TCU yavifuta vyuo vikuu vya TEKU na SJUT na kusitisha mafunzo kwa vyuo vikuu 5

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
TCU imevifuta vyuo vikuu viwili kikiwemo cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha Tabora na Mtakatifu Yohana (SJUT) cha Msalato Dodoma. Tume imeamuru wanafunzi waliokuwa wanasoma vyuo hivyo kuhamishwa kabla ya kuanza muhula wa mwaka wa masomo 2018/19. Pia mesitisha utoaji wa mafunzo kwa vyuo vikuu 5 nchini.

-------------

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo vitano na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo katika vyuo hivyo kuhamishiwa vyuo vingine.

Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 25,2018 jijini Dar es Salaam amevitaja vyuo hivyo kuwa nChuo Kikuu cha Mlima Meru, Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB) na Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga (ETU).

Vingine ni Chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta- Kituo cha Arusha (JKUAT- Arusha Center na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo) cha Bukoba mkoani Kagera.

“Vyuo hivi viko chini ya uangalizi maalum na hivyo hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo kuanzia astashahada, stashahada, shahada, shahada ya uzamili hadi shahada ya uzamivu kwenye programu za masomo,” amesema.

Profesa Kihampa amesema TCU imevifuta vyuo vikuu viwili vya Theophil Kisanji cha Tabora na Mtakatifu Yohana cha Msalato jijini Dodoma.

TCU imeviagiza vyuo hivyo kuwahamisha wanafunzi kabla ya kuanza kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Katibu mtendaji huyo amesema TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote kwenye vyuo saba.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian (MARUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kadinali Rugambwa (CARUMUCo).

Vingine ni Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastina Kolowa (SEKOMU), Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania- Kituo cha Marko (SJUT- St. Mark’s Center) na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).

“Vyuo hivi pia viko chini ya uangalizi wa Tume, vitaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo,” amesema Profesa Kihampa

“Tume imevitaka vyuo vikuu vyote vilivyotajwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo. Tume inawaarifu wanafunzi wote wanaotakiwa kuhama kuwasiliana na vyuo vyao kwa ajili ya maelekezo kuhusu taratibu za kuhama na vyuo wanavyotakiwa kuhama.”

Chanzo: Mwananchi

8fa424ba-c772-4a22-9477-ab3d4454b750.jpg
 
TCU imevifuta vyuo vikuu viwili kikiwemo cha Theophil Kisanji (TEKU) cha Tabora na Mtakatifu Yohana (SJUT) cha Msalato Dodoma. Tume imeamuru wanafunzi waliokuwa wanasoma vyuo hivyo kuhamishwa kabla ya kuanza muhula wa mwaka wa masomo 2018/19. Pia mesitisha utoaji wa mafunzo kwa vyuo vikuu 5 nchini.

Taarifa yako haina mashiko......Weka chanzo
 
Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo vitano na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo katika vyuo hivyo kuhamishiwa vyuo vingine.

Back
Top Bottom