Tecno Phantom ushauri tafadhali

Hatukatai Tecno in low quality products ,lakini pamoja na udhaifu wao bado wanakupa 12+1 monthly warranty....... technical supported sasa ni sawa kununua IPhone au Galaxy inayoingizwa nchini kama refurbish product?....au clone S4 isiyokuwa Na uhakika ikiharibika itatengenezwa na nani ....kwa hili nafikiri Tecno ni mshindi.
 

Phantom langu hapa nakong'oli tu.....addicted to tecno.
 
HAYA KANAWENI MIGUU MLALE NA HUU MJADALA UMEFUNGWA RASMI......UKIBISHA UTAPIGWA TU.

sawa kabsa, nadhani mjadala umekamilishwa hivi
1. samsung huwezi ifananisha na tecno
2. kununua tecno phantom kwa laki nne na nusu ni kuibiwa, ni heri kununua galaxy s4 clone kwa laki 2-3[/QUOTE]

Kwahiyo suala ni bei TU, ukibisha unapigwa.
 

Nakubali, tecno yuko vizuri hawa kina Samsung, nokia, sony na wengineo ni maigizo tu na mbwembwe za bei otherwise kazi ni ile ile.
Mimi natumia Precision Air, oooh mimi natumia fasjet, mwingine anatumia Excel Air lkn wote tunatia team kunako husika.
Hii ni biashara tu ambayo mchina anataka kuiteka na ameshaiteka muda mrefu.
Hii teknolojia ni rahisi sana tatizo ni kuijua tu sasa mchina anagharamia kupata elimu then anai-deliver nchini kwake wanafanya kazi.
Kwa Africa tecno itauzwa saaaana na matumizi yote ni sawa sawa na hayo ya Samsung, Nokia,Sony, Huawei n.k
Hakuna cha bei wala nini tunataka huduma tu.
Wapi Yutong inifikishe Mwanza from Dar chap, nataka nini mimi??
Jikague hapo ulipo kama huna kitu chochote cha kichina, hata key holder
 

Hadi boksa made in China mpaka yao ni uchina mtupu....UKIKAHIDI,UTAPIGWA,NASEMA WAPIGENI TU,TUMECHOKA.
 
Umegongelea msumari wa nchi sita, mkuu Kenwood..
 

Hapo sawa.
 
Mmmh mtoto mzuri kama mimi kutumia techno?hapana......jamani
 
Nimetokea kuipenda Samsung Galaxy S4 clone.
 
Kumbe humu kuna promotion za ulimbwende.
 
kinachowakatisha tamaa ni jina tecno au mchina????.wengi mmeiponda sana tecno bila kujua kuwa hiyo galaxy mnayoifagilia ingawa kusema ukweli wengi wetu uwezo wa kuinunua hatuna,kumbuka kuwa inatengenezwa korea jirani na china.bora mngeifagilia htc mngeshika hisia zangu.yote tisa phantom simu ya ukweli
 

umeona eeeeeeeeeeeeeee!!!!!.tuwashauri wabadili jina
 
ukiinunua futa jina tecno phantom....halafu usitangaze km ni tecno
kwa kupiga na kupoke kusurf na kudownload inafaaaaa....

sema phantom jina kama bomu.

maana ya phantom si ghost or illusory thing?????? duh....hapana sikushauri
 
umeona eeeeeeeeeeeeeee!!!!!.tuwashauri wabadili jina

Tatizo kubwa ni hili jina " Tecno " lkn simu hii hii ya material ya kuokoteza dampo itaendelea kuzipiga bao simu zenye majina makubwa kama Nokia sbb ya platform isiyo na wapenzi ya window .......karibu Tecno katika ulimwengu mpya wa Kit Kat 5.0...,,
 
Mkuu, ukinunua benz mil 60 na mimi nikanunua mark ii grande mil 15, unaweza ukaona kuna tofauti ya bei lakini wote tutaenda ofisini na gari hizo tutapaki jioni tutarudi nyumbani,weekend kila mtu ataenda beach na gari yake na mwisho wa mwaka kila mtu ataenda kijijini kwao kusalimia na gari yake. Unachotakiwa kujua bei ni tofauti lakini function ni sawa.pole kwa kupigwa simu bei kubwa (mara tatu ya tecno) lakini function zinafanana.
Ndio maana mmeulizwa hapo juu, tuoneshe kitu unafanya kwenye hiyo s4 yako na phantom a+ ikashindwa.
 

Nakubaliana na wewe mkuu ukitaka twende kwa level hii ya kienyeji
Maana hata mnywa mataputapu na mnywa Heineken wote wanalewa tu

Hili ni jukwaa la sayansi na teknolojia lakini kama unataka tujadili mambo ya kitaalamu kisiasa basi tutaishia gongo na johnny walker zipo sawa kwakuwa wote mnalewa

Binafsi nazungumzia kitaalamu ingawaje mimi sio mtaalamu kivile, kwamba Phantom A+ na S4 hazipo sawa hata kidogo
S4 hajamzidi A+ bei tu kama unavyoweza kujidanganya, KAMZIDI SPECIFICATION kitu ambacho kinadetermine ubora wa simu

Mwisho labda niseme hakuna anayesema A+ ni simu mbaya kutumia, ni nzuri sana kwa mazingira ya uchumi wetu lakini hili lisitutie upofu na kuanza kujidanganya eti A+ ipo sawasawa kwa kila kitu na S4

Na kama kweli hujui ni vitu gani S4 inaweza kufanya A+ haiwezi basi utakuwa unauelewa mdogo sana kuhusu haya mambo mkuu
 
Application zote zipo kwa phantom kama zilivyo kwa samsung. Unaweza kudowload nyingine yo yote uipendayo. Mm hutumia Phantom na naridhika nayo sana. Hiyo S 4 ya mabishoo tu haina la zaidi. Nunua phantom usijali. Isitoshe bei ni one third ya s 4 mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…