Tecno wanakuletea phantom 6 inakuja na ram ya 6gb na 32gb rom

TECNO Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
192
Reaction score
217
Kutoka Tecno wanakuletea Phantom 6, inakuja na RAM Ya 6GB na 32GB ROM.

Kuna fununu zilizosambaa kuwa Septemba hii ndio uzinduzi rasmi wa toleo jipya la Tecno Phantom huku ikitabiriwa kuwa ya kipekee kabisa tofauti na matoleo mengine kutolewa. Uzinduzi huu umezusha uvumi mkubwa miongoni mwa wale wapenzi simu. Kama inavyotarajiiwa, Tecno Phantom 6 itaweka rekodi katika soko la simu kimataifa.

Binafsi, bahati haikuwa yangu kupata fununu kamili mpaka nilipodokezwa na baadhi ya vyanzo vya habari vya kuaminika kuwa Tecno Phantom 6 imeboreshwa na itakuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhi kumbukumbu ikikadiriwa kuwa 6GB RAM na 32GB ROM.

Naweza nisiwe sahihi lakini pasi na shaka ninachotabiri ni kwamba Tecno Phantom itakuwa imeboreshwa zaidi kwenye uwezo wake wa kuhifadhi data yaani “Storage”. Ni adimu sana kupata simu yenye 6GB kama Tecno Phantom itakuwa na uwezo huu, itakuwa ni gumzo.
Processor.jpg

INAAMAANA GANI SMARTPHONE KUWA NA RAM KUBWA

Kwa uzoefu wangu, kuwa na RAM kubwa inamaana simu ina uwezo mkubwa wa kuchakata kulingana na matakwa ya mtumiaji, hii inamaanisha kwamba simu yako (Endapo utaamua kununua Phantom 6 na ninakushauri uinunue) haitokuwa inakwamakwama. Nafahamu matoleo kadhaa ya simu zenye uwezo mkubwa wa kuchakata ambapo inaweza kuendesha hata Apps 30 tofauti kwa mpigo bila kusuasua, lakini nikupe tahadhari kwamba matumizi yako ya data yatakuwa ya kukwamakwama sana.

Wakati faida mojawapo ikiwa kuendesha App tofauti kwa mpigo, faida nyingine ni kuwa ukubwa wa RAM ya Phantom 6 inaondoa tatizo la simu kupata moto. Kwa ajili ya kawaida huu ni ujanja ambao watengenezaji wa simu wametumia teknolojia na vifaa vinavyozuia simu kupata moto kupitiliza. Hivyo, mtazamo wangu kuhusu Tecno Phantom 6 ni kwamba inaweza ikawa sio tu yenye RAM ya 6GB pia prosesa ya hali ya juu.

Tunatumaini uzinduzi huu utamaliza mzozo na uvumi unaoendelea. endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.

Facebook: TECNO Mobile | Facebook

Instagram: TECNO Mobile Tanzania (@tecnomobiletanzania) • Instagram photos and videos

Twitter: TECNO Mobile TZ (@TECNOMobileTZ) | Twitter
 
An tekno ata waboresheje still can't buy it....used it once na ilkua boring sana.....
 
Wasotutishe na Ram iwapo processor itakuwa mbovu....

Compare 1GB RAM ya iPhone na 1GB ya Samsung au hata Tecno...

iPhone inakuwa ipo njema so 6GB zao waangalie na Processor
 
Simu za tecno utakuta camera ni 13 mega pixel lakini display ina 135 pixel per inch.[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kutoka Tecno wanakuletea Phantom 6, inakuja na RAM Ya 6GB na 32GB ROM.

Kuna fununu zilizosambaa kuwa Septemba hii ndio uzinduzi rasmi wa toleo jipya la Tecno Phantom huku ikitabiriwa kuwa ya kipekee kabisa tofauti na matoleo mengine kutolewa. Uzinduzi huu umezusha uvumi mkubwa miongoni mwa wale wapenzi simu. Kama inavyotarajiiwa, Tecno Phantom 6 itaweka rekodi katika soko la simu kimataifa.

Binafsi, bahati haikuwa yangu kupata fununu kamili mpaka nilipodokezwa na baadhi ya vyanzo vya habari vya kuaminika kuwa Tecno Phantom 6 imeboreshwa na itakuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhi kumbukumbu ikikadiriwa kuwa 6GB RAM na 32GB ROM.

Naweza nisiwe sahihi lakini pasi na shaka ninachotabiri ni kwamba Tecno Phantom itakuwa imeboreshwa zaidi kwenye uwezo wake wa kuhifadhi data yaani “Storage”. Ni adimu sana kupata simu yenye 6GB kama Tecno Phantom itakuwa na uwezo huu, itakuwa ni gumzo.View attachment 398195

INAAMAANA GANI SMARTPHONE KUWA NA RAM KUBWA

Kwa uzoefu wangu, kuwa na RAM kubwa inamaana simu ina uwezo mkubwa wa kuchakata kulingana na matakwa ya mtumiaji, hii inamaanisha kwamba simu yako (Endapo utaamua kununua Phantom 6 na ninakushauri uinunue) haitokuwa inakwamakwama. Nafahamu matoleo kadhaa ya simu zenye uwezo mkubwa wa kuchakata ambapo inaweza kuendesha hata Apps 30 tofauti kwa mpigo bila kusuasua, lakini nikupe tahadhari kwamba matumizi yako ya data yatakuwa ya kukwamakwama sana.

Wakati faida mojawapo ikiwa kuendesha App tofauti kwa mpigo, faida nyingine ni kuwa ukubwa wa RAM ya Phantom 6 inaondoa tatizo la simu kupata moto. Kwa ajili ya kawaida huu ni ujanja ambao watengenezaji wa simu wametumia teknolojia na vifaa vinavyozuia simu kupata moto kupitiliza. Hivyo, mtazamo wangu kuhusu Tecno Phantom 6 ni kwamba inaweza ikawa sio tu yenye RAM ya 6GB pia prosesa ya hali ya juu.

Tunatumaini uzinduzi huu utamaliza mzozo na uvumi unaoendelea. endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.

Facebook: TECNO Mobile | Facebook

Instagram: TECNO Mobile Tanzania (@tecnomobiletanzania) • Instagram photos and videos

Twitter: TECNO Mobile TZ (@TECNOMobileTZ) | Twitter
Haiwezi kuweka historia kwenye soko la simu maana hata huko china zinako tengenezwa hawszitumii we hushangai china kuwa soko kubwa la iphone.
China simu zinazobamba wanazotengeneza waoni xiomi sio tecno. Tecno wanatuuzia sisi africa
 
unanunua tecno simu latest version kabla hujamaliza kuichaji unaskia toleo jipya limetoka!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Nimecheka kwa kweli
 
Back
Top Bottom