeshuka wakati ule basi limesimama watu wachimbe dawa ukavuta sigara yako kwa raha, akanijibu shea wewe. Wote tulikuwa abiria na tumelipa nauli, nilifunga mdomo.
 
Dawa ni kuweka mabandiko ya tahadhari kwa abiria. Kisha kuahinisha aina ya makosa na faini yake.
Baada ya hapo kilakitu kitakua kasi tu, kama sio kazi tu.

Asante
 
Una point ila uliposema wazungu watufundishe ustarabu nikatambua nawe ni wale wale mabigirwa wa fikra mgando. mzungu ana ustarabu gani wewe zuzu?

Afadhali ya hilo tenga la kuku...kuna siku na mimi nilijidai na basi la mwendo kasi kutoka Kisutu hadi Ubungo, lilikuwa ni la Kivukoni Kimara...Duh, nilitaka kuteremka Magomeni yaani lilikuwa lina harufu ya samaki wa feri...watu wamechukua matenga/maboksi ya samaki...Duh, aisee sisi waafrika ni shida...
 
Una point ila uliposema wazungu watufundishe ustarabu nikatambua nawe ni wale wale mabigirwa wa fikra mgando. mzungu ana ustarabu gani wewe zuzu?
Unaanza matusi sasa. Jibu hoja acha ad hominen arguments. Kwanza umetukana inabidi sheria ya mtandao ikufunge!
 
Back
Top Bottom