Tembea KM 200 kwa 22,500 tu

Tembea KM 200 kwa 22,500 tu

~ Funga mfumo wa gesi asilia kwenye gari lako
~ Mfumo wako wa petrol au diesel uliopo hauondolewi unabaki

~ Kwa Mtungi wa kilo 15 gesi asilia unaogharimu shilingi 22,500 unatembea kilomita 200

~ Chaguo litakuwa lako kutumia mfumo wa gesi au petrol/diesel uwapo safarini.

GARI LAKO SASA LINAWEZA KUTUMIA GESI ASILIA

Utangulizi:

Taasisi Teknologia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na wadau wengine wa gesi asilia tunaongeza mfumo wa gesi asilia kwenye magari yanayotumia petrol. Mfumo huu unamwezesha mwenye gari kuwa na uwezo wa kutumia gesi asilia au petrol kulinga na upatikanaji wake. Kwa sasa tunafunga magari yote ya petrol kuanzia madogo IST hadi makubwa V8. Pia tumeanza kufunga gesi asilia kwenye daladala.

Gharama za kuweka huu mfumo:

Gharama inategemea na ukubwa wa injini yaani idadi ya cylinder za injini yako. Mfano kwa gari zenye:-

1. cylinder 4 gharama ni 1.8m,

2. Cylinder 6 gharama ni 2.2m

3. Cylinder 8 gharama inaenda mpaka 2.5m.

Hata hivyo kuna baadhi ya gari gharama hizi inaweza zidi kutokana na mfumo wa injini (kama brevis, crown na voxy ambayo injini zake ni GDI)

Faida za huu mfumo:

1. Unafuu wa gharama za uendeshaji;
Kutumia gesi unapunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 40 mpaka 50.

Bei ya gesi asilia iko chini sana, ukilinganisha na petrol. Mfano 1kg ya gesi ni sh 1500/= ukilinganisha na sh 2,200/= kwa lita ya petrol.

Kilo moja ya gesi unaweza kwenda zaidi ya km 20, na kwa mtungi wa 15kg ambao ni sh 22,500/= unaweza kwenda zaidi ya km 200.

2. Kupunguza uchafuzi wa mazingira;
Gesi ni safi ukilingalinisha na petrol au diesel.

3. Kuongeza kipindi cha kufanya matengenezo ya injini yako;
Kwa kuwa gesi asilia ni safi, basi hata injini yako inakuwa salama zaidi. Mfano kama ulikuwa unafanya matengenezo kila baada ya km 3000, kwa kutumia gesi asilia unaweza kufanya hata baada ya km 9000.

4. Gesi asilia ni salama zaidi;
Gesi asilia ni salama zaidi ukilinganisha na petrol kwani inahitaji joto kubwa sana ili iweze kuwaka ukilinganisha na petrol.

Mahali pa kubadilishia mfumo:

Kwa sasa Tanzania nzima ni sehemu moja tuu inafanya kazi ya kubadili, nayo ni Taasisi ya tecknologia Dar es Salaam (DIT).

Mahali pa kujazia Gesi:

Kwa sasa mahali pa kujazia gesi ni ubungo maziwa. Hata hivyo serikali iko mbioni kuongeza vituo zaidi ya 5 sehemu mbalimbali hapa Dar es salaam.

Hitimisho:
Taasisi ya Tecknolojia Dar es salaam DIT inakukaribisha sana uje uweke mfumo wa gesi asilia kwenye gari lako, kwani ni nafuu na salama zaidi.

Asante
Dr. Esebi Nyari
Mratibu wa gesi asilia- DIT
0755821240
0717962127
eusnyari@gmail.com
----------------------------------

Amua sasa kupunguza gharama za uendeshaji wa gari yako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Limitations ni nyingi mno kwani kituo kimoja tu cha kujaza gas kwanini msifanye iwezekane kununua mitungi ya gas mahali popote?
 
Kwa hizo sh 22,500tsh unatembea kilomita ngapi kwa mafuta? Nyoosheni maelezo. Nyie ni chuo kikuu.
 
Kwa hizo sh 22,500tsh unatembea kilomita ngapi kwa mafuta? Nyoosheni maelezo. Nyie ni chuo kikuu.

WaTanzania tumekuwa wavivu wa kusoma yaani heading umewekewa kila kitu lakini bado unauliza maswali ya hovyo hovyo
 
WaTanzania tumekuwa wavivu wa kusoma yaani heading umewekewa kila kitu lakini bado unauliza maswali ya hovyo hovyo
Kusoma tumesoma ila mtoa mada kachanganya maelezo ndio maana ana kanganya

Yeye kasema kilo moja ya gesi utaenda zaid ya 20km wakati huo huo anasema mtungi wa kilo 15 za gas unatembea kilomita 200 sasa piga hesabu hapa kilo15 za gas ukitembea 200km maana yake kwa 1kg ya gas utatembea kama 13.3 km, sasa hiyo 20+km aliyosema mtoa mada inatokeaje? Ndio hapo tunapo ona ujanja ujanja

Pia gharama za installation ni kubwa mno we ngoja vijana wa mjini waingie kitengo na mchina watu watafungiwa huo mfumo hadi kwaTsh. 20,000/=.
 
Kusoma tumesoma ila mtoa mada kachanganya maelezo ndio maana ana kanganya

Yeye kasema kilo moja ya gesi utaenda zaid ya 20km wakati huo huo anasema mtungi wa kilo 15 za gas unatembea kilomita 200 sasa piga hesabu hapa kilo15 za gas ukitembea 200km maana yake kwa 1kg ya gas utatembea kama 13.3 km, sasa hiyo 20+km aliyosema mtoa mada inatokeaje? Ndio hapo tunapo ona ujanja ujanja

Pia gharama za installation ni kubwa mno we ngoja vijana wa mjini waingie kitengo na mchina watu watafungiwa huo mfumo hadi kwaTsh. 20,000/=.
Pia ni vigumu sana kutumia mfumo wa gesi wakati kipo kituo kimoja tu cha kujaza gesi Tanzania nzima. Hili ndilo tatizo la nchi yetu, hatuna wajasiriamali. Hawa DIT wamehodhi hii biashara na hawataki kuacha wawekezaji waje na vituo ya kujaza gesi mikoani halafu wanategemea mtu atumie huu mfumo.
 
Yani mwenye V8 na mwenye ist wataenda km200 kwa kg 15 za gas?hajaandika kisomi kabisa
 
Mnazingua niko dodoma
Nikajaze mtungi ubungo maziwa?
Otherwise mfumo ni kwa wakazi wa dar
Kwenye heading ungesema kabisa kwa watu wa dar
 
Kama mfumo huu wa gas unapunguza matumizi ya mafuta kwa asilimia 40 mpaka 50 basi serikali ingeweka kipaumbele cha kubadilisha mfumo wa mafuta wa mabasi ya mwendo kasi mapema sana ili kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na nauli kwa watumiaji wa mabasi hayo.

Kwa magari ya binafsi kama daladala nk pangewekwa mpango wa kufunga mfumo kwa njia ya mkopo, mfano mtu atoe pesa nusu ya mfumo na nyingine atakuwa analipa kidogo kidogo kila anaponunua gas. Kwa sababu gas ni yetu, kukiwa na mpango mkakati mzuri baadaye tutapunguza matumizi ya pesa za kigeni(uingizaji wa mafuta kutoka nje).

Swala linaonekana zuri lakini naona kama halijapewa kipaumbele kwa sababu siku hizi wafanya maamuzi nao ni wafanya biashara mfano wa mafuta nk au wanafaidika na zile 10% za importation ya mafuta. Tujaribu kuwa serious kama kweli kuna faida kama mlivyo onesha
 
Hao watu ni wasumbufu sana, ukifunga huo mfumo bado watakupa manyanyaso kwenye kujaziwa gesi. Utaambiwa ukachukue kibali kwa dr. na huko ukienda utaambiwa dr. hayupo kasafiri nje ya nchi na hata akirudi leseni yake ya kutoa hivyo vibali imeisha muda, na hapo hapo utatakiwa ulipe shilingi laki moja kwa ajili ya kupewa hicho kibali na u-renew kila baada ya miezi 6. Kiufupi kuna upuuzi na ujanja ujanja mwingi kwenye huo mradi....
 
Kwa Ist nnaenda Km 450 kwa 30 litres.. gharama za kufunga huo mfumo ni kubwa sana na ukizingatia kwamba kituo cha kujaza hio gas asilia kipo Dsm pekeake. Hivyo sisi wa mikoani itakua ni kuchezea pesa tu.
 
Back
Top Bottom