Tembo 60 wateketezwa na majangili hivi karibuni

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,565
2,000
Mara baada ya OPERATION TOKOMEZA MAJANGIRI kusitishwa; Tembo wapatao 60 wameteketezwa na majangili katika kipindi hiki mpaka leo hii: SOURCE: TBC-Taarifa ya habari usiku huu:
MY TAKE:
Majangili yamejionyesha kuwa na Nguvu kuliko SERIKALI NZIMA na BUNGE ZIMA. Tukiendekeza SIASA za majitaka Tanzania itabakia historia kuwa tulisha wahi kuwa na wanyama waitwao TEMBO.
Makosa yaliyofanya na askari yasisababishe Tembo wetu waishe kijinga namna hivyo. OPERATION TOKOMEZA ianze haraka iwezekanavyo, na wewe Rais J.M.Kikwete hebu Gangamaa nawewe Tembo wanaisha, wakati Tumekupa majeshi yote yawe chini yako; kinachokushinda ninini?
 

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,281
2,000
Mara baada ya OPERATION TOKOMEZA MAJANGIRI kusitishwa; Tembo wapatao 60 wameteketezwa na majangili katika kipindi hiki mpaka leo hii: SOURCE: TBC-Taarifa ya habari usiku huu:
MY TAKE:
Majangili yamejionyesha kuwa na Nguvu kuliko SERIKALI NZIMA na BUNGE ZIMA. Tukiendekeza SIASA za majitaka Tanzania itabakia historia kuwa tulisha wahi kuwa na wanyama waitwao TEMBO.
Makosa yaliyofanya na askari yasisababishe Tembo wetu waishe kijinga namna hivyo. OPERATION TOKOMEZA ianze haraka iwezekanavyo, na wewe Rais J.M.Kikwete hebu Gangamaa nawewe Tembo wanaisha, wakati Tumekupa majeshi yote yawe chini yako; kinachokushinda ninini?

Ooohh!!katibu ameingia mstuni tena
 

Sibhonike

Senior Member
Apr 10, 2011
156
195
Dahhhhhh!!!!!!
General Secretary karudi kwa speed kali sana aiseeeeee!!!!
SABINI...!!!!!!
 

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
2,000
G.S aka tembo dentist ameendelea kula vichwa kama hana akili nzuri. TZ kweli ya kijinga
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,140
2,000
Kama taarifa hiyo ni ya ukweli tembo,twiga,chui na faru watakwisha kabla ya 2015 ili watawala wapya waanze kununua wa mbegu kama alivyofanya baba Ritz moko mwaka juzi kuwaingiza faru toka South Africa!
Niliwahi kuuliza humu jamvini kuwa huyu amiri jeshi anawaogopa askari anaowaongoza? Kama jibu siyo ni kuwa hajui matumizi ya askari anaowaongoza. Angekuwa anajua upuuzi huu ungeshaisha siku nyingi sana.
Na huenda anawachukia tembo kwani kila alowapa dhamana wakitekeleza majukumu yao anawaondoa kwenye hiyo wizara. Kwa ushahidi ona idadi ya mawaziri waliotumikia hiyo wizara. Huyu ajae atakuwa wa saba tangu aitwe rais. Hii si bure kuna analonufaika nalo hapo vinginevyo angeshafanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa. Kuna mengi yanafichwa kwa kuwa tunzipenda kucha zetu! Ila inakera sana kuona anavyowalea majangili na wezi wa mali ya umma.
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,145
2,000
Ooohh!!katibu ameingia mstuni tena


Huyu Katibu kwa kweli tishio sasa! Na kama ni kweli haya yamejiri nakwambia Kibo10 mpaka mwaka kesho mwishoni hautamwona hata tembo mmoja hapa Nchini tutabakigi na historia tu!
 
Last edited by a moderator:

mzawahalisi

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
749
250
Hii mambo ni serious sana, ila kwa kuwa sina lakufanya kwasasa ngoja nicheke, 'tembo dentist!?' you made my nighT ha ha haa.
 

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,565
2,000
Kama taarifa hiyo ni ya
ukweli tembo,twiga,chui na faru watakwisha kabla ya 2015 ili watawala
wapya waanze kununua wa mbegu kama alivyofanya baba Ritz moko mwaka juzi
kuwaingiza faru toka South Africa!
Niliwahi kuuliza humu jamvini kuwa huyu amiri jeshi anawaogopa askari
anaowaongoza? Kama jibu siyo ni kuwa hajui matumizi ya askari
anaowaongoza. Angekuwa anajua upuuzi huu ungeshaisha siku nyingi sana.
Na huenda anawachukia tembo kwani kila alowapa dhamana wakitekeleza
majukumu yao anawaondoa kwenye hiyo wizara. Kwa ushahidi ona idadi ya
mawaziri waliotumikia hiyo wizara. Huyu ajae atakuwa wa saba tangu aitwe
rais. Hii si bure kuna analonufaika nalo hapo vinginevyo angeshafanya
maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa. Kuna mengi yanafichwa kwa kuwa
tunzipenda kucha zetu! Ila inakera sana kuona anavyowalea majangili na
wezi wa mali ya umma.
Kwakweli inakera, na kwa jinsi hii naanza kuhisi labda Rais naye anahusika. Haiwezekani Majangili yatambe kiasi hiki yeye yupo kimya tuu. Watu tunajifanya kutetea haki za binadamu wakati mijitu ni mihalifu. Hivi JMK nini hasa waTZ tutakacho kukumbukia?
 

mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
842
1,000
Kwakweli inakera, na kwa jinsi hii naanza kuhisi labda Rais naye anahusika. Haiwezekani Majangili yatambe kiasi hiki yeye yupo kimya tuu. Watu tunajifanya kutetea haki za binadamu wakati mijitu ni mihalifu. Hivi JMK nini hasa waTZ tutakacho kukumbukia?

Kati ya wote waliokamatwa na kuteswa hapakuwepo na hata mmoja mwenye pembe, mkia wala mavi ya tembo! Hawa jamaa mradi wao huu! Haina tofauti na ule wa kusafirisha twiga live.
 

Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,777
2,000
Nimesikia ile Operation ilikaribia kuwanasa vigogo, wanasiasa wakaingilia na tume yao
 

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
Mradi wa chama huo,tunatafuta pesa ya uchaguzi 2015, secretary general ndo mtekelezaji wa project.
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,269
2,000
wanajamvi, hakika ili uweze kupambana na majangili wa pande zote yaani maofisini
na porini,hakutakiwi kuwa na huruma hata kidogo.
cha msingi inatakiwa kufanyika uchunguzi wa kina na kutambua kweli huyu tunayepambana naye ni jangili.
nakumbuka kenya waliwahi kufanya maamuzi kama ya kwetu -TOKOMEZA- wakati wa utawala wa MH DANIEL TOROITICH ARAP MOI hawakuwa na utani hata kidogo. ushauri wangu tukubaliane kuwa tembo,faru,twiga nk wameisha uwawa.
kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuzuia wasiuwawe.lkn tukiangalia nani ? kaua aliuwa tembo ndipo siasa
,kwani chuki zinaanzia hapo kila mwenye maendeleo kidogo anaonekana anahusika na ujangili.operation ikimkuta anaadhibiwa kitu ambacho kinakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. kwa kuwa ulinzi wa maliasili hizi uko ndani ya mipaka yetu, watawala wanatakiwa wakubaliane kuwa wenye mamlaka ya kulinda na kupanga operations hizo ni polisi.
tatizo katika nchi hii ninachokiona kila mtu na kila taasisi zinazohusiana na ulinzi wanataka kufanya kazi za polisi.hivyo itapangwa itazungumzwa,kila sababu kuonyesha kuwa polisi wameshindwa kazi ili tu,wasipewe jukumu linalowahusu wapewe idara zingine.
lakini kama usalama wa taifa watafanya kazi zao zinazowahusu,kisha zile wanazotakiwa kuzifikisha kwenye idara zingine kwa ajili ya kazi zikafika kwa wakati. ufanisi ungekuwa mkubwa saana wala malalamiko yasingekuwepo.polisi nao wakitekeleza majukumu yao,kwa kupatiwa fund ya kutosha na vitendea kazi.kama ambavyo idara zingine zinavyopewa fund na magari pindi zinapotakiwa kutekeleza kazi za kipolisi baada ya kuelezea na kufafanua ushindwaji wa polisi asilia.
hakuna ambacho kingeharibika.viongozi wa polisi waache woga na kukubali kila kitu kinachotoka /kilichopangwa na idara zingine. wao ndio wataalamu suala lolote linalihusu utekelezaji wa kipolisi wao ndio wawajibikaji.yaliyotokea sasa naamini viongozi wa polisi walijua yatatokea lakini sababu ya ukauzu wao walinyamaza kimya ,
najua mioyoni mwao nasema tulijua yatatokea kitu ambacho nidhambi zaidi ya dhambi aichukiayo MUNGU.
 

Tulizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
848
1,000
Mara baada ya OPERATION TOKOMEZA MAJANGIRI kusitishwa; Tembo wapatao 60 wameteketezwa na majangili katika kipindi hiki mpaka leo hii: SOURCE: TBC-Taarifa ya habari usiku huu:

Hii taarifa ni ya kweli.. and I hate politics inapoingilia operesheni za kijeshi... Huwezi kuwakamata majangiri kwa kuwapigia magoti na kuwaomba msamaha eti umekuja kuwamata.... Ningefurahi kuona baada ya kumaliza kuwashughulikia majangiri operesheni ingehamia mijini na kuwaadhibu wafujaji na wezi wa pesa za raia wanaopigika..

Nani anajua jinsi Sokoine alivyowashughulikia wahujumu uchumi...kama uhuru wa kisiasa wa leo ungekuwepo enzi yake na haki za kibinadamu tunazoongelea leo....basi Sokoine asingeiweza ile kazi ya kuwashughulikia wahujumu uchumi..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom