Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA

Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA

Ndio maan hali ya nchi ni ovyo, kwa kuwa na watu kama hawa katika sehemu nyingi za serikali zilizo nyeti.
 
Kazi inayofanywa na CHADEMA katika M4C Si ya kubezwa hata kidogo. Mzee Tendwa hajui majukumu yake. Anadhani kazi yake ni kukibeba CCM na kuwabeza wapinzani. KAULI ZAKE za kila mara kuhusu kazi za CHADEMA zimekuwa zikimsuta mwenyewe. Hana hoja na vyombo vya habari vijiulize pia kama kweli anayosimamia huyu babu yanafanana na kazi yake au?!!
 
tendwa u have to know that all snitches wana kufa kwa aibu saana its pride and shame
 
Msimlaumu bure jamani, Tendwa ni Mlezi wa CCM, Lazima apambane pale ambapo chama chake kitatishiwa madaraka(maslahi)
 
Tusubiri katiba mpya (kama itaboreshwa ipasavyo), aombe nafasi ya kukalia kiti anachokalia sasa.
GOD bless TZ.
 
Wanipe mimi hiyo kazi kwan vijana tumekufa ndio wang'ang'anie hawa wazee wasiojiweza waendelee kuongoza akati wameshavurugwa?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Inawezekana alikua safari hata saga la Gas Mtwara halijui, wengine tunafahamu ule uamsho wa wana Mtwara ni matokeo ya M4C, kwa wale mnaomfahamu mwambie wana Mtwara wameelewa somo!
 
Hv mzee huyu anasumbuliwa na shetani gani kichwani mwake????!!!! Kila siku kutishia cdm,mara nitakifuta. Sasa mzee tendwa jaribu moto wa kufuta cdm tuone kama hautamaliziwa nyumbani kwako na wanao kwani wanatambua cdm kama tumaini jipya la watz,
 
Kwao ndo KPI, Parfomance ya mtu CCM inapimwa kwa Kuitusi au Kuikejeli CDM.
Si unaona akina Jerry, Mwigulu etc etc
 
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.

Yeye kama mlezi wa vyama vya siasa kwa nini asingetoa ushauri wa bure kwa CDM kuhusu operations hizo. Kwanza yeye kinamuuma nini hata kama wamekurupuka?? Ajira yake imeshaisha, hayo maoni katoa kama Tendwa.

BTW: CDM walishasema hawako tayari kushirikiana na Tendwa bali watafuata sheria za nchi..period. Hapo alienda kuuza jino lake tu.
 
Kwa kuwa tendwa huwa anadundwa makofi na mkewe atakuwaje na uwezo wa matumizi mazuri ya akili?
 
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.

Mkuu wazee kama hawa ubongo wake ume atrophy kwanza aache unafiki mlezi gani wa vyama anakadi ya magamba?
 
Back
Top Bottom