Tendwa awatisha kakobe, sheikh yahya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa awatisha kakobe, sheikh yahya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by matambo, Oct 3, 2010.

 1. m

  matambo JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tendwa awaonya Kakobe, Sheikh Yahya
  • Ajiandaa kutunga sheria kali dhidi ya wanajimu

  na Danson Kaijage, Dodoma


  [​IMG]
  MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amevunja ukimya na kuwajia juu baadhi ya viongozi na watabiri wa nyota ambao wamekuwa wakiwatishia wapiga kura, kwa kuwalisha mafundisho yasiyo sahihi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu suala la wagombea kurudisha fomu za gharama ya uchaguzi kwa wakati, Tendwa alisema watu hao wamekuwa wakitaka kuhatarisha usalama.
  Aliwataja viongozi hao kuwa ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship na mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, kuwa ni watu hatari, ambao wanaweza kuleta fujo ndani ya nchi kutokana na mafundisho yao pamoja na utabiri usio kuwa na msingi wowote.
  Alisema kitendo cha Askofu Kakobe kutoa elimu ya uraia kanisani kwake, kinaonyesha wazi amejiingiza katika kampeni za kisiasa na kusahau kazi yake ya kuwahudumia watu wake neno la kiroho.
  Alisema viongozi wa dini wanatakiwa kutoa elimu ya kiroho ambayo itawapa mwanga waumini wao, ili waepukane na maovu na si kugeuza madhabahu kuwa uwanja wa siasa.
  Alisema kitendo cha Sheikh Yahya kutoa utabiri wake kupitia kipindi chake cha ‘nyota’ kinachoonyeshwa katika moja ya vituo vya televisheni jijini Dar es Salaam, kinaonyesha wazi kukipigia kampeni moja ya chama kati ya vyama viwili vyenye nguvu, jambo ambalo ni mwelekeo wa uvunjifu wa amani.
  Alisema kutokana na tabia ambazo zinaonekana kukua kati ya makundi ya dini na siasa, kuna kila sababu ya kuangalia upya sheria ambayo itaweza kudhibiti viongozi wa dini kutojiingiza katika siasa ama kuwadhibiti watu kama Sheikh Yahya, ili usomaji wa nyota uwe kwa faida yake na si kuwachanganya wananchi.
  Akionekana kuwa mkali, Tendwa aliponda baadhi ya taasisi ambazo zimekuwa zikitoa taarifa za mgombea gani anaongoza kupendwa.
  Bila kutaja taasisi hizo, hivi karibu Kampuni ya utafiti ya Synovet ilitoa matokeo ambayo yanaonyesha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete, anaongoza kwa kupendwa.
  “Nina shangazwa na taasisi zinazoendesha kura za maoni juu ya mwenendo mzima wa hali ya kisiasa na kutoa mwelekeo wa ushindi katika vyama vya… huu ni uchochezi kwa wananchi,” alisema Tendwa.
  Akizungumzia urudishaji wa fomu za gharama za uchaguzi, alisema wagombea wote wanatakiwa kurudisha fomu hizo ili zifanyiwe uhakiki.
  Alisema mgombea ambaye atabainika hajarudisha fomu hiyo ataenguliwa katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kupewa adhabu ya kutogombea nafasi yoyote katika uchaguzi wa mwaka 2015. Alisema pamoja na hilo, baada ya uchaguzi wagombea watapewa siku 60 ili kupeleka vielelezo vya mapato na matumizi kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili kubaini iwapo gharama zilizowasilishwa zimetumika kama ilivyokusudiwa. Alisema iwapo sheria hiyo itaonekana imekiukwa, kwa kuonyesha mgombea ametumia pesa nyingi zaidi, atalazimika kutoa maelezo na iwapo maelezo yake hayatakubaliwa, atafutiwa matokeo.

  source TANZANIA DAIMA 03/10/2010
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tendwa tendwa vipi tena mzee wangu. Nani amekwambia viongozi wa dini hawaruhusiwi kuelimisha waumini kuhusu siasa? Usimwonee kakobe na wala usimweke fungu moja na "mtabiri" yahaya. Mbona hujawahi kumkemea pengo au unamwogopa? Kila raia ana uhuru wa kuelemisha watu khs uchaguzi km alivyofanya kakobe
   
 3. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nani kakwambia viongozi wa dini hawana wajibu wa kutoa elimu ya uraia,mbona JK alipoambiwa kuwa ni chaguo la Mungu hukusema lolote?Au kwa sababu kilicho semwa ni ukweli mtupu?Ujumbe umefika na mwenye masikio amesikia.
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  shehe yahaya toka lini akwa kiongozi wa dini
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hehehe TENDWA.
  nakuona unavyojigeuza kitandani hapo huku ukiota ndoto zako kama kawa.
  AMKA
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  msumari wa Kakobe naona umewachoma kotekote,
  Askofu Kilaini alisema JK ni chaguo la MUngu Tendwa akawa kimya, Shehe yahaya ameongea mengi lakini kimya, hili la Kakobe ndio Shehe Yahaya kaingizwa ili ionekanwe Tendwa anawapiga mkwara wote, cha muhimu ni kakobe kurudi tena na kujibu hoja zote zilizotolewa na hayo mapepo
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tendwa acha kutisha Kakobe maana mbona uliwakuwa wapi pale Yahaya aliposema kuwa Jk ni chaguo la Mungu?? Mbona hakutoka na kusema mamboi kama haya. kakobe Sema ukweli alisema ukweli kabisa
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tendwa hujui dini wala kazi ya viongozi wa dini. Dini hutakiwa kukidhi mahitaji (maisha bora) ya kiroho na ya kimwili. Huwezi kuindoa siasa kwenye majumba ya ibaada.
   
 10. m

  matambo JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Binafsi namuona ni mnafiki, laiti labda viongozi wa dini wangemsifia jk, lazima angekaa kimya, after all kakobe hakumpigia debe kiongozi yeyote rather alikuwa anawasisitizia waumini wake umuhimu wa kupiga kura kitu ambacho nafikiri ni recommendable,

  tendwa alipaswa amsifu kwa hilo
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu aliandika hapa kama Tendwa Kichwani zinamtosha sasa naweza kusema waziwazi kwamba huyu jamaa hazimtoshi, maana alikuwa wapi wakaati Yahaya anasema kwamba wataompinga JK watakufa?

  Huyu Jamaa Hazimtoshi
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tendwa kwa usanii simuwezi,mzee kijana huyu sound nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Labla tuangalie kwa undani zaidi, Kazi ya Tendwa ni nini? Ofisi yake inatakiwa kushughulikia nini? Usajili wa vyama na kuangalia mwenendo wa vyama kutokana na masharti ya usajili? watu kuongea maneno yanayohusiana na vyama, wagombeana siasa.

  Anajua nani ni mwanadini na dini inaishia wapi kabla ya kuwa siasa? Tukijua haya tunaweza kum-judge Tendwa. Otherwise inabidi aseme ni kwanini alikuwa kimya Kilaini aliposema JK chaguo la Mungu, na kwanini anapinga ZK kusema kwenye siasa hakuna chaguo la Mungu.
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Tatizo kubwa katika kipindi hiki ni kila mtu kujifanya Msanii wa kulamba viatu vya mheshimiwa. Muda mrefu tu Sheikh Mnajibu alikuwa anabwabwaja maneno ambayo yangeweza kuhatarisha Amani ya Taifa, Huyu bwana Tendwa alikuwa amekaa kimya akiogopa kusema kitu maana anajua Sheikh yuko connected na ngazi za juu na ndio maana ziko kimya hata pale anapodai kuwa kuna mgombea uraisi atapoteza maisha.
  Amemsikia Askofu Kakobe akiongea na waumini wake akiwapa darasa la kufahamu haki zao, Tendwa anarukia treni kwa mbele na kujifanya kutoka onyo kwa wote wawili!!
  Ulikuwa wapi Sheikh alipokuwa anabwabwaja?
  Acheni Unafiki.
  Siku Zenu Zinahesabiwa.
   
 15. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mi binafsi nimeshindwa kumwelewa huwa mzee mwenye Pengo (mwanya), nilichoshindwa kukielewa ni mahusiano kati ya mahubiri ya kakobe kuhusu uraia na uvunjifu wa amami! Je ni kweli maneno ya kakobe yanavunja amani? Nafikiri Tendwa ndo anavunja amani.

  Kwa upande wa Mnajimu ni kweli maneno yake yanavunja amani kwa kuwatisha watu. Je Mwanya ulikuwa wapi kumkemea? Hii ndo inazihilisha kuwa huyu naye ni mramba viatu vya JK.
   
 16. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,441
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Bw Tendwa sasa hivi huna la kufanya kwani umesema itungwe sheria ya kudhibiti vitendo vya kuwatisha au kuwashurtisha wapiga kura,ina maana kwa sasa unabweka lakini huna meno ya kung'ata,unapojikuta katika hali kama hiyo ukashindwa kufanya yale uliotarajia unakuwa muungwana unajiuzulu mapema kweupe.
   
 17. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  tendwa wewe unataka kuvuruga uchaguzi, huna lolote
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni Tendwa ndio Tatizo na sio Kakobe
   
 19. W

  We know next JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa hakika mfa maji hutumia njia zozote kujikwamua asizame. Watu ni wale wale, na wanajitahidi kusaidiana, nacho waasa kama wanapitia mtandao huu wa JF basi wajiangalie sana Historia isije wahukumu. Kwa hakika watasimama kizimbani, kwa hiyo ni vyema wakaelewa hilo na kuepuka hayo, kila mtu kwa nafasi yake.
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Tendwa Elimu ya urai kuhusu swala zima la upigaji kura hujalitimiliza nchini sasa mie sijaona kakobe kakosea wapi usipende kusoma habari ungelienda na kuangalia marudio ya yale mahubiri na ndio maana yakarudiwa tena baaada ya waandishi kuandika habari tofauti.

  mara ngapi niwaaambie nyie viongozi kabla ya kuongea jambo lipime katika nyakati hizi usilopoke watu wakuone kwenye runinga na magazeti asubuhi jamani khaaa
   
Loading...