VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Katika kile kinachoonekana kama udhalilishaji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hasa Kitivo cha Sheria),Mamlaka ya Vyuo Vikuu Nchini almaarufu kama TCU imewapanga wanafunzi wenye Daraja la pili kusomea Sheria Chuoni hapo. Nyaraka nilizonazo zinaonesha kuwa wapo wanafunzi wenye Daraja la pili la alama 10 waliochaguliwa chuoni hapo.
'Huu ni udhalilishaji. We ought to have a Cream of the Nation,as we always do' alisema mmoja wa Waadhiri Waandamizi chuoni hapo. 'Tutaona namna ya kubaki na tuwatakao darasani,wacha waje' aliongeza Mhadhiri huyo.
Ifahamike kuwa UDSM ilikuwa ikiishia Daraja la kwanza la alama 8 la Kidato cha sita. Kitivo cha Sheria cha UDSM ndicho cha kwanza katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na kimekuwa na wivu wa kutunza heshima yake kwa kuchagua wanafunzi wenye ufaulu wa juu sana. TCU,ambapo yumo Mkuu wa Kitivo hicho zamani Prof.Sifuni Ernest Mchome,imefanya kusudi? Hapa si kuwatafutia matatizo wanafunzi kwakuwa wengi 'wataliwa vichwa'? Yangu macho na masikio...