Tendwa ampinga Werema kubadili sheria ya maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa ampinga Werema kubadili sheria ya maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 4, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  VYAMA vya siasa nchini vitaendelea kufanya maandamano ya amani pale inapobidi kwa kuwa hatua hiyo inaruhusiwa kisheria na ni haki ya msingi ya kila mtu na chama chake katika kujitafutia haki.

  Aidha, imeelezwa kuwa mpango wa kutunga sheria itakayodhibiti maandamano ya vyama vya siasa nchini unaodaiwa kutajwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) , Jaji Frederick Werema, ni kutaka kuvinyima vyama haki za msingi za kikatiba.

  Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Msajili wa Vyama, John Tendwa, alipozungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi katika jimbo la Igunga na marejesho ya fomu za gharama za uchaguzi mkuu uliopita.

  “Labda kama AG hakueleweka au alitafsiriwa vibaya, sidhani kama anaweza akasema ataleta muswada wa sheria ya kudhibiti vyama vya siasa kufanya maandamano nchini, kwa kuwa hiyo ni haki ya kikatiba na yeye ni mwanasheria anayeifahamu Katiba, sijui, sikumsikia ninyi ndio mnanieleza katika swali lenu hapa.

  “Lakini kama hivyo ndivyo, basi itabidi abadilishe sheria nyingi sana, kwa sababu zipo kihalali na kwa malengo ya kujenga, endapo maandamano yanakuwa na nia nyingine hapo inawezekana kukawa na kasoro, lakini kuyadhibiti bila sababu kwa kuwa ni ya vyama vya siasa sidhani kama itakuwa sawa, ngoja tuone. Itakapotokea ndipo hapo tutajua,” Msajili alisema.

  Habari Leo
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na Tendwa, bila maandamano haki haitendeki
   
 3. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  Nakumbuka mgomo wa madaktari pale Muhimbili 2005.... Kama noma na iwe noma sikubali leo narevenge mimi.... Hadi mishahara ikaongezwa, big up maandamano na migomo.
   
 4. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sometimes Tendwa is brain!
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Saa mbovu (ya mishale) huwa inasema ukweli mara mbili kwa siku!
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika Tendwa na utu uzima wako nawe SIMAMIA HILI UACHE LEGACY,manake umma umekua na sumu juu yako kuwa uwa unakibeba chama cha mapinduzi,simamia kidete jambo hili mpaka kieleweke kwaa kuwa utakuwa umeacha MARK yako kuwa you did something SPECIAL for the Country.

  Manke ukisimamia kwa upande wako wewe wenye kusudio baya wataona AIBU kwa kuwa wewe UTAKUWA UMESIMAMIA TANZANIA,wakisimamia upinzani itaonekana WATAKAOFADIKA NI WAO NA SI TANZANIA KAMA WATAWALA WANAVYOONA.

  Please Msajili UKISIMAMIA HILI UTATUACHIA TANGIBLE DEMOCRACY KWA KUWA WEWE PIA NI MJENZI NA MSIMAMIZI WA DEMOKRASIA KUPITIA OFISI YAKO YA USAJILI WA VYAMA VYA SIASA.

  BIG UP KWAHILI USITETELEKE,SASA HIVI ITS ALL ABOUT TANZANIA.UTAHESHIMIKA KWA KUACHA MCHANGO NA UTETEZI USIYO YUMBA KATIKA SWALA LA SHERIA NYANGAU YA MAANDAMANO AMBAYO MWANASHAERIA MKUU ANAKUSUDIA KUIMBA.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati najiuliza kama AG wetu ana sifa za kuwa Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala ya kisheria. Muda mwingi amekuwa akipwaya na hutoa hoja zake kwa jazba na kisiasa. Kumbuka ushauri wake kuhusu Dowans.
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Uongozi sio kitu chepesi na haiwezekani kumfurahisha kila mtu wakati wote. Huwezi kujua labda Tendwa anajaribu kuzima moto uliowashwa na Werema unaoashiria kuzaliwa kizaazaa kisiasa. Werema amepata nafasi aliyo nayo kiushikaji na ni lazima amtetee bosi wake kwa kutumia mbinu zozote anazoweza kuzifikia hata kama itaudhi wengine. Kama vile mapenzi yasivyokuwa na masikio wala macho, acha atunge sheria yake, ikipita itatumika kinyume cha watawala pale zamu yao itakapofika nao kuitwa wapinzani. Sadamu alinyongwa kwa sheria aliyoishinikiza yeye mwenyewe ili kudhibiti wapinzani wake, akajikuta anaitumikia baada ya yeye kugeuka mpinzani ghafla pasi kutegemea. Wanajisahau sana watawala wetu. Wamuulize rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak anajisikiaje kupelekwa mahakamani akiwa amebebwa kwenye machela tena na wale aliowaita wapinzani zamani.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapa Werema aliingizwa mjini na Lukuvi na hata siku anasema hili bungeni Lukuvi alikuwa pembeni yake aki-smile. Kwa upande mwingine tangu CHADEMA wapite nyumbani kwa Lukuvi na kuanika ufisadi wake kwenye uvunaji wa misitu huyu bwana ameonekana kupambana na CHADEMA na inaelekea ni mtu wa visasi.

  Ushauri wangu wa bure wa Lukuvi, achana na CHADEMA kabisa au utajikuta umegeuzwa dodoki. You are not clean and you know it, sasa hiki kiherehere chako kitawafanya CHADEMA wapige kambi ya nguvu jimboni kwako and you'll vanish!

  Kwanza ile report ya viwanja vya wazi ulijidai kufanya wakati ukiwa mkuu wa mkoa Dar es Salaam iko wapi?
   
 10. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kwa kauli ya CG,kuwa wanarekebisha sheria kuhakikisha maandamano yakifanyika hayawaathiri wasio yaunga mkono inaweza kupitishwa kirahisi na wabunge wa ccm ila wajue kuwa sheria hyo itakuwa mwiba kwao pindi watakapogeuka chama cha upinzani,because that may happen soon or later.angalizo,enyi ccm muwe na busara,fanyeni mambo ambayo yatawasaidia hata nyie bdae kwa namna pekee ya upinzani si kufanya maandamano kwani imedhirika uchaguzi ulopita kuwa hata kupitia box la mpiga kura INAWEZEKANA...as a matter of fact,jitengenezeeni mazingira mazuri ya kuwa chama cha upinzani kuliko kuwatengenezea watawala wa kesho mazingira mazuri.am just saying!
   
 11. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  I concur with you!
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ukiona mihimili inagongana ujue kuna 'walakini' katika serikali iliyopo madarakani.
  Migongano ya Spika yuleeee vs Mkulu wa takukuru,
  Migongano ya Werema vs Feleshi,
  Mivutano ya Tendwa vs Werema,
  Hapo juu ni mifano michache tu ya 'walakini' ulio hadharani, sembuse 'walakini' usio hadharani...yaani chini-kwa-chini.
   
 13. L

  Lua JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huwa simuamini sana tendwa maana yupo kama kinyonga na kauli zake! subili tuone!
   
 14. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yule aliyetaka wabunge wapimwe akili bungeni..naona alipaswa kusema viongozi wa serikali wapimwe akili pia na mwanasheria mkuu werema angekuwa wa kwanza maana sielewi kama alifikiri kabla ya kusema...
   
 15. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Katika ofisi yake mwenyewe (AG); wengi wanasema, tena wakati mwingine bila kificho kwamba si mzuri sana katika sheria, na zaidi, waliomtangulia (hasa Chenge) walikua more competent (kisheria, si katika mambo mengine)...zaidi, kwa tabia yake binafsi ya ukale uliopitiliza, nadhani atampa tabu sana boss wake (JK) katika kuendana na kasi ya sasa nchini...in short, huyu bwana amekua AG katika zama ambazo haendani nazo, angefaa sana awamu ya kwanza au ya pili at least..
   
 16. N

  Nyampedawa Member

  #16
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu Mbopo hata mimi huwa nafiri hivyo. Wakati Sita alivyokuwa spika walikuwa wakitofautiana sana kwa namna ambayo Sita alikuwa akimuoana AG kama hafahamu vizuri sheria.
   
 17. N

  Nyampedawa Member

  #17
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Baelezee baelewe. Wao bado wako usingizi kwamba watatawala milele. Dalili zinajionyesha hawataki kuamini.
   
 18. b

  bulunga JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama hakusiikia
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  AG naona alidesa siko badala kuambulia maziwa akaambulia sumu
   
 20. Imany John

  Imany John Verified User

  #20
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  wanasemaga wanafikiri kwa matumbo na si kichwa!
   
Loading...