Msenyele
JF-Expert Member
- Feb 7, 2012
- 338
- 86
Habari za leo wanajamvi? Bila shaka mko njema kabisa baada ya kumaliza shughuli za hapa na pale, hasa ukizingatia asubuhi ndo inatoa picha kamili ya siku.
Turudi kwenye mada, simu tecno y6 takribani miaka mitatu sasa. Wakati simu zinazimwa sehemu ambapo line ya voda ilipoteza network na nilipoiweka kwenye simu nyingine ikasoma vizuri.
Kwa kuwa nilikuwa natumia tigo pia nikadhani pengine sehemu line imeharibika nikajaribu hivyo nikazibadilisha kwa kuweka sehemu palipokuwa na voda nikaweka tigo ikasoma na palipokuwa na tigo nikaweka voda ikasoma na hivyo nikaendelea kula maisha kama kawaida.
Mwezi mmoja baadae voda ikapoteza network tena (ikawa inaandika emergency call only). Nikaona isiwe taabu, nikajaribu kuweka airtel ikakubali na voda nikawa naitumia kwenye simu nyingine na maisha yakaendelea kusonga mbele.
Wiki iliyopita airtel imegoma nikajaribu kuzibadilisha tigo na airtel zikagoma zote na nilizozirudisha kama zilivyokuwa mwanzo tigo ikakubali, na sasa simu imekuwa ya line moja na huenda na yenyewe itapotea muda si mrefu na ikipotea tigo nitakuwa nimebakiza kutumia ttcl, zantel, halotel na sasatel.
Nawauliza wanajamvi, ndio tcra bado wananyemelea simu feki, maana wataniua na pressure ya kulikosa jamvi hili maridhawa.
Na je, kama itakuwa inaelekea kwenye kifungo cha tcra hakuna maujanja ya kuirejesha tena uraiani?
Naomba kuwasilisha