Mkuu wa Wilaya Jokate ameandaa mbio za Wajawazito Korogwe

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Jokate Mwegelo ameandaa mbio za Mama Wajawazito wilayani Korogwe zilizopewa jina “#MAMATHON’. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ya Mei 28 mwaka huu lengo ni kutoa elimu na kuhamasisha wajawazito kufuatilia afya na lishe bora kwa mama na mtoto.

Wanawake wote wanaohitaji kushiriki MAMATHON mkajiandikishe katika vituo vya afya vyote na MAMATHON yetu hakuna kiingilio ni bure, wanawake wote na kina baba wote katika MAMATHON hii kuna zawadi kemkem kwa kina mama na hakuna mtu atatoka mikono mitupu siku hiyo" Jokate Mwegelo

"Tutajikita katika kutoa elimu kwa vitendo pamoja na kugawa vifaa vya kujifungulia kwa wajawazito, lengo ni kuwafikia wajawazito 2,000 ambao wako tayari kujifunza kuhusiana na afya ya uzazi, ushauri juu ya lishe bora na mazoezi kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua" - Jokate Mwegelo

"Siku ya MAMATHON (Mei 28, 2023) tutakuwa na matukio yafuatayo; matembezi ya kina mama wajawazito. Mafunzo ya umuhimu wa mazoezi na lishe bora kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua, mafunzo haya yatafanywa na wataalamu" - Mhe. Jokate Mwegelo Mkuu wa wilaya ya Korogwe.

"Pia (Siku ya MAMATHON Jumapili ya Mei 28) tutatoa mafunzo juu ya mradi wa M-MAMA. Jinsi ya kupata huduma hii na umuhimu wake, washiriki watapata bure huduma ya kupima vipimo vya afya kama vile; presha, wingi wa damu, kipimo cha sukari na vipimo vingine muhimu vya afya" - Jokate Mwegelo

IMG-20230525-WA0194.jpg
IMG-20230525-WA0197.jpg
IMG-20230525-WA0198.jpg
IMG-20230525-WA0195.jpg
 
Back
Top Bottom