Mauaji, utesaji, ubakaji na unyama wote operation tokomeza ni mbinu ya majangili.

Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
112
Ukatili uliofanyika kwenye operation tokomeza ni mbinu iliyosukwa kiufundi na mtandao waa majangili. Mbinu hii wamesuka kiufundi wakiwatumia viongozi wa operesheni hiyo. Na kati ya mbinu waliyotumia ni Mauaji, Utesaji na ubakaji wakijua kabisa kuwa wakifanya hivyo ni lazima operesheni hiyo itasitishwa na wao kuendelea na ujangili kama kawaida. Hebu fikiri kuanzia operesheni hiyo kusitishwa Tembo 60 wamekwisha uawa. Hii inadhihirisha kabisa kuwa viongozi wakubwa wa serikali ni wahusika wa biashara hii ya meno ya tembo. Serikali ina vyombo vyote vya usalama kama Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Jwtz na jeshi la wanyama pori lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa kudhibiti majangili. Je ni kusema kuwa vyombo vya ulinzi havina uwezo?. Kuna baadhi ya viongozi wamekwisha tuhumiwa na vyombo vyao vimekamatwa vikiwa na shehena kubwa ya meno ya Tembo lakini mpaka hivi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake. Hii haiitaji sana kufikiri bali jibu moja ni kuwa wanaofanya biashara hii ni viongozi wasiokuwa waaminifu wa chama na serikali. Ndugu watanzania wenzangu tuiombee sana nchi hii ambayo imekosa viongozi waadilifu wenye mapenzi mema na hii Nchi. Tumeshuhudia hata waziri wa utalii ndugu Kagasheki akijiuzulu lkn kwa maoni yangu ni kwmba mfumo mzima umeoza na hata akiingia mwingine hatutarajii mabadiliko makubwa. Ndugu wana Jf tutafakari kwa kina tukitanguliza maslahi ya Nchi na vizazi vyetu. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom