Uchambuzi huu una mapungufu mengi:
1. Pamoja na kwamba lengo la vyama vyote lilikuwa kushinda kiti cha Ubunge, mafanikio katika zoezi zima la Igunga hayawezi kufungwa tu katika kushinda ubunge. mwanafunzi huyu wa PhD alitakiwa kuliona hili. kwa CHADEMA ambayo haikuwepo Igunga mpaka miezi 2 tu iliyopita, kufanya ilivyofanya, na hizo asilimia ilizopata, huwezi kupuuzia jambo kama hilo. uchambuzi hauwezi kujifunga katika matokeo ya leo tu, lazima kuangalia implications kwa chaguzi zijazo. kwa mfano, hao anaosema walikuwa na umri wa miaka 15-17 kuwa ndio wapenzi wa CHADEMA, wote watakuwa na umri wa kupiga kura katika uchaguzi wa 2015, na kwa hiyo idadi ya wapenzi wa CHADEMA itaongezeka zaidi kadiri siku zinavyokwenda.
2. CCM wametumia rafu nyingi ikiwa ni pamoja na kutumia viongozi wa serikali na nafasi zao. hii inaonesha kwamba CCM wanazidi kuondoka katika siasa na kujishikiza kwa vyombo vya serikali. hili haliwezi kufunikwa na "ushindi wa Igunga".
3. kuishambulia CCM ni mbinu muafaka. ndicho chama kilicho madarakani, na ndicho kilikuwa kinatetea jimbo. mwandishi akumbuke kwamba kabla ya uchaguzi huu, CUF ndio ilikuwa chama rasmi cha upinzani jimboni hapo. lakini kampeni za CHADEMA zimewapeleka kuwa chama pinzani katika jimbo hilo. ni wajibu wa CHADEMA sasa kuimarisha mtaji huu mpya, imani waliyopewa na wana Igunga si haba. itawasaidia sana 2015. daima waangalie mbele, sio kutuama katika mambo ya jana kama msomi huyu wa "PhD" anavyotaka kutusadikisha.
4. ni vizuri kukumbuka kwamba maeneo ya Igunga yana watu ambao ni wagumu kukumbatia mageuzi. wanakumbatia serikali na kungojea wapewe maelekezo. ndio maana kuanzia mkuu wa wilaya mpaka ngazi ya chini ya utawala, walikuwa katika kuhakikisha ujumbe wa serikali ni kuchagua ccm tu, na kutumia mbinu chafu kutekeleza hilo. lakini pamoja na yote hayo, kuna kila sababu ya CHADEMA kushangilia kwa sababu pamoja na mazingira hayo magumu, wameweza kupata asilimia nzuri. yaliyoshindikana miaka yote hiii yanaweza kufanyika 2015. big up!!