Teknohama inavyoweza kuimarisha utawala bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknohama inavyoweza kuimarisha utawala bora

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jul 15, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  TEKNOHAMA INAVYOWEZA KUIMARISHA UTAWALA BORA


  Teknologia ya habari na mawasiliano TEKNOHAMA ( ICT ) imekuwa ni chombo imara katika jinsi serikali mbalimbali duniani zinavyowasiliana na wananchi . Mtandao umekuwa ndio nyenzo kuu ya kuhakikisha mawasiliano kati ya wananchi na serikali zao yanakuwa imara pamoja na kuwezesha programu na aina nyingine ya vifaa kutumika katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa sawa katika kuwasiliana na serikali zao .

  Kuna wakati ambapo unaweza kuona picha yenye maelezo kuhusu sehemu fulani labda barabara mbovu au mazingira machafu kwenye blogu fulani kisha ukaona watu kadhaa wameweza kutoa maoni yao kuhusu picha hiyo baada ya muda wahusika wa eneo hilo au viongozi wanaenda kufanyia marekebisho barabara hiyo huu ni mfano mmoja wa jinsi TEKNOHAMA inavyoweza kufanya kazi kwa jamii .

  Mtandao umewapa fursa wananchi wengi kuweza kuwasiliana haswa kwa kutumia mitandao jamii ambayo serikali kadhaa au idara za serikali hizo kuanzisha kurasa zao au tovuti za serikali ambazo zinaviunganishi na mitandao jamii kwa ajili ya makundi haya mawili kuweza kuwasiliana kwa ukaribu zaidi .

  Mahusiano haya kati ya serikali na wananchi wake yako kwa njia nyingi kuna wale wananchi ambao wanapenda kugombea nafasi kadhaa za uongozi kwenye vyama au sehemu zingine wengi wao wameweza kutumia fursa zilizopo kwenye mitandao jamii kwa ajili ya kutoa maoni , kuulizwa maswali au kishiriki mijadala mingine ya kitaifa mfano unaweza kutembelea www.wanabidii.net tafuta mada inayoitwa Natangaza Nia .

  Ukitaka kuona jinsi TEKNOHAMA inavyoweza kuleta utawala bora kwa nchi nyingine unaweza kutafuta habari zinazohusu kiongozi wa Venezuela alivyoamua kutengeneza account kwenye mtandao wa twitter ili wananchi wawe wanafuatilia mambo kadhaa anayoyafanya yeye pamoja na kuulizwa maswali ambayo anaweza kuyajibu hapo hapo kwa kutumia vijana zaidi ya 50 ambao wameajiriwa nae kwa ajili ya kujibu maswali na maoni mbalimbali .

  Kwa upande wa nchi ya Marekani Jimbo la Minnesota wananchi wao wanaweza kufuatilia mijadala mbalimbali inayohusu eneo lao kwa kutumia tovuti maalumu za serikali ya jimbo hilo au kwa njia ya televisheni na wanaweza kuuliza maswali na maoni yao moja kwa moja kwa uwazi .

  Hapa kwetu Tanzania tuliwahi kuwa na mtandao kama www.wananchi.go.tz ambao lengo lake kuu lilikuwa ni kwa wananchi kutoa maoni na mengine ya kujenga jamii zao kwa serikali ya Tanzania mtandao huu umepotea kidogo kwa sasa hivi lakini unaweza kuunganishwa na tovuti zingine za jamii na kutangazwa vizuri inaweza kuleta tija kwa jamii nyingi hapa Tanzania .

  Kuna mtandao unaoitwa www.tzonline.org ambapo unaweza kupata taarifa kadhaa zinazotolewa na serikali au vyombo vinavyohusika na serikali moja kwa moja pamoja na kuanzisha Tanzania Awareness List ambapo unaweza kupatiwa taarifa za kila mwezi kuhusu Tanzania na wananchi wake hizi zote ni kazi ambazo zimeweza kufanyika kwa uwazi kwa Kutumia TEKNOHAMA .

  Kwa wale wasikilizaji wa radio watakuwa wamewahi kusikia Tangazo moja ambapo mfanyakazi mmoja wa serikali analalamika kwa kukosa taarifa Fulani toka makao makuu na sikuhiyo kiongozi anatakiwa kutembelea sehemu yake na mwenzake akamwambia si aende kwenye mtandao achukuwe taarifa hiyo lakini inaonyesha mwenye wasiwasi alikuwa hajui au hana elimu ya teknohama hata kidogo kiasi cha kutokutambua hili suala .


  Pia Kumekuwa na changamoto zingine za kiulinzi na usalama haswa kwa wale vinara wa kutoa maoni na kuuliza maswali kwenye mitandao hii haswa ya jamii mfano uchina kuna kesi kadhaa za wanablogu kukamatwa na kufungwa kutokana na maoni yao wanayoyatoa na kujihusisha na mitandao hii kama ilivyotokea hapa nchini kwa waendeshaji wa mtandao wa JamboForum nao kukamatwa na vyombo vya dola .

  Nchini iran baada ya Wanaharakati kutumia kwa ukamilifu mtandao jamii wa Twitter kwenye maandamano yao na kutoa taarifa zingine serikali ya nchi hiyo ikaanza kufuatilia wenye kumiliki anuani za twitter waliokuwa viongozi wa maandamano yao na kwa baadhi ya nchi serikali za nchi hizo zinatengeneza mitandao yao jamii ambayo inafanya kazi kwa maslahi ya uongozi ulio madarakani .

  Pamoja na kuwa na vikwazo kama hizo bado serikali zinaweza kutumia TEKNOHAMA haswa mitandao jamii katika kuwasiliana na wananchi wao na kufanyia kazi yale ambayo wanaona yanawafaa kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kutumia sheria na taratibu zinazoongoza nchi husika .  YONA F MARO
  WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Shy
  naona kwako Teknohama Umebobea zaidi kwenye mitandao ya kompyuta na tovuti. Naongezea kitu ambacho watu wengi tunakisahau Tukiongelea mambo ya TEKNOHAMA.

  Nadhani kumekuwa na Kosa kwenye taasisi nyingi za kutoa huduama na biashara kutumia gharama kubwa kujaribu kuona kuona suluisho la matatizo mengi au kuwa karibu na wanachi zaidi ni kuanazisha website,blog na vitu vinavyoendana.

  Kwangu mimi hasa kwa serikali na taasisi zake kwa tanzania.naona kuna udhaifu na wengi wentu tumekuwa tunao. Tunasahu kuwa tunaposema TEKNOHAMA= wafanyakazi +SIMU+ FAX, TOVUTI, na IS nyingine.

  Unakuta Wizara una mtandao tena labda wanajitahidi kuwa na sehemu ya kupokea maoni. lakini wizara hiyo hiyo mwananchi wa magu akipiga simu kuulizia jambo fulani au kuelezea kero yake response anayopata ni tofauti. Ukweli wataanzanai wengi tuna access na ufahamu zaidi wa matumizi ya mawasiliano ya SIMU kuliko tulivyo na acces na mawasiliano ya TOVUTI .

  Nadhani hii ni changamoto kwa TAASISI nyingi.

  • Taasisi ina TOVUTI ambyo ni rahisi kuhesabu idadi ya kero, mapendekezo yaliyoripotiwa .Lakini Taasisi hiyo hiyo haina rekodi ni simu ngapi za kero zimeingia kwa wiki.

  • Unapiga simu wizara fulani wewe unatakiwa kujitambulisha ni nani wakati aliyepokea hawajibiki kujitambulisha.
  • taasisi ya huduma haina call register
  • Inashangaza kazi za masekretary wa zama hizi za TEKNOHAMA hazitofautinia na kazi za masecretary wa 1980.Masecretary wanatakiwa watumike kopokea maoni na kero na kufuatiloa majibu kwenye idara zinazohusika na kurudisha majibu kwa mwanachi husika.
  Kwa hiyo nadhani Taasisi nyingi za serikali zinaweza kuwa karibu zaidi na wanachi bila hata kuwa na TOVUTI.
   
Loading...