Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA

Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA

Kwa nini mnapenda kutumia vibaya neno MZEE??(hilo neno lina heshima yake na lina maana yake...) badala ya mzee kama mngetumia TAAHIRA au CHIZI hamuoni kama ujumbe ungekuwa na maana mliyokusudia?? Mimi kama wengi wenu ninaamini huyo zoba ni TAAHIRA na NI CHIZI...call a spade a spade!!
 
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.

Lengo lake nikudhoofisha juhudi za CHADEMA. Hebu hizo kanda zianze kufanya kazi haraka aone moto wake
 
Kwa hali ya kawaida linakuwa jambo la kushangaza sana anayeitwa msajili wa vyama vya siasa kutoa maoni kama yale kwa chama cha siasa kwa nafasi aliyonayo.
Amewekwa pale ili afanye anayoyafanya sasa. Ni kada wa CCM huyo!!!
 
Refarii anachezesha gemu wakati huohuo anaumizwa na kandanda safi linalochezwa na timu moja dhidi ya nyingine.
 
Refarii anachezesha gemu wakati huohuo anaumizwa na kandanda safi linalochezwa na timu moja dhidi ya nyingine.

hahaha! Tendwa anachezesha mechi ya Cdm dhidi ya ccm, mpira umemgonga muamuzi na kuelekea langoni mwa Cdm, bahati nzuri mlinda mlango wa Cdm (Mbowe) amefanya kazi ya ziada na kuugonga umetoka nje ya uwanja, ni kona kuelekea lango la Cdm.................
 
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.



....

kwa kauli hiyo ana mgao wake pale Lumumba.
 
Namshangaa huyo mzee kwa kauliza kinafiki,mwanzo yeye na ccm wenzake walisema Cdm nichama cha msimu,leo motowake anauona unatishia kibarua chake 2016 eti anajifanya anawaonea huruma Cdm kuanza halakati mapema watachoka.Wakichoka inamhusu nini yeye? si ndio nafuu yake? ajiandae kufanya makabidhiano nyalaka zote awe nazo asije kusingizia eti panya walikula au zilinyeshewa na mvua
 
1 said:
icon1.png
Wanasiasa waache kuchochea Udini-Tendwa
"Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ameitaka serikali kukomesha uchochezi wa kidini ambao anaamini unachochewa na baadhi ya vyama vya siasa.

Akizungumza katika mkutano wa Baraza la vyama vya siasa Tendwa amesema uchochezi wa kidini ni hatari na kuonya vyama vyenye tabia hiyo kuacha mara moja.

Tendwa amekuwa mara kadhaa akitoa lugha ambazo hajazifanyia utafiti na kuonekana kama kituko mbele ya jamii."​



Kachanganyikiwa huyu ... hajui majukumu yake au aliambiwa ahakikishe anaangamiza upinzani sasa kashindwa anaanza kubwabwaja ...​
 
Back
Top Bottom