TENDWA Hatukuelewi

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,066
Hivi karibuni msajili wa vyama vya siasa amekuwa mstari wa mbele kuonyeshwa kutokuridhishwa na baadhi ya vyama kuwafukuza viongozi wake.

Hatumuelewi Tendwa kuwa ni kweli anatetea kukua kwa demokrasia au anaionea huruma serikali kwa gharama za chaguzi ndogo.
Ikiwa anataetea kukua kwa demokrasia angeanza kwa kuilaumu serikali kwa kutumia hila kuzuia mgombea binafsi ingawa tayari ilishabwagwa mahakamani.

Ikiwa anatetea serikali kuhusu gharama ingekuwa bora kuishauri serikali kwa kutumiwa na chama tawala kuacha kupandikiza watu kwenye vyama vya upinzani kwani hii ni hatari.
Kwenye vyama vya uoinzani linapatikana jukwaa la kujadili siasa mbadala na ikiwa serikali na chama tawala watalivunja jukwaa hili ni wazi kitakachofuatia ni vurugu.

Ili vyama vya upinzani vikue ni lazima ijengwe nidhamu ya hali ya juu na ufuataji wa taratibu na kanuni uwe wa kiwango cha juu na yoyote anayekwenda kinyume hatua kali kuchukuliwa ni sahihi.
Alitimuliwa Rais wa Zanzibar itakuwa wabunge ambao wanaonyesha dhahiri kuvuruga upinzani?

John Tendwa tumia muda wako kuishauri serikali na acha vyama vya upinzani viendelee na "storming" kabla ya "normalization na performing"
 
Ingawa napinga Kafulila na Hamad kufukuzwa lakini hoja yako ina ukweli fulani.
 
Anaiunga mkono Chadema.Chama cha ukombozi.Mbona hata watumishi wa wakoloni walimuunga mkono Nyerere wakati wa kupigania ukombozi? Sasa unashangaa nini? Nadhani nimekujibu swali lako.Una swali la nyongeza?
 
wewe unaichukulia kidini zaidi..yaani unayoongea kama gazeti la Al NUUR......I am sure you are more than that...
 
cdm haitetewi na mtu mmoja wala kiongozi wa taasisi yoyote bali wakulima na wafanyakazi wanyonge wa nchi hii.
 
Tendwa kwa kweli mimi simwelewi,anajichanganya sana.
Sisi tunaulalamikia huo utaratibu siku nyingi sasa anaona unaitia serikali hasara anaanza kwa kuviona vyama vya upinzani ndo vinakosea.

Huyu malaria sugu nae ni wakudharau kama huyo tendwa wake.
 
Kwa kweli Tendwa hajui analolifanya, kama hoja yake imeegemea kwenye gharama za uchaguzi na kunyimwa kwa haki za kuwakilishwa kwa wananchi hata Rostam alijiuzulu baada ya kuona anataka kufukuzwa ccm. kwa mtazamo wangu naona jambo hili linafanana kwa pande zote na hili la Hamadi Rashidi.
 
Tujitahidi Watanzania kuweka SIASA na DINI tofauti tusije tukafika NIGERIA.
Kwenye CUF kuna WAKRISTU na WAISLAM na kwenye CHADEMA kuna WAISLAM na WAKRISTU.Tuache kuchanganya DINI na SIASA.
 
sheria ni msumeno na haki ya kumfukuza mtu uanachama inafanywa na chama husika kama serikali inaona kuna tatizo basi sheria nyingine itungwe lakini sio kutoa comment kinzani kwa case mbili zinazofanana!
 
Hivi Mr Nice alipoimba ule wimbo wa KIKULAAACHO KUMBE KIKO NGUONI MWAKOOO, RAFIKI YAKOOO KUMBE NDIYE ADUI YAKOOOO...
 
1. Hii sheria ya kupoteza ubunge pindi unapofukuzwa chama wameitunga hao hao akina CCM (Tendwa na Werema pia ni CCM pure, na part of the machine)

2. Hii sheria ilishawahi kutumika kumuondoa Mrema bungeni alifukuzwa/ alipohama CCM. Mbona wakati huo hakukuwa na ulalamishi kiasi hiki. Hivi leo CCM ikimfukuza uanachama mbunge, Tendwa na Werema watatoka kuishambulia kiasi hiki?

3. Hii sheria ipo kwa sababu walioitunga walijua kuna siku itatumika. Walipoitunga na kuipitisha walikuwa wanajua hali yetu ya uchumi. Leo kwa nini wanalaumu vyama vya siasa kwa kufuata sheria walioitunga hao wenyewe?

4. Werema anasema kuwa CUF imevunja katiba kwa kutofuata maagizo ya mahakama. Jamani mimi siyo mwanasheria, lakini sidhani kama mtu akishindwa kufuata maagizo ya mahakama anakuwa amevunja katiba. Mara nyingi unasikiaga kuwa mtu kama huyo anakuwa AMEDHARAU MAHAKAMA, siyo KUVUNJA KATIBA.

Vyote kwa vyote, nahisi kuwa hawa waheshimiwa wawili wamelewa madaraka kupindukia.

Halafu hii gharama ya uchaguzi mdogo kuwa Billion 19 Tshs inabidi ufanyiwe uchunguzi. Inatumika kwa ajili ya kitu gani? Naona kama vile ni nyingi mno.

2101 kulikuwa kuna viti kama 300. Jee ina maana uchaguzi uligharimu serikali karibia Trillion 6? Budget ya serikali ya 2012 ni ngapi vile?
 
Hivi karibuni msajili wa vyama vya siasa amekuwa mstari wa mbele kuonyeshwa kutokuridhishwa na baadhi ya vyama kuwafukuza viongozi wake.

Hatumuelewi Tendwa kuwa ni kweli anatetea kukua kwa demokrasia au anaionea huruma serikali kwa gharama za chaguzi ndogo.
Ikiwa anataetea kukua kwa demokrasia angeanza kwa kuilaumu serikali kwa kutumia hila kuzuia mgombea binafsi ingawa tayari ilishabwagwa mahakamani.

Ikiwa anatetea serikali kuhusu gharama ingekuwa bora kuishauri serikali kwa kutumiwa na chama tawala kuacha kupandikiza watu kwenye vyama vya upinzani kwani hii ni hatari.
Kwenye vyama vya uoinzani linapatikana jukwaa la kujadili siasa mbadala na ikiwa serikali na chama tawala watalivunja jukwaa hili ni wazi kitakachofuatia ni vurugu.

Ili vyama vya upinzani vikue ni lazima ijengwe nidhamu ya hali ya juu na ufuataji wa taratibu na kanuni uwe wa kiwango cha juu na yoyote anayekwenda kinyume hatua kali kuchukuliwa ni sahihi.
Alitimuliwa Rais wa Zanzibar itakuwa wabunge ambao wanaonyesha dhahiri kuvuruga upinzani?

John Tendwa tumia muda wako kuishauri serikali na acha vyama vya upinzani viendelee na "storming" kabla ya "normalization na performing"

Hiki ndicho nilichoandika,Uislamu na Ukirsto umeingiaje?
Kwani nini tunapoteza mwelekeo na vipi udini unashika kasi kiasi hiki?
 
kama makanisa yalikipgia sana kelele cuf, lkn yapo kimya kuhusu cdm. Jee na yeye anatawambiaje kuhusu ari mpya, nguvu mpya alionayo kwa sasa kutka kumsaidia hr?

Kwa nini udini jamani,tutaliangamiza taifa kwa mambo ya kijinga
 
Maalim seif alisema wazi. Wamemfukuza Hamad kutokana na kutoa siri za Cuf kwa Chadema.alizataja baadhi ya siri pale Manzese tendwa hataki kusikia, anaziba masukio.Isitoshe chadema iliwatimua madiwani wake wa 5 huko Arusha. Tendwa alipohojiwa na chombo kimoja cha habari Cha kimataifa. tendwa alidai viongozi wakuu wa Chadema wametumia Katiba yake na hawana makosa , na yeye kajidai kama mlezi hawezi kuingilia swala hili huku wananchi waliowachagua ni watz, wanaotumia katiba hii ya watz. chadema imeasajiliwa kwa katiba hii wanayotumia CUF.hivi sasa chadema inafanya kila njia kukifanya cuf ipoteze dira tzbara. Ilianzia bungeni kwa kuita CCM B na hatimae hadi kwenye vyombo vya habari. chadema imefanya urafiki na CDU. hii ni kinyume na katibaya TZ ni wazi swala hili ni kinyume Cha Sheria za nchi. tendwa anaglikuwa makini na Mkweli alingalitolea ufafanuzi. hapa anangoja Cuf ijiunge na al Nahda Cha TUNISIA kifungue katiba na kionyeshe waz.

Naunga mkono maneno yako MS.

Kwa Hakika Msajili wa Vyama Tz ni mnafiki mkubwa. Kumbuka kuwa katiba, kaanuun za vyama vyote vilivyosajiliwa Tz yeye anavyo. Na vile vile kwa mujibu wa katiba yeye ni mlezi wa vyama vyote ana nafasi ya kuwaita viongozi wa chama chochote kwa ushauri. Na kwa mantiki hiyo alikuwa na nafasi kuzungumza na vyama hivyo kabla maamuzi kutolewa.

nafikiri Tendwa amechanganyikiwa na kukumbuka jamvi wakti kumekucha. Mbona hakusema lolote wakti Rostam alipoachia ubunge. au hakukuwa na gharama hapo. Au ana ajenda gani na Hamad Raashid?
Nafikiri kuna kitu ambacho Hamad Rashid alikuwa anafanya kwao kwa kuihujumu CUF na kwa kuwa ameshitukiwa na kufukuzwa sasa wanahaha kutafuta watampata nani.

Poleni sana
 
Back
Top Bottom