Team michepuko inawahusu

Michepuko ina easy stress jamani ila tuifanye kwa uangalifu!
 

Kwanza sijatoka povu Excel, pili kwa vile umekomaa sana mpaka naona unatoka unga unga kwenye k..pa basi natoa mwongozo kidogo.

Nini maana ya michepuko? Ni ile tabia ya kuwa na kufanya mapenzi na watu tofautitofauti. Kwa mfano, bwana Excel ameoa na ana mke aitwaye Maimuna, halafu Excel huyo huyo aanzishe mahusiano ya kimapenzi yenye kuhusisha ufanyaji wa mapenzi/ngono na Asha, Mwajabu, Pili, Katarina n.k. Hii ndiyo tunaita MICHEPUKO>

Nini kinapelekea watu wawe na michekupo? Tukitoa sababu za kuchumi kwa jinsia zote, sababu ambazo zinapelekea wao kuchepuka ni TAMAA ZA MWILI na KUTORIDHISHWA KIMAPENZI NA WENZI WAO WA NDOA. ILA hakuna tatizo lisilotatulika, huridhishwi na mkeo/mumeo mfundishe jinsi gani akuridhishe na utaridhika! Kwa wenye tamaa, nadhani wanajiendekeza tu, hivi kama unauwezo wa kujizuia usitoe hewa chafu mbele za watu, unashindwa kutawala tamaa zako za mwili? Wewe ni binadamu una akili na utashi na sio MBWA ambae hana uwezo huo!

Kwa nini tunasema michepuko sio dili? Hebu fikiria wewe mwanaume ambae umeoa na una wanawake wengine watatu, ambao nao pia wana wanaume wao, ambao nao pia hao wanaume inawezakana pia nao wana wanawake wengine, then mnatengeneza kitu kinaitwa MTANDAO WA NGONO. Hatari ipo pale ambapo katika mtandao huo unakuwa si wa ngono salama, yaani watu wanaenda bila kinga! Hapo ndipo tunasema michepuko sio dili kabisa kwani ni rahisi sana kuata maambukizi. Tulia na mmoja uepuke ukimwi na magonjwa mengine.

KUEPUKA MICHEPUKO INAWEZEKANA KABISA!! Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu (huku na wewe ukiwa mwaminifu), elezaneni hisia zenu kwa uwazi, kama huridhishwi na mwenzi wako mweleze ukweli na mwelekeze nini afanye uridhike.

Kama wote tutakuwa na hofu ya Mungu (maana amekataza uzinzi) na tukaogopa hili gonjwa hatari basi wote tutabaki njia kuu then tutaokoa kizazi chetu dhidi ya janga hili.
 

hapa sawa mkuu WALIMWEUSI..

endapo ungemwaga desa kama hili pale kwenye thread, mambo yangeenda safi kabisa!

unajua unapofanya utafiti ama unapoenda mahalai fulani kuchunguza tatizo lililopo kule, ukienda na negative approach, hutoweza kupata majibu chanya...

asante lakini kwa mchanganuo mzuri...
 
Last edited by a moderator:
Watu na mautundu yao! Mtu ana mke wa ndoa mmoja, nyumba ndogo mbili na one night stand kibao. Akina mama wa nyumbani ndo daaah, kaka we gengeni, muuza mkaa, muuza maji, kaka wa urembo, dalali n.k.
 
Mmmhhh walio na michepuko hawatakuja humuu
 
Mmmhhh walio na michepuko hawatakuja humuu

Yaani kweli inasikitisha! Mtu kapata mchepuko leo, kesho wanaenda kugegedana, tena unakuta mwanaume anajisifu eti niliend ch...! Ptuuuuuuuuuu! Kweli kuna wanaume na wanawake majasiri! Mtu umemjua leo, kesho unaenda kumnanihiiii! Aisee SIO DILI KABISA!Mnajiua hivi hivi.
 
Michepuko dill yani niache kuchuliwa kuogeshwa kwa maji yenye viungo??kisa tangazo! Na rudi home nakuta umevimba kama umetiwa ndimu...kisa? Mwambie wa kwako aache michepuko siyo wawengine.

hahahaha mkuu mkuu kweli we bazazi, mi naamini siyo dili, japo njia kuu ina foleni na mikingamo kibao suna siyo mbaya
 
ndugu yangu wewe usifanye hivyo Mungu apendi kabisa

hata kama umeninuwa na mkeo ndo umcheat kiasi hicho hujui unajiletea maangamizi yako jamani?

rudi kwenye njia kuu rafiki

Michepuko dill yani niache kuchuliwa kuogeshwa kwa maji yenye viungo??kisa tangazo! Na rudi home nakuta umevimba kama umetiwa ndimu...kisa? Mwambie wa kwako aache michepuko siyo wawengine.
 
jamani jamani msifanye hivyo hamjui kuwa Mungu afurahishwi na kitendo hicho
kwani ukikaa na mkeo kuna tatizo gani kwani mpaka umcheat amekukosea nini?
kwanini hjamani mnakuwa hivyo?

hahahaha mkuu mkuu kweli we bazazi, mi naamini siyo dili, japo njia kuu ina foleni na mikingamo kibao suna siyo mbaya
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…