- Source #1
- View Source #1
Wanaukumbi.
Baraza la ma askofu TEC linaomba Msaada lisaidiwe na serikali.
Maombi yakikataliwa wananua.
Hali tete leo hii ndiyo wanamtambua Rais Samia wanaomba msaada, Rais Samia achana na hawa wamezoe kudekezwa waendelee kutoa matamko.
Wasubiri umalize muda wako pesa hamna zinapelekwa kwenye miradi ya taifa

- Tunachokijua
- Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ni baraza la maaskofu wa katoliki nchini Tanzania abalo lilianzishwa rasmi mwaka 1956 na kutambuliwa na seikali mwaka 1957.
Madai
Mdau mmoja amechapisha video inayomuonesha Askofu wa Kanisa katoliki akitoa hotuba yake mbele ya Rais Samia Suluhu Hassa, na kueleeza kuwa ni ya mwaka 2026 ambapo baraza hilo linaomba msaada kwa Rais.
Uhalisia wa video hiyo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video iliyotumka si ya mwaka 2026 kama inavyoelezwa bali imetumika kwa lengo la kupotosha.
Kwa kutumia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia Juni 25, 2021 ambapo Tumaini TV ilichapisha video hiyo kupitia mtandao wao wa Youtube.
Na aliyekuwa akiongea kwa wakati huo alikuwa ni Rais wa TEC Mhashamu Gervas Nyaisonga ambapo alimueleza Rais mambo mbalimbali ikiwemo kuomba taasisi zao za elimu zirudishiewe hahi yake ya kudahili.
Kwa sasa Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania si Nyaisonga tena bali ni Mhashamu Askofu, Wolfgang Pisa ambaye hakuna kumbukumbu zozote zinazomuonesha kuwa alizungumza mbele ya Rais na kuomba pesa.