Tegeta Escrow: Waliochota kwenye Masandarusi watajwa, gari lililotumika kubeba ni la Ikulu

Katika kila chama kuna wezi sasa hivi ndani ya CCM tunawashughulikia wabaki wasafi
Nachojua katika magamba kila muhula una wezi wake na ufisadi wake ngoja huu uishe ndio mtaona ufisadi wa kila namna utakavyo funuliwa ccm ni ile ile
 
Atakua yule mshikaji mnadhimu au mnikulu aliestaafu ndie alitoa gari.

Hili la kupambana na rushwa Magufuli baba tunyooshe. Umeonyesha kua uwezo na nia unazo za kupambana na wezi.

Kama hizi hela hazikua za wizi kwa nini zilichukuliwa kwenye masandarusi na mabegi. Hela halali ukazichukue kwa kujificha?

Baba tunyooshe.
Siyo shaban kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama fedha zilikuwa zao halali kwanini wakachukue kwenye "visalfeti"? Hao nao waswekwe kwa utakatishaji.
Mpaka sasa hivi kauli rasmi ya Serikali iliyotolewa na Mkuu wa nchi wakati huo ni kuwa zile zilikuwa pesa za watu binafsi. Hivyo suala kuwa mtu alibebaje zake binafsi au alitumia mfuko gani kubebea haliwezi kuwa ni hoja ya msingi hapa.
 
Kwa kuhamisha magoli tu hamjambo, hata hivyo tumekwisha wazoea hamna effect yoyote ya kusaidia watanzania wote lengo lenu mnataka tuvurugane tu mpate sababu ya kwenda kuishi uhamishoni. Wapuuzi kabisa nyie. Sasa watajwe wa Simba Trust then what! Hauto suluhisho ni kalalamika tu. Msitubabaishe!!!!
Tulishasema hizi ni drama za jpm tu!
aanze kuwataja wale waliomo kwenye simba trust ndio tutamuona sio mpiga porojo!
ila masuala ya kusema eti fulani muacheni apumzike......

Haya ccm anandamaneni kumpongeza! kubafuuuu!!
 
Waligawana hadharani kama mbwamwitu wanavyomla ngiri, utashangaa huku nako Chenge yupo, duuuh Chenge ni mwisho wa matatizo
 
Mimi nachosangaa tu kuona Watanzania wakiwa na imani na ccm tena kutaka iendelee kuongoza baada ya miaka 50 ya kutufikisha hapa

Tatizo la wananchi wanakosa mbadala. Mwaka 2015 wananchi walidhani watapata mbadala ila wakachanganyikiwa pale fisadi aliyekuhubu ndani ya CCM na kujitokeza eti ndiye mbadala wa rais kutoka CCM kisa alikatwa kuwania urais ndani ya CCM. Wananchi wenye akili hawakukubali upuuzi huu na wakairudisha CCM. WaTZ hawadanganyiki kirahisi sana.
 
Hawa woooote wanyongwe tena mbele ya wakuu wa phase 3&4. Hawa wakuu ambao si wapimbavu na wala si malofa wana kinga, nadhani ni kinga ambayo haiwazuii kurejesha pesa ya mgawo nasikia nyingine ziko simba trust na south Africa. Kinga yao iwaachie uhai tu basi, mali yetu warudishe. Haya ni mambo ya aibu, kwanza yamemkwaza sana JPM ktk kutekeleza kile alichokusudia kuwafanyia watanzania. Kama si uchafu huyo hata Bunge lingekuwa live, na wanasiasa wangekuwa mtaani na huenda wangekuwa hawana shughuli maana mafisadi wangeishakwisha, hewa zingeishatoweka, tungekuwa tunaogelea katika makinikia.
 
Ikulu Ipi? Hivi gari ya Ikulu Inaweza Kufanya hiyo kazi? Walikosa hata Noah tuu Wakatumia Gari lenye Logo hii pale mbele na (E) ambayo Ni rahisi kujikana magari hayo huwa hayaonekani Hovyo hata karakana ya Kutengeneza Magari hayo yakiharibika Ipo Ikulu palepale

Kwa Propaganda za Kitoto kama hizi acha Magazeti ya Kipuuzi kama Haya yapigwe Ban!

DBDi-xOXcAAsbV0.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom