Tendwa azuia maandamano CUF kwenye ofisi yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa azuia maandamano CUF kwenye ofisi yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 30, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  WAKATI Chama cha Wananchi (CUF) kimepanga kufanya maandamano makubwa kuanzia Buguruni Sheli hadi kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, msajili huyo amepiga marufuku maandamano kufika katika maeneo ya ofisi hizo.

  Taarifa za kupingana kwa taasisi hizo mbili zilitolewa jana kwa nyakati tofaiti na kila moja ikitoa sababu zake za kuchukua hatua husika.

  Mapema asubuhi, Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba alisema msimamo wao ni kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Lewis Makame ajiuzulu kutokana na kushindwa kuzuia na kuhakikisha uwajibikaji na uwazi kwenye taratibu za uchaguzi na kutaka tume hiyo ivunjwe na kuweka watu safi wenye kuijua demokrasia.

  "Tutaendelea na maandamano hayo bila kuchoka na yatafanyika nchi nzima kwani tume imeshindwa kuunda asasi za kuhakikisha usalama na uwazi katika vipindi kadhaa vya uchaguzi hapa nchini." alisema Prof. Lipumba.

  lakini ilipofika mchana, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Bw. John Tendwa naye aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kueleza kuwa yupo tayari kupokea ujumbe wao katika maandamano yanayofanyika leo lakini wapange maeneo tofauti na viwanja vya eneo la ofisi yake.

  Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa iko katika Barabara ya Mirambo, ikiwa takriban mita 300 kutoka kwenye geti la Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete, Ofisi ndogo ya Bunge na maeneo mengine nyeti ya serikali.

  "Nimekubali kuwapokea lakini niliwataarifu kuwa eneo letu ni dogo na hapa tupo karibu na ofisi mbalimbali ikiwa ni Benk Kuu, Ofisi ndogo ya bunge, Shule ya Msingi, Wizara ya Fedha pamoja na Magereza, tunahitaji kulinda usalama," alisema Bw. Tendwa.

  Alisema kuwa katika maandamano hayo si kila mmoja ana nia ya kufikisha ujumbe kama ulivyokusudiwa bali miongoni mwao wapo watu wanaoweza kufanya vurugu na kuvunja amani iliyopo.

  "Katika msafara wa mamba hata kenge wamo, sisi tunaangalia usalama, pia kesho ni siku ya kazi, niliwashauri na pia ninaweka msisitizo kuwa tupo tayari kuwapokea mahali popote," alisema Bw. Tendwa

  Alifafanua kwamba baada ya kupata taarifa kuwa wanataka kuandamana, aliamua kuwapa taarifa kuwa yupo tayari kukutana katika maeneo mbalimbali ya wazi ikiwa ni pamoja na eneo la Mnazi Mmoja, Kidongo chekundu pamoja na Jangwani lakini hakupata majibu yoyote.

  "Tatizo la CUF ni kuwa namba wanazoziweka katika paper (nakala za machapisho) yao ukizipiga huwapati, mpaka umpigie mtu binafsi," alisema.

  Wakati hayo yakiendelea, CUF kwa upande wake ilikuwa ikiendelea na maandalizi ya maandamano na Profesa Lipumba alipoulizwa msimamo wa Tendwa alisema hakuwa na taarifa nao lakini kijana wake alikuwa polisi akizungumzia suala hilo.


  Imeandikwa na Prosper Mosha, Yusuph Katimba na Husna Ridhiwan
   
 2. s

  sanjingu Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maandamano ni haki ya kikatiba au ya kiraia?
  Kimsingi maandamani yanayofanyika ni kama kupoteza wakati.
  Kwani unaweza kufaanya maandamano na madai yote yasihugulikiwe zaidi
  ya kupuuzwa tu. Ninacho shauri kwamba badala ya kushugulikia mandamano
  tumwambie rais aunde taasisi ya uchaguzi badala ya tume.
  Kwani tume inafanya kazi ya rais na sio ya taifa.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,581
  Likes Received: 18,562
  Trophy Points: 280
  Jana usiku Tendwa alitangaza kwenye habari kuwa CUF wametimiza masharti, hawatakuja mjini na wamepata kibali cha polisi kuandamana, hivyo atayapokea hayo maandamano.Kama kuna mwenye update ya maandamano hayo atuletee.By the way, hawa CUF kumpelekea Msajili kilio cha chao dhidi ya NEC ni kama kesi ya nyani kumpelekea ngedere, the right forum ni kumpelekea mkulu mwenyewe au kuipeleka NEC mahakamani.
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwani wewe hujui kubwa Tendwa naye ni agenti wa CCM, maana kumbuka yule msajiri aliyepita alitaka kugombea ubunge kupitia CCM
   
 5. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Pia na mabadiliko ya Katiba.

  Hivi kwanini vyama vingine havikushiriki?? kama ni CUF pekee hakuna uzito.

  Juzi walitangaza Tanzania ina vyama vya siasa 18. Mimi nafahamu 5 (CCM, CHADEMA, NCCR, CUF, TLP) hivi vingine ni vipi?
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi ushauri wangu ni Kwamba vyama makini kama CUF na CHADEMA ni kugoma kwenda kwenye uchaguzi mkuu mwakani bila ya katiba huru na tume huru ya uchaguzi pia
   
 7. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sheria ya uchaguzi inasemaje? Ikiwa watagoma uchaguzi hautafanyika? Au hili litasaidia jumuiya za kimataifa kuingilia kati? By the way si unasikia kauli za jumuiya za kimataifa kuhusu hali ya kisiasa Pemba? Wanaangalia tu kwa mbali hawawezi kuingilia uhuru wa nchi...
   
 8. N

  Nanu JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Uzuri wa maandamano ni kupata attention ya donors na hapo JK hawezi kusema mambo yako shwari akiulizwa huko nje maana watakuwa na data ambazo sio za kificho na watasema zimepatikana through maandamano. Maandamano kwa ujumla zinatuma ujumbe mzito sana na kwa haraka zaidi na utafika mbali zaidi.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  acha waandamane bwana nchi lenyewe limeshaoza hili
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nilipenda kama kuandamana mpaka asubuhi na kuona kuwa wanataka mabadiliko ya katiba Tanzania
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  ndiomaana tunasema cuf ni kama taasisi ya dini..................tumewachoka kwa kuandamana............wanawapotezea watz muda badala ya kuwaacha wafanye shughuli za kujipatia kipato muda mwingi wanashawishiwa kuelekea kwenye maandamano......
   
 12. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Wewe na nani mnasema?...

  Ni haki yaoo kuandamana...huyo anayeshawishika kuwafuata nafikiri ana jambo la kumpeleka kwenye maandamano. Mfano mmoja tu wa wazi, Imetangazwa kuanzia tarehe 4 - 10 October 2009 ndio muda uliotolewa wa kujiandikisha kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa. Umejiuliza kama utakuwa safarini inakuwaje? Hii ina maana umenyimwa haki yako ya kikatiba ya kushiriki katika ucahguzi huo. Is this fair?
   
 13. K

  Kyaruzi Member

  #13
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Tendwa ni wa kupuuzwa tu, maandamano ( muradi yawe ya amani ) ni haki ya vyama tatizo lake yeye nini?
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hongera CUF ,huu ndio mwanzo au hatua ya kwanza kuelekea madai makuu ya Katiba ,ni lazima wananchi washirikishwe kikamilifu katika madai ya kuondoa mazindiko ya Sultani CCM , aidha si lazima Chama fulani ila wananchi wanaweza kushiriki chini ya Chama fulani kwa maana hawawezi kuzuka na kufanya maandamano kama nzige ,ni lazima pawepo na wigo au mwega utakaoweza kuyataarisha na kusimika msimamo uliowakilishwa kutoka kwa wananchi mbali mbali ,hata kama ikiwezekana kukusanya signatures za wananchi wanaounga mkono ,mapinduzi ya kisiasa Tanzania kwa kuwezesha tume huru ya uchaguzi na mabadiliko makubwa ya katiba chini ya siasa za vyama vingi ,Katiba zilizopo zinailinda CCM na kuipa udhibiti wa vyombo vyote vya dola.
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Ukiweza kujiuliza kwa kuandika hapa kwamba kwa nini Vyama vingine basi nami ni haki ya kila mtanzania kupata haki hizo maana kweney vyama walioko si wanyama ni watanzania , huna budi nawe kujiuliza ujmechukua hatua gani uona haki hii inatendeka na si kuwa nyooshea wengine vidole . Hili ndilo kola la wengi wetu hapa JF kujifanya Nchi ni wana TLP , Chadema etc . Iga mfano wa mwanakijiji na mimi nina kueleza haya . Usinyooshe vidole nawe una haki ya kwenda Mahakamani kutaka Katiba huru .
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kila mtu anayo haki ya kuandamana na kuona kuwa kila ambacho yeye anataka anatimiziwa, kuna mtego mkubwa sana katika uchaguzi Tanzania kwa jambo hili ndio muhimu sana katika Tanzania
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...hivi Raisi ni nani afanye kila kitu,kwanza wanaotakiwa kufanya marekebisho ya kuunda au kuvunja tume ya uchaguzi ni Bunge la Jamhuri sio Raisi,kumpa au kufikiri Raisi anatakiwa kufanya kila kitu ni udikteta,ongea na mbunge wako au wabunge unaowajua waambie waandike muswada wa hiyo sheria unayotaka ikajadiliwe bungeni,kwa wenzetu kuna watu wanaitwa lobbyst na think tanks nyingi tuu hao ni kuweka pressure na kuwaambia wawakilishi wanataka mabadiliko gani katika sheria na wengine wanasaidia kuandika bill nzima inayopelekwa bungeni ingawaje hawasemi,tunahitaji watu wanaoelewa wa kuwapa pressure wabunge underground ili mabadiliko yafanyike ingawaje maandama nayo yanasaidia kuweka issue kwenye media lakini mengi hayana substance.
   
 18. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kwani CCM wao maandamano yao ufanywa saa ngapi!!!!!!?????? Wewe unasema pamoja na nani au unamsemea nani kwamba CUF ni taasisi ya dini!!!! Toa mawazo yako usiwasemehe wengine mkuu!!!!

  Tiba
   
 19. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jana nimeona kwenye vyombo vya habari na mzee tendwa atayafanyia kazi yale yake na ujumbe atawafikishia wahuiska


  wamesisitiza cuf katiba mpya na tume huru hayo ndio mambo mawili makuu yaliomo kwenye maandamano yao
   
 20. K

  Koba JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Nafikiri CUF wanakosea sana na wanafanya mambo kama watu wasioelewa,huyo tendwa hana uwezo wowote wa kubadilisha chochote na wala hahusiki na sheria zilizopo,yeye kawekwa tuu kama mfanyakazi na kufuata sheria zilizopo ambazo hana uwezo wa kuzibadilisha,haya maandamano/pressure inatakiwa kwa watunga sheria sio huyu Tendwa.
   
Loading...