Temeke: DC Jokate Mwegelo azindua mradi wa usalama barabarani

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo siku ya Ijumaa 22/10/2021 amezindua mradi wa Usalama Barabarani katika Kata ya Temeke kwa shule za msingi Ruvuma na Madenge chini ya ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Amend kwa ushirikiano na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Tarura, Jeshi la Polisi na Wananchi wa eneo husika, pia utanufaisha shule zipatazo nane .

Kupitia mradi huu shirika la Amend limeboresha miundombinu ya barabara na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule hizo, waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na wananchi wa eneo hilo kwa ujumla.

Mradi huu unatarajiwa kunufaisha takribani shule nane katika kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote watumiapo barabara hiyo.

Mradi huu umeboresha miundombinu ya barabara ikiwa pamoja na utowaji wa Elimu ya Usalama Barabara kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mandenge na Ruvuma, na Waendesha pikipiki ( bodaboda ) wa Kata ya Temeke.

@jokatemwegelo @ikulu_mawasiliano
@ortamisemi

#kaziiendelee
 
Back
Top Bottom