Tecno camon 16s yazinduliwa rasmi

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezindua rasmi simu yake mpya toleo la CAMON 16s leo jijiini Dar es Salaam pamoja na kuwatambulisha mabalozi wa simu hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, meneja mahusiano wa kampuni hiyo bwana Eric Mkomoya amesema simu hiyo sio tu imelenga kurahisisha mawasiliano bali kuleta mapinduzi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazotegemea zaidi teknolojia hasa upande wa kamera.

“Pamoja na kwamba simu ni kifaa cha mawasiliano lakini kutokana na sifa za TECNO CAMON 16s mtumiaji akiitumia kwa ufanisi itampa maslahi makubwa kuanzia wafanyabiashara, wajasiriamali , wasanii, wafanyakazi maofisini na hata wanafunzi wa vyuo vikuu” Amesema Mkomoye.

Image 1.jpg

Msanii wa bongo Muvi Elizabeth Michael (LULU) akipiga selfie kwa TECNO CAMON 16s

Akibainisha baadhi ya sifa za simu hiyo Mkomoye amesema TECNO CAMON 16s ina kioo kikubwa chenye inchi 6.6, kamera nne nyuma na huku kamera kuu ikiwa na 48MP, amesema ukubwa wa kamera hiyo unaiwezesha Camon 16s kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu ikiwezeshwa na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI.

Image 2.jpg


Mwonekano wa mbele na nyuma wa TECNO CAMON 16s


“Pamoaja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu TECNO CAMON 16s ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM. Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwamakwama” Aliongeza Mkomoye.

Image 3.jpg


Mtangazaji Omary Tambwe katika pozi akipiga selfie kwa ktumia TECNO CAMON 16s



Image 4.jpg


Mlimbwende Jihan Dimack na Muigizaji Lulu wakitazama selfie zilizopigwa na TECNO CAMON 16s.



Akiwatambulisha mabalozi wa TECNO CAMON 16s, Mkomoye alisema mabalozi hao watashirikiana na kampuni hiyo ili kurahisisha kufikisha ujumbe kwa wateja na watu wote wanaopenda kutumia simu zenye teknolojia ya kisasa. Mabalozi hao ni pamoja na Omary Tambwe, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye ni msanii wa bongo muvi pamoja na Miss University Bi. Jihan Dimack.

Kufahamu zaidi ujio wa simu hii bofya link kwenda kwenye ukurasa wao wa Instagram;

https://cutt.ly/VgDoVDQ
 
Ingependeza zaidi kama mngeweka hizo picha za selfie kutoka kwenye hiyo simu ili wadau watathimini zaidi
 
bei elekezi ni Tsh 400,000/= simu imefika mikoani kote, je wewe unapatikana mkoa gani tukupatie jina la duka utembelee
 
Internal storage 128 gb
Ram 4 gb

Kweli tekino ni upuuzi mtupu... Wangeweka hata ram 6 basi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom