Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
VYAMA vya siasa nchini vitaendelea kufanya maandamano ya amani pale inapobidi kwa kuwa hatua hiyo inaruhusiwa kisheria na ni haki ya msingi ya kila mtu na chama chake katika kujitafutia haki.
Aidha, imeelezwa kuwa mpango wa kutunga sheria itakayodhibiti maandamano ya vyama vya siasa nchini unaodaiwa kutajwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) , Jaji Frederick Werema, ni kutaka kuvinyima vyama haki za msingi za kikatiba.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Msajili wa Vyama, John Tendwa, alipozungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi katika jimbo la Igunga na marejesho ya fomu za gharama za uchaguzi mkuu uliopita.
Labda kama AG hakueleweka au alitafsiriwa vibaya, sidhani kama anaweza akasema ataleta muswada wa sheria ya kudhibiti vyama vya siasa kufanya maandamano nchini, kwa kuwa hiyo ni haki ya kikatiba na yeye ni mwanasheria anayeifahamu Katiba, sijui, sikumsikia ninyi ndio mnanieleza katika swali lenu hapa.
Lakini kama hivyo ndivyo, basi itabidi abadilishe sheria nyingi sana, kwa sababu zipo kihalali na kwa malengo ya kujenga, endapo maandamano yanakuwa na nia nyingine hapo inawezekana kukawa na kasoro, lakini kuyadhibiti bila sababu kwa kuwa ni ya vyama vya siasa sidhani kama itakuwa sawa, ngoja tuone. Itakapotokea ndipo hapo tutajua, Msajili alisema.
Habari Leo